Kocha Twalib Puzo akitoa maelezo kwa washiriki (hawako pichani) kuanzia kushoto ni Iddy Zuberi, Sosho Kizito, Twalib Puzo, Vicent Shinde katika mafunzo ya mpira wa kikapu kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18 kutoka katika shule mbalimbali za sekondari jijini mwanza, yakiendelea kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba na yanatarajiwa kumalizika leo saa 10 jioni katika uwanja huu.
Mafunzo hayo yameandaliwa na kusimamiwa na Shirika la kijamii la Planet Social development (PSD) la jijini Mwanza pamoja na Mambo Basketball kutoka Dar es Salaam yamejumuisha jumla ya vijana 81 ikiwa wavulana ni 68 na wasichana ni 13.
Mafunzo hayo yalikuwa na malengo yafuatayo:
1.Kuangalia vipaji na jinsi ya kuviendeleza katika kusaidia maendeleo ya mchezo huu hapa Tanzania ambao ni wito wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).
2.Kupata na kutoa picha halisi kwa wachezaji ikiwa ni sehemu ya mafunzo tutakayoyafanya mwakani kwa kushirikiana na kocha wa Basketball program ya Memorial Newfound University kutoka Canada. Hii ni baada ya mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwezi wa saba mwaka huu ambapo kijana wa ki Tanzania Alphaeus Kisusi alifanikiwa kupata “Partial Scholarship” kwenda kusoma katika chuo hicho.
3.Kubadilishana uzoefu na makocha wa mchezo huu hapa mwanza katika kuendesha mafunzo kama haya kwa siku zijazo.
4.Kuendeleza ushirikiano wa vikundi vyetu (Mambo Basketball na PSD) katika kutekeleza malengo tuliyojiwekea kama US Sports program Alumni baada ya safari yetu ya mafunzo nchini Marekani mwaka 2009 iliyogharamiwa na Ubalozi wa Marekani – Tanzania.
Washiriki kwenye training.
Mafunzo haya yanatarajiwa kufungwa na Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania ndg. Mussa Mziya akiambatana na mlezi wa vijana katika chama cha mpira wa kikapu Mkoa wa Mwanza ndg Altaf H. Mansoor “Dogo”
No comments:
Post a Comment