Tuesday, June 28, 2011

VINJARI ZA MSIMU WA DHAHABU JIJI LA SANGARA

"Kwa faida ya wale wasio na kawaida ya kumgeuza samaki kutokana na mila zao walizojiwekea agiza samaki mbili namna hii, kisha kula ile pande iliyo juu ya samaki w0te - Of coz utakuwa umekula samaki kamili,BASSSi!" Says Adam Mchomvu aka Baba Jonii

Nguli wa muziki wa Ragga na Dancehall Shaggy ameondoka leo jijini Mwanza majira ya saa 6 kuelekea Dar es salaam ambapo atapanda pipa jingine kurudi kwao.

Awali alitembelea vivutio vya utalii vilivyoko jijini Mwanza kama vile Bismark Rock, sehemu za biashara kuu ya zao la samaki, hifadhi ya makumbusho ya tamaduni za wasukuma iliyopo Bujora na halikadhalika sehemu zote za vivutio mwambao wa ziwa victoria.

Amesifia mazingira mazuri ya jiji la Mwanza, makaribisho aliyopata toka kwa waandaaji Prime Times Promotion na mashabiki wa Mwanza.

Mie na best female vocalist wa bendi ya Shaggy aitwaye Aisha

CEO wa blogu hii na Shaggy

Wednesday, June 22, 2011

ZIMEBAKI SIKU TANO TU! HAINA MAJOTROOOOO!!!!

'''Chuki zenu hatuzisikii, hatuongei, na wala hatuoni....EEeeeh'''

Paparazi.

Ni pilikapilika za show kubwa kuliko zote hapa nchini SERENGETI FIESTA 2011 inayoanzia jiji la Miamba Mwanza 'Mtu mzima Shaggy in tha house' siku ya jumapili ya tarehe 26 juni pichani toka shoto ni Zamaradi, G.Sengo na Baba Johnii aka Mchomvu ndani ya 88.1 leo mchana.

Street pande za Kirumba Mwanza.
Wakazi wa Rock City wameonekana katika pilika za huku na huko madukani kujinunulia mavazi kuhakikisha kuwa wanashaini ile kisawasawa kuilaki burudani ya kweli ile hali upande wa watoa huduma mbalimbali iwe za mahoteli, malazi, chakula, wadau wa usafiri maduka ya mavazi na kadhalika wao wameahidi kutoa huduma safi katika kipindi hiki cha matayarisho hata kwa siku husika.

Tuesday, June 14, 2011

'SERENGETI FIESTA 2011 MWANZA NDIYO KWANZA'

Shaggy.

MBONA tayari imekwisha tambulikaaaa kwambaaaa.... Serengeti Fiesta 2011 'Mwanza ndiyo kwanza'. Nina maaanisha kuwa wakazi wa Mwanza ndiyo wamekabidhiwa funguo za Show za 'kufufuka mtu' za msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta.

Dhamana hii haijaja hivi hivi mwanawane' bali ni kutokana na utashi, mapenzi mema na makaribisho yenye thamani ya hali ya juu wayatoayo wakazi wa Rock City na Wilaya zake kwenye matukio ya Fiesta miaka yote....

Wakazi wa Mwanza husapoti muziki ladha zote, lakini jiulize ni muziki gani ulianza kushika kwa kasi na kukubalika hata leo na kuwarusha wengi!!!?
Wataalamu wa mambo watakwambia.. Ni Ragga, Dancehall na Reggae (ingawa reggae kilimanjaro grafu zinasoma juu kinoma) Tehe!! Lakini ukizungumzia Dancehall na Ragga->Mwanza ni Nowmaaaa!!!

SASA ANAKUJA MKALI WA RAGGA & DANCEHALL
Mr. Lover-lover/Mr. Romantic & Fantastic true jamacian rasta ilve ur music 'Shaggy' anatua Mwanza, siku ya Tukio ikiwa ni JUMAPILI ya tarehe 26juni2011 katika Uwanja wa CCM Kirumba uliopo wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.It's nice and cool man, Shaggy Welcome to Mwanza!!..........
Coz Mwanza Haina Majotrooo!!,
@ g.sengo

HATIMAYE MOYO WANGU YA PHILBERT KABAGO YATINGA SOKONI!!!

Kabago.
Mkali wa michano kutoka The Rock City Mwanza, ambaye vilevile ni prizenta wa Passion Fm, Philbert Kabago ameshusha rasmi mtaani kitu cha album. Blogu hii imefanikiwa kuchonga na mshtaa' na hiki ndicho alichosema- "Album imetoka rasmi, so na hii ni baada ya kuwa katika maandalizi makubwa, nimeamua kuiachia album hii yenye jina 'Moyo wangu' ikiwa na ngoma kibao za ukweli kama vile 'Dear', 'Moyo wangu' ambayo imebeba jina la album, 'mama' alioimba kumuenzi marehemu mama yake, wivu, 'Umeme wa mgao' ambayo ndio inayotamba kwa sasa kwenye baadhi ya vituo vya radio n.k"

Dj Ali D akishusha mibaraka kwa album.
Kuhusu wasanii aliowashirikisha katika album hiyo jamaa amefunguka kwa kusema kuwa ni pamoja na Farida, MB Dog, Mr hill, Hussein machozi, G.Sengo na wengine wengi. Album imefanyika katika studio mbalimbali zikiwemo Tetemesha Records, Mo Record za mwanza na Family studio Arusha! Wasambazaji ni GMC.

Thursday, June 9, 2011

Shhhhhhhhhhh, ITAFAHAMIKA TU MUDA SI MREFU!!!!

Kuna tetesi kuwa huyu mjamaa kutoka the gunners Arsenal ya pale Emirates Uingereza huenda akatua Manchesta Yunaited, teh teh teh, kocha wake Arsene Wenger hataki kumuweka sokoni na hasa kwa mashetani hao wekundu, ila ye mwenyewe sasa msikie hapa akihojia na TF1 Telefoot huko kwao Ufaransani-"Do I want to go to Man United? Initially, we should see if it's real and if it is concrete." MMMMh!

Imelipotiwa kuwa Arsenal imeshindwa kumshawishi nahodha Cesc Fabregas kubaki,na badala yake anaonekana siku zake zimewadia kurudi klabu yake ya zamani Fc Barcelona.
Meneja wa washika bunduki Arsene Wenger amemruhusu kuondoka lakini haruhusiwi kujiunga na vilabu vya England.

THUG LOVING!

Rapa ja rule hatimaye amejisalimisha mwenyewe mahakamani huko manhattan na ataanza rasmi kutumikia kifungo cha miaka miwili jela akikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na silaha aina ya bastola. Kabla hajaingia kortini ja alionekana akisaini autographs za mashabiki wake nje ya mahakama huku akiwaaga"see you in 18," akaongeza na neno"one love",akapigwa pingu huku akiiangalia familia yake akiwemo mama yake,mke wake aitwaye Aisha ambao wote walikuwa wakilia kwa huzuni,kwa pamoja wakamwambia"LOVE YOU".Bongoshega inasema"tutakukumbuka ja rule coz ulikuja bongo na ukatupa burudani ya ukweli".WE'LL BE MISSING U NEGRO!

WAPI KUFULI FAZA?


Watoto siku zote wana maisha ya tofauti sana.Waacheni waje kwangu maana ufalme wao ni wa mtu kama mimi!