Thursday, May 31, 2012

UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA

Kuanzia Alhamisi hii, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake. Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Masimba.

The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi, Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).

Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu; BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?

MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?

BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?

MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa

BC: Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka utotoni au la?

MM: Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk Show haikuwa ndoto yangu hapo awali. Lakini kama unavyojua,maisha huenda yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu. Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.

BC: Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania. Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini chanzo?

MM: Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha ha haaaa

BC: Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?

MM: Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio hapa tulipo hivi sasa.BC: Katika pitapita yangu ya mitandaoni nimesoma mahali kwamba Oprah ni miongoni mwa wanawake wanaokuvutia sana na yeye ni sababu mojawapo ya w ewe kuanzisha The Mboni Show ikiwa kama hatua mojawapo ya kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya. Kuna ukweli wowote katika hilo?

MM: Ni ukweli kabisa kwamba Oprah Winfrey ananivutia kupita kiasi. Pamoja na hayo show yangu haitokuwa ki-Oprah moja kwa moja. Sitaki na wala siwezi kumuiga kwa kila kitu. Ntakachofanya mimi ni kuchukua yale ambayo naweza kuyachukua na hususani kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania zaidi. The Mboni Show ni show ya kitanzania kwa ajili ya watanzania.

BC: Katika maelezo ya awali ya The Mboni Show umeeleza kwamba malengo ya show yako ni kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya watanzania. Mmejipanga vipi kufikia malengo hayo?

MM: Yaani Jeff you will be Suprised .Wewe subiri tu utajionea.Lakini ki-ukweli The Mboni Show imejipanga vilivyo. Nawaambia The Mboni Show ndio kimbilio la Watanzania na mwokozi wao ha ha ha ha

BC: Mlolongo wa kuanzisha TV show ni mrefu na bila shaka umepambana na vikwazo kadhaa mpaka kufikia hatua hii. Unaweza kunieleza kidogo kuhusu vikwazo ulivyopitia na kitu gani kilikuwa kinakupa msukumo kwamba endelea tu usikate tamaa?

MM: Jeff sio kitu rahisi kama watu wanavyofikiria. Mimi na timu yangu tumeanza production since April last year na imagine ndio kwanza tumemaliza juzi juzi.Ni wazi kwamba katika kutimiza lengo au azma hii nimepitia vikwazo vingi ambavyo kwa kweli nisingesimama imara ningeweza kabisa kukata tamaa. Lakini mwisho ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia mpaka kufika hapa. Kwa upande wa kitu ambacho kilikuwa kinanipa msukumo naweza kusema ni asili yangu ya kuwa mvumilivu na mbishi sana ninapotaka la kwangu. Hizo ndizo silaha zangu; uvumilivu na ubishi wenye manufaa. Vikwazo vilikuwa vingi sana ingawa sitopenda kuvitaja.Kwa ufupi nawaambia sio kitu kirahisi hata kidogo, ni kukomaaa tu mpaka kieleweke.

BC: Tunaposikia mtu anaanzisha kipindi cha televisheni kuna maswali kadhaa yanakuja. Je kitakuwa ni kipindi cha kurekodiwa ndani ya studio maalumu au kitakuwa kipindi cha kurekodiwa nje ya studio kwa maana ya mtaani nk. Kwa upande wenu format ya production ya The Mboni Show imekaaje?

MM: Kwa upande wetu tuna sehemu maalum ya kurekodia kama hii session ya kwanza vipindi vyote tulirekodia pale Serena( zamani ilikuwa ikiitwa Movenpick). Nawashukuru sana Serena kwa mchango wao katika kufanikisha hili. Next session itakuwa the same japo huwa tunatoka kidogo na kurekodi nje. Kuna mtu ambaye tumerekodi naye nje na hivi karibuni tunapanga kuingia mtaani. The Mboni Show ni kwa ajili yenu watanzania. Popote tutawafuata.

BC: Upo ukweli kwamba Hosts wengi wa TV show huwa yawabidi wawe na tabia ya kujisomea sana ili kupata mawazo na mitazamo mipya kila mara na kwenda na wakati. Je, na wewe pia una hulka hiyo au umejipanga namna gani katika kuhakikisha kwamba sio tu unakwenda na wakati bali unapata ideas mpya mpya za show nk?

