Thursday, April 12, 2012

MWANZA YATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU JENERALI MSTAAFU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Ernest Ndikilo leo ameongoza Umma aliojitokeza kutoa salamu za rambirambi kwa mwili wa aliyewahi kuwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aliyefariki dunia siku ya Jumanne wiki hii akiwa na umri wa miaka 87 ambaye ameagwa rasmi leo jijini Mwanza.
Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro alizaliwa mnamo tarehe 1/01/1923 nakufariki dunia 10/04/2012.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikiro akimfariji mke mdogo wa marehemu Zainab Kiaro.
Mmoja wa wanafamilia (Kushoto) akimfariji mke wa kwanza wa marehemu Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aitwaye Penina Kiaro (Kulia).
Makamanda wakijadiliana.
Makamanda wakizidi kufurika eneo la tukio kutoa salamu zao za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Makamanda wakiwa eneo la juu katika kilima kidogo cha mawe ili kushuhudia ibada ya salamu za mwisho jijini Mwanza.
Safu ya Makamanda wengine.
Mwili huo ulitoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mchana na hatimaye majira ya saa saba ukaagwa hapa katika nyumba yake ya kikazi maeneo ya Kapripoint kabla ya kusafirishwa kuelekea wilayani Tarime mkoani Mara kwaajili ya Mazishi.
Kwa mwendo wa pole mwili ulipelekwa eneo rasmi.
Moja kati ya wanajeshi akiongoza moja ya vifungu kwenye ibada hiyo.
Mapaparazi.
Wakati wa kutoa heshima za mwisho uliwadia.
Jeshi la polisi usalama barabarani nao walikuwepo kutoa heshima zao.
Heshima...
Heshima ziliendelea kutolewa.
Makamanda wakipanga mikakati.
Mzee Gachuma katikati akifanya majadiliano na baadhi ya maafisa wa Jeshi.
Msafara.
Mwili wa marehemu aliye kuwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro umesafirishwa leo kuelekea wilayani Tarime mkoani Mara kwaajili ya Mazishi ambayo yatafanyika kesho.

Wednesday, April 11, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA KANUMBA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Msanii wa kike wa filamu Tanzania Elizabeth Michael Kimemeta maarufu kama Lulu,amefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwingine wa filamu Marehemu Steven Kanumba.

Amefikishwa mahakamani ikiwa ni siku nne, tangu alipokamatwa mara baada ya kifo cha msanii huyo ambaye inaaminika kuwa walikuwa na uhusiano wa Kimapenzi.

Mbele ya Hakimu mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam,Bi Augustina Mbando,Elizabeth Michael Kimemeta ajulikanaye kama Lulu kwa jina la Usanii,aliwasili mahakamani hapo akiwa chini ya Ulinzi mkali wa askari Polisi waliokuwa wamevaa kiraia na wengine wakiwa wamejihami kwa silaha.

Mara baada ya Kufikishwa mahakamani,upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa serikali Bi Elizabeth Kaganda ulimsomea shtaka moja ambalo ni la mauaji, kosa ambalo ni kinyume cha sheria ya kanuni ya adhabu kifungu cha 196.

Wakili huyo wa serikali Bi Elizabeth Kaganda,alidai mbele ya mahakama kuwa mnamo tarehe 07 mwezi April mwaka 2012,katika eneo la Sinza Vatican,msanii Elizabeth alimuua msanii Steven Kanumba.

Akiwa amevalia gauni kubwa lijulikanalo kama dera lenye rangi ya Njano mtandio wa rangi ya waridi na kandambili nyekundu mshtakiwa alionekana kutokuwa na wasi wasi pamoja uzito wa tuhuma za mauaji anayokabiliwa nayo huku akijibu maswali kadhaa kuhusu wasifu wake.

Msanii huyo alikanusha kuwa na umri wa miaka 18 baada ya kuulizwa ,ambapo yeye amesisitiza kuwa ana umri wa miaka 17, hii ikiwa ni tofauti na habari ambazo zimekuwa zikiripotiwa kuhusu umri wa msanii huyo ambaye sasa anatambulika kama mshtakiwa.

Kesi hii ya mauaji inatajwa kwa mara ya kwanza na mshtakiwa hakutakiwa kukiri wala kukana mashtaka.

Upande wa mashtaka umeieleza mahakama kuwa kesi bado iko kwenye upelelezi ambapo inatarajiwa kutajwa tena April 23 mwaka huu.

Mshtakiwa amepelekwa rumande hadi siku hiyo wakati kesi hii itakapotajwa tena.

Kwa upande mwingine tukio la kufikishwa mahakamani kwa mtuhumiwa huyo kumefanywa kwa usiri mkubwa na kufanya waandishi wa habari wengi wameshindwa kufuatilia kwa karibu tukio lenyewe.

Kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo na kusomewa shtaka la mauaji ya Kanumba kumetokea siku moja baada na Marehemu Steven Kanumba kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni.

Mazishi yake yalichukua sura ya kitaifa kutokana na umaarufu aliojijengea msani huyo katika jamii ya watanzania na hata nchi za nje.

Monday, April 9, 2012

TAMASHA LA PASAKA UWANJA WA TAIFA 2012

Upendo Kilahilo jukwaani.

Kundi la msanii John Lisu likitumbuiza live jukwaani.

Sehemu ya watu waliojitokeza kushuhudia Tamasha la Pasaka 2012,

Solomon Mukubwa na memba wake akiwapungia mkono wananchi.

Vinara wa muziki wa injili wakiingia eneo la tukio Uwanja wa Taifa huku wakitabasamu,kutumbuiza tamasha la pasaka 2012,kulia ni Christina Shusho, Upendo Kilahilo pamoja na Upendo Nkone wakiwa na watoto wao..

Msanii wa muziki wa injili, Rose Muhando wakati akiwasili Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kutumbuiza katika Tamasha la Pasaka la kwanza ambapo kesho shughuli nzima itaelekea katika mji wa Dodoma...

Cheza ndani ya Yesu...

Msanii wa Muziki wa Injili kutoka Afrika Kusini, Rebecca Malope (katikati), akiwa upande wa vyombo vya muziki kuweka mambo sawa muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani.

Ni raha tele....

Furaha inapozidi huna budi kusimama kuimba na kucheza....

PICHA NA www.fullshangwe.blogspot.com

MANENO YA MWISHO YA KANUMBA ALIYONENA KWA MAMA YAKE MZAZI JANA KABLA YA MAUTI.

Mama Kanumba anayeitwa Flora Mtegoa
Wakati Taifa la Tanzania likiwa katika majonzi mara baada ya kupoteza moja kati ya vijana wake walio peperusha vyema ndani na nje ya mipaka pendera yake kupitia tasnia ya Filamu STEVEN KANUMBA, yafuatayo ni mahojiano kati ya mdau wa blog ya G. Sengo mkoani Kagera mwandishi wa habari anayeitwa Nicolaus Ngaiza, aliyoyafanya na Mama Kanumba (Flora Mtegoa).
Mama yake Steven Kanumba (kushoto) akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na moja ya nduguze.
Katika mahojiano yaliyofanyika leo majira ya saa nane mchana katika uwanja wa ndege Bukoba katika harakati za safari kuelekea jijini Dar es salaam ILIKUWA HIVI:-
Nicolaus Ngaiza:- Mama unamwelezeaje Steven Kanumba katika kipindi cha uhai wake?
MAMA:- Kanumba mtoto wangu mtiifu, rafiki yangu, mpendwa wangu, mtotowangu wa karibu na jana niliongea naye kwenye simu na alfajiri naambiwa kafa.

Nicolaus Ngaiza:- Pengine alizaliwa sehemu gani mwaka gani?
MAMA:- Kanumba alizaliwa tarehe 8/1/1984 mkoani Shinyanga, katika hospitali ya Government Shy.

Nicolaus Ngaiza:- Baba yake yuko hai?
MAMA:- Baba yake yuko hai yuko Shinyanga anaitwa Charles Kanumba

Nicolaus Ngaiza:- Katika kipindi hiki kigumu unawambiaje watu wa Bukoba?
MAMA:- Naomba waniombee kwani hali yangu siyo nzuri kwani niko katika kipindi hiki kigumu.

Nicolaus Ngaiza:- Labda mama kijijini kwenu ni wapi?
MAMA:- Mimi natoka Wilayani Muleba, kata ya Izigo, kijiji cha Itojo.

Nicolaus Ngaiza:- Steven Kanumba sisi tunamjua kwa jina hilo jeh! hakuwa na jina la kinyumbani?
MAMA:- Hakuwa na jina lolote la kinyumbani zaidi ya hilo Kanumba la Kisukuma yeye ni msukuma.

Nicolaus Ngaiza:- Tungependa kujuwa neno la mwisho mlio weza kuzungumza pamoja.
MAMA:- Aliniambia mama natuma nauli uje tuagane naondoka naenda Marekani, akiwa mwenye furaha, tunataniana...

Nicolaus Ngaiza:- Labda aliwahi kukwambia ndoto zake katika maisha kwamba analenga kufanya nini?
MAMA:- Yeye ndoto zake ni kuendeleza sanaa yake na ninashukuru alikuwa amefika mbali kisanaa.

Nicolaus Ngaiza:- Labda kifamilia alikuwa ameoa au alikuwa na mtoto?
MAMA:- Hajawahi kuoa na hakuwa na mtoto...
SIKILIZA Clouds fm USIKU HUU SAUTI YA MAMA HUYU ITASIKIKA.
RIP ... STEVEN KANUMBA 'THE GREAT'