Saturday, December 29, 2012

TASWA YAFANYA MKUTANO MKUU NA WANACHAMAWAKE BAGAMOYO MKOANI PWANI.


Baadhi ya wanachama wa TASWA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete. 

Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akizungumza katika mkutano Mkuu leo 

Baadhi ya wanachama wa TASWA wakiburudika katika hotel kubwa mjini bagamoyo ya Kiromo view Hotel jana usiku kutoka kushoto ni Somoe Ng'itu, Hadija Khalili' Zena Chande na Angela Msangi

Shafii Dauda akiwa na dada Asha Muhaji. 

Mmiliki wa blog ya Bongo Staz Mahmud Zubeir kulia akizungumza na Wiliam Chiwango na Salim Said Salim

Mjumbe wa mkutano huo, Rajabu Mhamila 'Super D' akijitambulisha kwa mgeni rasmi

 
Ni wanachama wa TASWA wakisikiliza mada mbalimbali.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete walipokutana katika mkutano mkuu wa Taswa

 

Mmoja wa waandishi wa habari Egbert Mkoko akitoa salamu kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TASWA. 


Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akitoa neno la shuklani kwa wajumbe waliohuzulia mkutano wakati wa kufunga mkutano huo.

Mwanachama wa Taswa Saleh Ally akichangia mada wakati wa mkutano huo.

 
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete pamoja na mweka hazini wa TASWA Sultani Sekilo walipokutana katika mkutano mkuu wa Taswa

 Picha na www.burudan.blogspot.com

Thursday, December 27, 2012

MH. LAMECK AIRO NA MIKAKATI YAKE KUKUZA ELIMU JIMBO LA RORYA.



Mbunge wa Rorya Lameck Airo akifanya uzinduzi rasmi wa shule ya msingi kata ya Kirogo yenye madarasa mawili tu huku mengine mapya yakiendelea kujengwa kwa nguvu ya wananchi pamoja na sapoti ya mbunge huyo kama sehemu ya kusapoti maendeleo ya elimu wilaya ya Rorya mkoani Mara. 

Hatua yapili kuelekea kuona kibao cha uzinduzi. 

Hatua hii nifaraja kwa wananchi wa kata ya Kirogo kwani ni safari kuelekea kuisaka elimu bora yenye manufaa kwa watoto waishio maeneo ya karibu katani humu.

Jiwe la msingi la jengo hili limewekwa na Mhe. Lameck Airo Mbunge wa Wilaya ya Rorya tarehe 21/12/2012.

Uhaba wa madawati katika shule nyingi za msingi na sekondari nchini umeendelea kuumiza vichwa vya wengi wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla hali iliyomlazimu mbunge Lameck Airo kujisukuma kuchangia madawati kama inavyoonekana pichani ndani ya moja ya madarasa haya.

Mara baada ya kufanya ufunguzi kwa shule hiyo Mhe. Mbunge Lameck Airo alizungumza na wananchi wa kata hiyo kuweka msisitizo kwa masuala kadhaa ikiwemo matunzo ya majengo ya shule, ukarabati wa kila mara, kuhamasisha elimu na uboreshaji wa michezo.

Wananchi wa kata ya kirogo wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wao kwenye kusanyikohilo.

Mzee kiongozi wa kata hiyo akimkabidhi Mhe. Mbunge Lameck Airo zawadi ya kuku dume (Jogoo) kuafiki mchango wake katika maendeleo ya kata ya Kirogo. 

Mmoja wa akinamama wa kata ya Kirogo akijidai na vazi lake kusanyikoni.

Katika kuchangia na kuendeleza michezo ndani ya kata ya Kirogo Mbunge wa Rorya Mhe. Lameck Airo aliikabidhi mipira kwa Captein wa timu ya Cheleche Fc George Fabian (kushoto) kama hamasa kwa timu hiyo iliyo moja ya timu zinazofanya vizuri katika uwakilishaji kata hiyo kwenye kandanda.

Wednesday, December 19, 2012

Mh. Lowassa azindua josho la kisasa kwa mifugo kijiji cha Mfereji Monduli Juu

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo katika kijiji cha Mfereji Monduli juu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikaribishwa kwenye kijiji cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu,mara baada ya kuzindua josho la kisasa la Mifugo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Mifugo ikiingizwa kwenye Josho hilo,mara baada ya kuzinduliwa.
Wakazi wa kijiji cha Mfereji,Monduli juu wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati wa hafla ya uzinduzi wa josho la kisasa katika kijiji cha Mfereji Monduli juu. ambapo ametoa wito kwa wakulima na wafugaji nchini kuacha uhasama wa kugombea ardhi.

Amesema kuwa kila mtu ana haki yake hivyo ni muhimu kwa jamii hizo kuheshimiana na kukaa pamoja kutatua tatizo la ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo pamoja na kilimo.Kumekuwa na matokeo mengi sehemu mbalimbali ya kupigana kuwania ardhi kati ya wakulima na wafugaji, miongoni mwa maeneo hayo ikiwa ni mkoani arusha.

Amewaambia watu wa jamii ya kimasai ambao ni wafugaji kuingia katika ufugaji wa kisasa utakaowazuia kuhama hama kutafuta malisho ya mifugo yao.''Jamani watanzania wenzetu hawatakubali mtakapovamia maeneo yao bila ya ruhusa ni lazima tuondokane na tabia hii'' alisema.

Tuesday, December 18, 2012

MAKAMUZI YA SKYLIGHT BENDI NDANI YA KIOTA CHA THAI VILLAGE, DAR

Aneth Kushaba AK 47akiwajibika.
Mwanamuziki Mary Lukas akiimba sambamba na wadau SKYLIGHT Band ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar.
Maunoooo!
Vijana wa SKYLIGHT BAND wakiongozwa na rappa SONY MASAMBA wakikamua jukwaani.
Mwanamuziki Joniko Flower akiporomosha mistari sambamba na Mary Lucas.
 Mwanamuziki Mad Ice akiongea na mpiga gitaa wa bendi ya Skylight mara alipopewa nafasi ya kuimba.
Fundi Mitambo wa Skylight bendi akishow Love.
Marafiki.
Mwanadada Flora nae alikuwepo.
Kila mmoja akionyesha umahili wake wa kukata mauno.
Mambo ya pwani...
 Marafiki wakishow love.
 Wadau waliojitokeza kwa wingi kufurahia burudani.
Kazi kweli kweli...
Furaha ilitawala.
Blogger King Kif akiwa na Mwanamuziki Mad Ice.
Show Love
Mdau Mbogo (kulia) akishow love na rafiki yake.