MM: Kama nilivyogusia hapo mwanzo, siri yangu kubwa ni kuangalia kwa makini show za wengine zinafanywaje. Namuangalia mtu kama Oprah,Tyra, Monique, Hellen etc ili kupata mtazamo tofauti na ili niweze kuboresha show yangu kila mara. Sidhani kama ni lazima sana kusoma sana vitabu kwa sababu inategemea na aina ya show uliyonayo au unayoifanya.

BC: Mbali na hii venture mpya ya kuwa Host wa TV show, wewe ni mjasiriamali. Siku hizi, kama tunavyoona, wanawake wengi zaidi nao wanaingia kwenye ujasiriamali. Una ushauri gani kwa wanawake wenzio kuhusiana na ujasiriamali?

MM: Kwanza lazima ujue hiki kitu ” Fanya kitu ambacho unakipenda na unakiweza. Wanawake wengi tunakurupuka kwenye ujasiriamali na wakati hatuuwezi. Watu wanafanya kama fashion. Let’s say mimi napenda kuwa na Boutique kwa sababu napenda fashion na ninaimudu.Haya sasa nina talk show kwa sababu naipenda na ninaimudu. Kwa hiyo wanawake wenzangu, tujaribu kufanya kitu ambacho tunakipenda na kukimudu. Ni rahisi zaidi kufanikiwa ukiwa na hayo mambo mawili. Mapenzi kwa kitu unachokifanya au kutaka kukifanya na uwezo wa kukifanya.

BC: Mwisho una ujumbe gani mahususi kwa watanzania? Na pia kwanini mtu achague kuangalia The Mboni Show badala ya show zingine lukuki kwenye luninga?

MM: Ujumbe kwa watanzania wenzangu “Tupende vya kwetu, tuthamini vya kwetu, Tupendane na tushirikane. Kama unaona una connection na wewe huna uwezo nao ila kuna mwingine anaweza basi msaidie na sio kubaniana na kuoneana vijiba vya roho bila sababu za msingi.. Na pia tupende kusifiana. Mwenzako kafanya kizuri basi mpe hongera zake na kama kakosea basi muelekeze( muongoze). Ha ha ha ha Trust me The Mboni show iko kitofaut kabisa na zile tulizozizoea.  Kwenye The Mboni show unapata kila kitu. Full package ha ha ha ha.

Kwa mengi zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya The Mboni Show katika www.thembonishow.com.

Wednesday, May 30, 2012

MISS NYAMAGANA WATEMBELEA FURNITURE HOUSE

 Mwanadada Joyce Rewben wa Furniture House akiwaonyesha warembo wa miss Nyamagana bidhaa zinazouzwa ndani ya duka hilo lililopo ghorofa ya kwanza ndani ya Jengo la CCM mkoa wa Mwanza.

 Moja kati ya engo za furniture ndani ya duka hilo.

 Furniture House ambao ni moja kati ya wadhamini kinyang'anyiro cha miss Nyamagana 2012 kitakachofanyika ijumaa hii ndani ya Gold Crest Mwanza, pamoja na zawadi kutoka kwa wadhamini wengine, Furniture House itatoa zawadi ya sofa hili lenye thamani ya shilingi Milioni mbili na laki mbili kwa mrembo atakaye valishwa taji la Miss Nyamagana.

 Sofa at Furniture House.

 Warembo wakiwa wamesimama pamoja na wadau wa Furniture House ambao ni moja kati ya wadhamini wa Miss Nyamagana 2012. Walioketi ni Joyce Reuben (L) na Timilo Mohamed (R).
Mtangazaji wa Star Tv Abdalah Tilata (L) akiwa na Cameraman Baraka Samson wakiperuzi kwaliti' za view walizochukuwa eneo la tukio.
 Didi-daaaah..!

 Dush-waaa...!

 Zawadi nyingine toka TBL na STOPER ENTERTAINMENT kwa washindi wa Miss Nyamagana 2012 ni kama ifuatavyo mshindi wa tatu shilingi laki 2, mshindi wa pili lshilingi laki 3, wa kwanza ni shilingi laki 5 sambamba na Sofa kutoka Furniture House, mshindi wa nne hadi wa kumi kifutajasho cha shilingi 50,000/= kila mmoja na zawadi nyingine kibao toka kwenye category mbalimbali.

Monday, May 28, 2012

SHOW YA DIAMOND NDANI BIG BROTHER AFRICA 2012

STELLA AGUSTINO NDIYE MISS ILEMELA 2012-2013

Mshindi wa taji la miss Ilemela 2012 Stella Agustino (katikati) akiwa na mshindi wa pili Hapiness (kushoto) na mshindi wa tatu

Majaji miss Ilemela 2012.
Wadau katika pozi kushuhudia tukio...

Warembo walioingia kumi bora miss Ilemela 2012.
Sharowbarow President Bob junior akimalizaaaaa...
Flash na sehemu ya Gold Crest Hotel.

Mshiriki namba moja.

Mshiriki namba 2.

Mshiriki namba 3.

Mshiriki namba 9.

Mshiriki namba 4.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya toka jijini Mwanza Dogo Baraka ni sehemu ya burudani iliyowakonga wengi waliofika kushuhudia miss Ilemela akitunukiwa taji usiku wa tarehe 25/05/2012

Pichani huyu si mshiriki miss Ilemela 2012 bali ni sehemu ya Onyesho la mavazi ya Harusi toka Munira Classic.

Wadau wakichukuwa matukio.com hapa ni mwendo wa face book.

Onesho la mavazi ya harusi toka duka la mavazi ya harusi na sendof na urembo Munira Classic.

Mbunifu wa mavazi Munira akitambulishwa mbele ya umma uliojitokeza.

Mc wa tukio Mr. G. Sengo toka Clouds Fm Mwanza.
Meza ya majaji chini ikitafakari muonekano wa kwanza kupitia open show ya Miss Ilemela 2012.

Ze pipooo.

Wadadaz wakipata flash kwa blog....

Ni moja kati ya burudani zilizokuwepo kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka miss Ilemela 2012 anaitwa Anna kutoka nchini Namibia akicheza Belly Dance.

Hapa Chief Judge Muhksin Mambo toka Star Tv (nyuma ya mshiriki no 7) alipokuwa akitaja kumi bora.

Ze flawaz..

Kipaji toka moyoni mshiriki wa kinyang'anyiro miss Ilemela Stela akionyesha kipaji cha kucheza wimbo wa Fally Ipupa - Bakanja.

Mshiriki wa kinyang'anyiro cha Miss Ilemela  Hapiness akichora ndani ya kuonyesha vipaji.

Kipaji toka moyoni mshiriki Zaifath kipaji cha kuimba.

Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi mshindi nafsi ya 3 cheki ya shilingi laki mbili.

Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi mshindi wa nafsi ya pili Hapiness, cheki ya shilingi laki tatu.
Afisa Promosheni wa Nyanza Bottling Co. LTD watengenezaji wa soda jamii ya Coca cola Mr.Rutta, akimkabidhi Miss Ilemela 2012 Stella Agustino, cheki ya shilingi laki tano.

Tuesday, May 22, 2012

BOB JUNIOR KUPAMBA MISS ILEMELA 25/05/2012 IJUMAA GOLD CREST HOTEL ILE MWaaa!!!Producer Mkali, Rais wa wasafi mwenye kipaji cha uanamitindo, mwenye mvuto kwa mabinti, mwimbaji mwenye uwezo wa kuichezea sauti yake atakavyo, msanii ambaye tangu kuzaliwa kwake hajawahi kutengeneza video mbovu, msanii mwenye vipaji vingi kuliko wote, Rais wa Masharobaro Bob Junior ndiye atakaye tumbuiza katika Miss Ilemela 2012 .

Miss Ilemela itafanyika Ijumaa hii ya tarehe 25/05/2012 katika ukumbi wa Gold Crest jijini Mwanza. Kiingilio Miss Ilemela 2012 ni shilingi 20,000/= vitikawaida na VIP ambako kutakuwa na sapraiz kibao ni shilingi 40,000/= tu...
Akizungumzia juu ya sifa za wanyange wa Miss Ilemela mratibu wa kinyang'anyiri hicho Bi Ester Morris amesema kuwa warembo wa safari hii wanamvuto na sifa za kuwania taji loloteulimwenguni kwani ilifika wakati aliamua kubadilisha kambi na kutobainisha wapi ameweka kambi rasmi kwa warembowake kwa nia ya kuepuka usumbufu wa kutembelewa mara kwa mara na wadau wasiopitwa na vyenye mvuto.

