African Stars Entertainment Tanzania(Aset) ambao wanajulikana kwa jina la “Twanga Pepeta” walikuwa kivutio cha sherehe za miaka 50 ya Uhuru London juzi Jumamosi. Kikosi hiki cha watumbuizaji maarufu wa Kibongo kilikaribishwa na Urban Pulse, Jestina George wakishirikiana na Ubalozi wa Tanzania mjini hapa. Twanga Pepeta katika picha ya pamoja na viongozi
Cllub 2000 palikua hapatoshi
Akiwakaribisha wote Balozi Kallaghe alisema sherehe za miaka 50 ni idhinisho kuwa Tanzania ni nchi ya amani inayostahili kuwa fahari yetu sote. “Waangalie Waingereza wanavyoorodhesha tarehe na mida ya majengo yao muhimu. Kutambua na kusherehekea muda kamili wa matukio ya jamii ni jambo muhimu na la kawaida,” alikumbusha kiongozi huyo na kupigiwa makofi.
Muda wa kusugua visigino
Makamuzi yakiendelea
Sekta ya kukaanga chips..Kikazi zaidi
Mh Balozi na Mama Balozi wakifungua mziki
Mh Chabaka na Mchumba wake wakicheza
Twanga wakifanya kweli
Kila mtu akifurahia show ya twanga
Na Freddy Macha
Watanzania wa kila rika, nasaba na taaluma walifurika toka miji ya Leeds, Bristol, Birmingham, Northampton, Milton Keynes na vitongoji mbalimbali kufurahia vigongo vya bendi hili lenye makao makuu Mango, Kinondoni Dar es Salaam. Ukumbi wa Club 2000 Banqueting Suite ulioko nyuma ya uwanja maarufu wa Wembley ulishuhudia tafrija hiyo wakati viongozi rasmi wa serikali walipofungua tafrija wakicheza nyimbo maarufu za Kitanzania kama ule wa mwanamuziki Salum Abdallah (“Wanawake wa Tanzania” na “Tujenge Nchi Yetu”) marehemu alizoimba mara baada ya Uhuru mwaka 1961.
Viongozi waliojumuika walikuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa, Mheshimiwa Aggrey Mwanri, Balozi wetu Uingereza, Mheshimiwa Peter Kallaghe, naibu wake Mheshimiwa Chabaka Kilumanga na Ofisa Habari ndani ya ubalozi,Mheshimiwa Amos Msanjila aliyehamasisha wageni kwa kunyofoa kinywaji cha “champagne” mahsusi kuzindua maadhimisho.
Kutokana na maombi mengi ya washabiki Twanga Pepeta itafanya Show ya pili siku ijumaa Tarehe 2 Desemba 2011 katika mji wa Milton Keynes kwenye ukumbi wa Golden Lounge, Unit 35 Barton Road, Bletchley Milton Keynes. MK2 3UH
Show hii imeandaliwa na Urban Pulse wakishirikiana na Miss Jestina blog.