Monday, October 24, 2011

Mh Naibu Balozi Wa Uingereza Amvisha Pete Mchumba Wake

Mr Chabaka akitoa pete
PETE ambayo ni Diamond ya Ukweli
Wachumba wakiwa na baadhi ya marafiki zao na familia
Wapenzi wakiwashukuru wageni waalikwa.
Ni sherehe fupi ya kuvalishana pete ya Uchumba iliyofanyika Jumamosi Tarehe 22 Oktoba 2011 kati ya Naibu Balozi wetu Mh.Chabaka na Bi Irene. Sherehe hii ilihudhuriwa na baadhi ya ndugu pamoja na marafiki wa karibu waliojumuika kwa pamoja kushuhudia tukio hili muhimu katika safari yao ya kuelekea kwenye ndoa.

Vazi alilovaa Bi Irene limebuniwa na kutengenezwa ramsi na Anna Lukindo. Tarehe na pamoja taratibu zote za harusi zitatolewa rasmi muda muafaka utakapowadia.

Hivyo basi Blogu hii pamoja na Urban Pulse Creative na Miss Jestina George tunapenda kuwapa hongera na fanaka katika penzi lao na maisha yao ya baadae, Mungu Awabariki.

Sunday, October 23, 2011

ARUSHA YATIKISA VODACOM MWANZA CYCLE CHALLENGE 2011.

Picha kulia ni mkurugenzi wa Vodacom Tanzania Kanda ya ziwa Steven Kingu sambamba na mkuu wa udhamini Vodacom Tanzania George Rwehumbiza wakimkabidhi Mshindi wa kwanza wanaume Richard Laizer kutoka Arusha zawadi ya kitita cha shilingi milioni 1.5 baada ya kuwashinda washiriki wengine 400 kwenye mbio za baiskeli za Vodacom Mwanza Cycle challenge iliyomalizika leo jijini Mwanza na kudhaminiwa na Vodacom sambamba na SBL kupitia Malta Guinness na Redio Clouds.

Mshindi wa pili Mindi Mwangi kutoka mkoani Shinyanga aliyekuwa akitumia baiskeli ya kawaida tu hapa akipokea kitita chake.

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli wanawake kilomita 80 Sophia Husein akipokea kitita cha shilingi milioni moja toka kwa wadhamini.

Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Bia ya Serengeti SBL bw. Ephraim Mafuru akikabidhi zawadi kwa Zavalina Abel aliyeshiriki mbio za kilomita 10 zilizomalizikia katika vilima vya Bugando na hafla ya kukabidhi zawadi kufanyika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Si mnaona jamaniiii!!

Washiriki katika pozi.

Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Bia ya Serengeti SBL bw. Ephraim Mafuru kwa upande wake ametoa pongezi kwa chama cha baiskeli kanda ya ziwa kwa kazi kubwa ya kufanya mapinduzi kwenye mashindano hayo ya sita, kuyapendezesha na kuwa na mwonekano wa kitaifa zaidi.

Washiriki mbio tofauti katika pozi wakisikiliza yanayojiri.

Mashindano yalikuwa na kila sifa za kuvutia, vuta hisia kilomita 196 kwa baiskeli...Duh!!

Haaooo darajani...

Ajali nazo zimo hapa ziligongana kama baiskeli saba hivi....kisa utelezi wa ganda la ndizi.

Mtu kule baiskeli kule...!!

Pamoja na walume hawa kutumia baiskeli hizi za teknolojia hawakufua dafu... mbele ya washosha ng'ombe wazee wa shy.

Akitumia baiskeli isiyo na teknolojia (mfupa) mzeiya wa Shy akiovateki tena kwenye kilima...

Balaaa mwanawane, mzee mzima huyoooo....

Kulia mtu, kushoto mtu hapa ni kazi tu..

Hapa jeh!!

Kote tambarare, shughuli ilikuwa ni kukimaliza kilele cha Bugando...

"Isiwe tabu sheria si zinaruhusu, kwenye kilima to finito ... naikokota"


Kutoka kushoto ni Bukuku wa blogu maarufu ya Full Shangwe, Brand Manager wa Malta Guinness bw. Maurice Njowoka, Butunga wa TBC, Blogger maarufu Michuzi Jr na G.Sengo.

Thursday, October 20, 2011

KAMBI YA MAFUNZO MPIRA WA KIKAPU KUMALIZIKA LEO JIJINI MWANZA

Kocha Twalib Puzo akitoa maelezo kwa washiriki (hawako pichani) kuanzia kushoto ni Iddy Zuberi, Sosho Kizito, Twalib Puzo, Vicent Shinde katika mafunzo ya mpira wa kikapu kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18 kutoka katika shule mbalimbali za sekondari jijini mwanza, yakiendelea kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba na yanatarajiwa kumalizika leo saa 10 jioni katika uwanja huu.

Mafunzo hayo yameandaliwa na kusimamiwa na Shirika la kijamii la Planet Social development (PSD) la jijini Mwanza pamoja na Mambo Basketball kutoka Dar es Salaam yamejumuisha jumla ya vijana 81 ikiwa wavulana ni 68 na wasichana ni 13.

Mafunzo hayo yalikuwa na malengo yafuatayo:
1.Kuangalia vipaji na jinsi ya kuviendeleza katika kusaidia maendeleo ya mchezo huu hapa Tanzania ambao ni wito wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).
2.Kupata na kutoa picha halisi kwa wachezaji ikiwa ni sehemu ya mafunzo tutakayoyafanya mwakani kwa kushirikiana na kocha wa Basketball program ya Memorial Newfound University kutoka Canada. Hii ni baada ya mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwezi wa saba mwaka huu ambapo kijana wa ki Tanzania Alphaeus Kisusi alifanikiwa kupata “Partial Scholarship” kwenda kusoma katika chuo hicho.
3.Kubadilishana uzoefu na makocha wa mchezo huu hapa mwanza katika kuendesha mafunzo kama haya kwa siku zijazo.
4.Kuendeleza ushirikiano wa vikundi vyetu (Mambo Basketball na PSD) katika kutekeleza malengo tuliyojiwekea kama US Sports program Alumni baada ya safari yetu ya mafunzo nchini Marekani mwaka 2009 iliyogharamiwa na Ubalozi wa Marekani – Tanzania.

Washiriki kwenye training.

Mafunzo haya yanatarajiwa kufungwa na Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania ndg. Mussa Mziya akiambatana na mlezi wa vijana katika chama cha mpira wa kikapu Mkoa wa Mwanza ndg Altaf H. Mansoor “Dogo”