Tuesday, May 3, 2011

WHO ARE THE SMARTEST ARTISTS IN BONGO?

Bila shaka ushasikia kwamba kuna maraisi,wenyeviti,makatibu wakuu nk wa usafi ndani ya Bongo hususani miongoni mwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya na wasanii wa filamu.Kuna misemo kama vile “masharobaro” na mambo kama “wauza sura” nk.Kuna maana nyingi katika majina kama hayo na pia kuna utata wa ki-lugha kuhusu maana halisi.Kuna vijembe kama vile “masharo uharo” nk nk.Usije sahau tafsiri ya Malkia wa Mipasho Bongo,Khadija Omar Kopa kuhusu neno au jina sharobaro.

Lakini Sarah kutoka Angalia Bongo anajaribu kuja na mtizamo tofauti kwamba u-smartness au umaridadi kama tulivyokuwa tukisema hapo kale kidogo,ni muhimu ukaenda na umaridadi wa kichwani na sio kuishia kwenye mwili na mavazi peke yake.Hapo ndipo anapojaribu kuja na orodha ya wasanii ambao ni SMART nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment