Wednesday, July 25, 2012

THE GREAT LAKE ZONE ENTERTAINMENT YATEMBELEA KISS FM MWANZA

Pressenter wa Kiss Kolabo Mix Show Ezden 'The Rocker'  mbele akiwa na wageni wake toka The great lake zone entertainmen leo asubuhi pindi walipotembelea kuelezea harakati mbalimbali za kundi hilo linalojihusisha na vipaji mbalimbali Rock City.


Mkurugenzi wa The great lake zone entertainment Fabian Fanuel (kushoto) akiwa na Meneja wake Albert G. Sengo walipotembelea studio za Kiss Fm Mwanza kuelezea mikakati mbalimbali na michakato inayotaraji kujiri siku zijazo sekta ya burudani jijini Mwanza.


Mratibu kitengo cha sanaa za maigizo na uchekeshaji wa majukwaani toka kundi la The great lake zone entertainment Smith Swai akifafanua jambo. 


Mratibu wa masuala ya Modoz'  Nanji akifafanua jambo jinsi sekta hiyo itakavyoshirikishwa pande za kanda ya ziwa.


Time to show love kwa flash Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Fabian Fanuel, mratibu Nanji, The Rocker (mwenyeji wetu) na mratibu Smith Swai.


Kwa flash kutoka kushoto ni Nanji, The Rocker, G. Sengo na Smith.

Monday, July 16, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 YAMALIZIKA KWA WAWILI KUTWALIWA TOKA MWANZA


Mwanza itawakilishwa na washiriki wawili tu katika mchakato wa kitaifa kutafuta washiriki watakaoingia kwenye kambi ya EBSS jijini Dar es salaam pichani ni majaji wa EBSS mwaka 2012 Master J, na Salama Jabir wakimkumbatia Madam Ritha (katikati) mara baada ya shughuli nzito kumalizika jana katika ukumbi maalum uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Madam Ritha akishow Love na Jamaa aliyeweka rekodi.... Bubu aliyejitokeza kwenye shindano na kushindana kuimba (search BUBU AFANYA KWELI EBSS MWANZA)

Kijana mdogo kuliko wote ambaye kama vigezo vya kubanwa na shule visingekuwepo na kwasababu EBSS inathamini Elimu, basi alikuwa na ushawishi mkubwa kwa majaji. 

Akifanya mahojiano mara baada ya kutoka chumba cha usaili.

Mmechisho umo-mo.

Washiriki walipata vinywaji bure toka Coca cola.


Waliochemsha walipataje shida kuzing'oa namba zao...

Full kujiamini... mstarini kuelekea usailini..

Thats wozup...


Kutoka Mwanza hadi Dar es salaam ni umbali wa kilimeta 1200 na  ni washiriki 1200 waliojitokeza kwenye usaili wa EBSS Mwanza, kati ya hao ni 8 tu ndiyo walionekana kuwa na kipaji toka moyoni wastani wa  kilometa 150 ndipo umpate mshiriki mmoja, lakini hatimaye wawili tu kati ya hao nane wakapatikana kuwakilisha jiji la Mwanza kutokana na wengine kukosa sifa.  Jeh hii inamaanisha kuwa Mwanza haina vipaji?

Sunday, July 15, 2012

YUSUF MANJI MWENYEKITI YANGA, MAKAMU WAKE CLEMENT SANGA

Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manjikulia na Makamu mwenyekiti Clement Sanga wakiwa katika uchaguzi huo jana
Habari kwa hisani ya dinaismailblogspot.com
Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:


Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji  (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%


Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%,  Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%


Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068),  Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)


kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama