Tuesday, August 27, 2013

SERENGETI FIESTA 2013 NDANI YA SINGIDA USIKU WA KUAMKIA LEO.
 

Msanii Muigizaji wa filamu na muziki wa bongofleva,Shilole pichani shoto akiimba mbele ya maelfu ya wakazi wa Singida waliojitokeza kwa wingi kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013,ndani ya Singida Motel.
 Sehemu ya umati wa watu wakishangilia burudani iliyokuwa ikiendelea kwenye kiota hicho cha Singida Motel.
 Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Sir Juma Nature akiwa na wasanii wenzake wa kundi la TMK -Wanaume Halisi,wakilishambulia jukwaa vilivyo.
 Anajiita Raisi wa Manzese,kutoka kundi la Tip Top Connections,Madee akiwaimbisha mashabiki wake,ndani ya Singida Motel wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea.
 Mashabiki waliokuwa wamejibanza ubavuni mwa jukwaa,nao walikuwa wakipata ile kitu roho inapenda kutoka kwa wasanii mbalimbali waliokuwa wakitumbuiza jukwaani.
 Pichani kulia ni Niki wa Pili na shoto ni kaka yake Joe Makini,wote ni wasanii wa muziki wa kizazi kipya a.k.a hip hop wakiwa sambamba na mtangazaji wa Clouds FM,Adam Mchomvu wakishangilia jambo nyumba ya jukwaa.
 Chumaaaa a.k.a Chid Benz akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani.
 Sehemu ya umati wa watu waliofika kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
 Anajiita mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiimba nyimbo zake za mahaba,mbele ya maelfu ya wakazi wa singida na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye tamasha hilo ambalo hufanyika mara moja kwa mwaka.
 Ommy Dimpo a.k.a pozi kwa pozi akiwa na madensa wake wakitumbuiza jukwaani
Kutoka kundi la Wanaume TMK,Chege na Themba wakilishambulia jukwaa
 Dj Mahiri kutoka Clouds FM,Dj Zero akifinya finya mashine zake kwa namna ya pekee kabisa,iliyokuwa ikiwafanya mashabiki kibao wazidi kuchenguka na kupiga mayowe kila wakati.
 Wenywewe wanajiita Makomando,wakilishambulia jukwaani kwa pamoja usiku hu0 wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea ndani ya Singida Motel.
Ni full kujiachia usiku huo ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,wengine wakiwa juu ya miti aaahhh nomaa sanaaa.!
 Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Singida wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huo kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013 linalofanyika kwenye viwanja vya Singida Motel usiku huu.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Petter Msechu akiwaimbisha mashabiki wake waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha la serengeti fiesta 2013  ndani ya Singida Motel.
 Ni ndani ya Singida Motel tamasha la Serengeti Fiesta 2013 
 Wasanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT,Lina na Amin wakilishambulia jukwaa kwa pamoja,huku wakazi wa Singida waaliofurika mwishoni mwa wiki ndani ya Singida Motel wakipiga mayowe ya shangwe.
 Amin Jukwaani akiwambisha mashabiki wake,huku mayowe kila kona yakisikika ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya Singida Motel,mkoani Singida.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Abdul Kiba akiimba jukwaani kwa hisia usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2013,ndani ya Singida Motel  mkoani Singida. 
Ni burudani Serengeti Fiesta nomaa sanaaa katika usiku huo.