Sambamba na burudani ya Bob Junior kinyang'anyiro hicho kitapambwa na onyesho la mavazi ya harusi, ufukweni, ofisini na mitoko mbalimbali yakionyeshwa na wadau spesheli. Wadhamini wa miss Ilemela mwaka 2012 ni Sahara Communication, Gold Crest Hotel, Lakairo Investment, Nyanza Bottling Co. LTD, Star Max Electronics, Dunia ya warembo na  G. Sengo Blog.

Thursday, May 17, 2012

PATRICK MAFISANGO OF SIMBA SC IS DEAD

Marehemu Patrick Mafisango (kwenye kiduara) katika picha ya pamoja na kikosi cha Simba enzi za uhai wake.
Mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda kiungo mkabaji Patrick Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari leo alfajiri katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam.
Hili ndilo Gari alilopatanalo ajali marehemu Patrick Mafisango maeneo ya TAZARA jijini Dar.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba bwana Aden Rage amesema kuwa taarifa za awali juu ya chanzo cha kifo cha mchezaji huyo zinasema kuwa mchezaji huyo amekutwa na mauti akiwa anaendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.

Msiba huu unakuja wakati kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda Milutin Sredovic 'Micho' akiwa amemteuwa kepteni wa zamani wa timu hiyo Hamada Ndikumana a.k.a 'Katauti' na Patrick Mafisango kujiunga na timu ya taifa hilo (AMAVUBI) kwaajili ya maandalizi ya nchi zitakazofuzu kwenda Brazil kwenye michuano ya Kombe la dunia 2014.

Kabla ya  kuichezea Simba mchezaji huyo alitokea Azam Fc ya jijini Dar es salaam.
Patrick Mafisango is dead.
Mwenyezi Mungu ilaze mahali pema peponi roho ya marehemu Patrick Mafisango.

Saturday, May 12, 2012

HONDA YAJISIMIKA KIBIASHARA ROCK CITY

Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akizindua tawi jipya la Kampuni ya Quality Motors Limited mkoani Mwanza, kampuni inayo jihusisha na usambazaji na uuzaji wa pikipiki, majenereta, na vifaa mbalimbali vya kampuni ya Honda nchini Tanzania.

Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akijaribu ubora wa moja kati ya mali zilizopo kwenye tawi hilo jipya huku akishuhudiwa na wadau wa karibu wa kampuni hiyo.

Ufunguzi wa tawi hilo utakuwa na manufaa mengi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwani wataondokana na adha ya nishati ya umeme ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika utendaji kazi wao wa kila siku hali inayosababisha kuingia katika gharama za ziada zinazokwamisha maendeleo kutokana na kipato chao duni, ikumbukwe kuwa wakazi wengi hususani wa visiwani hutumia majenereta kama chanzo cha nishati ya umeme kwa viwanda vya usagaji na ukoboaji nafaka, umeme wa majumbani maduka ya kuchaji simu, karakana za uchoeleaji na kadhalika.
Uzinduzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka ambapo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ukiendelea kuwa tegemeo kwa wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na tozo nafuu la nauli, hali inayo wafanya wananchi wengi kuufanya usafiri huo kuwa kimbilio lao

Mteja wa kwanza katika duka la Honda Mwanza bw. Vicent Hariah kutoka kampuni ya African Wheels and Tyres LTD akikabidhiwa pikipiki yake mara baada ya kuinunua.

Wateja wakipata maelezo toka kwa wahudumu na wadau wa Tawi la Honda Mwanza lililopo katika barabara ya Kenyeta karibu na tawi la Benki ya Posta.
Honda 'Best quality at Chinese price'

Honda at Quality Motors, Nyerere road Mwanza.

Sudhir Bargaonkar ni meneja masoko wa Kampuni ya Quality Motors Limited akimtembeza mgeni rasmi kwenye karakana ya tawi hilo jipya lililozinduliwa.

Wakitoka kwenye karakana ambapo pia katika duka hili spea mbalimbali za Honda iwe ni jenereta au pikipiki zitauzwa.

Picha ya kumbukumku... Hadi kufikia mwezi march 2012 halmashauri ya jiji la Mwanza ilikuwa na madereva wa pikipiki za biashara zaidi ya 6,000 wanaotambulika nao wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku.