Tuesday, June 14, 2011

HATIMAYE MOYO WANGU YA PHILBERT KABAGO YATINGA SOKONI!!!

Kabago.
Mkali wa michano kutoka The Rock City Mwanza, ambaye vilevile ni prizenta wa Passion Fm, Philbert Kabago ameshusha rasmi mtaani kitu cha album. Blogu hii imefanikiwa kuchonga na mshtaa' na hiki ndicho alichosema- "Album imetoka rasmi, so na hii ni baada ya kuwa katika maandalizi makubwa, nimeamua kuiachia album hii yenye jina 'Moyo wangu' ikiwa na ngoma kibao za ukweli kama vile 'Dear', 'Moyo wangu' ambayo imebeba jina la album, 'mama' alioimba kumuenzi marehemu mama yake, wivu, 'Umeme wa mgao' ambayo ndio inayotamba kwa sasa kwenye baadhi ya vituo vya radio n.k"

Dj Ali D akishusha mibaraka kwa album.
Kuhusu wasanii aliowashirikisha katika album hiyo jamaa amefunguka kwa kusema kuwa ni pamoja na Farida, MB Dog, Mr hill, Hussein machozi, G.Sengo na wengine wengi. Album imefanyika katika studio mbalimbali zikiwemo Tetemesha Records, Mo Record za mwanza na Family studio Arusha! Wasambazaji ni GMC.

Thursday, June 9, 2011

Shhhhhhhhhhh, ITAFAHAMIKA TU MUDA SI MREFU!!!!

Kuna tetesi kuwa huyu mjamaa kutoka the gunners Arsenal ya pale Emirates Uingereza huenda akatua Manchesta Yunaited, teh teh teh, kocha wake Arsene Wenger hataki kumuweka sokoni na hasa kwa mashetani hao wekundu, ila ye mwenyewe sasa msikie hapa akihojia na TF1 Telefoot huko kwao Ufaransani-"Do I want to go to Man United? Initially, we should see if it's real and if it is concrete." MMMMh!

Imelipotiwa kuwa Arsenal imeshindwa kumshawishi nahodha Cesc Fabregas kubaki,na badala yake anaonekana siku zake zimewadia kurudi klabu yake ya zamani Fc Barcelona.
Meneja wa washika bunduki Arsene Wenger amemruhusu kuondoka lakini haruhusiwi kujiunga na vilabu vya England.

THUG LOVING!

Rapa ja rule hatimaye amejisalimisha mwenyewe mahakamani huko manhattan na ataanza rasmi kutumikia kifungo cha miaka miwili jela akikabiliwa na mashtaka ya kukutwa na silaha aina ya bastola. Kabla hajaingia kortini ja alionekana akisaini autographs za mashabiki wake nje ya mahakama huku akiwaaga"see you in 18," akaongeza na neno"one love",akapigwa pingu huku akiiangalia familia yake akiwemo mama yake,mke wake aitwaye Aisha ambao wote walikuwa wakilia kwa huzuni,kwa pamoja wakamwambia"LOVE YOU".Bongoshega inasema"tutakukumbuka ja rule coz ulikuja bongo na ukatupa burudani ya ukweli".WE'LL BE MISSING U NEGRO!

WAPI KUFULI FAZA?


Watoto siku zote wana maisha ya tofauti sana.Waacheni waje kwangu maana ufalme wao ni wa mtu kama mimi!

Saturday, May 7, 2011

Al-Qaeda YATHIBITISHA KIFO CHA OSAMA

Al-Qaeda imethibitisha kifo cha kiongozi wake, Osama Bin aden, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kundi hilo na kutangazwa kupitia mitandao mbalimbali ya itikadi kali.Taarifa inayothibitisha kifo

Tarifa hiyo imesema damu ya kiongozi huyo "haitapotea" na kuwa al-Qaeda itaendelea kushambulia Marekani na washirika wake. Kifo cha Bin Laden kitakuwa "laana" kwa Marekani, na kutoa wito kwa Pakistan kuanza harakani, imesema taarifa hiyo.

Bin Laden alipigwa risasi na kufa siku ya Jumatatu, wakati makomando wa Marekani walipovamia nyumba yake katika mji wa Abbottabad nchini Pakistan.

Osama Bin Laden
Uvamizi huo ulifanywa bila ya mamlka za Pakistan kufahamu, na hivyo kuongeza mvutano kati ya nchi hizo mbili. Mikutano kadhaa ya hadhara inafanyika nchini Pakistan siku ya Ijumaa, kupinga hatua hiyo.

Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mitandao yenye itikadi kali imesema sauti ya kiongozi huyo wa al-Qaeda iliyorekodiwa wiki moja kabla ya kifo chake itatolewa hivi karibuni.


"Damu ya Osama Bin Laden itaendelea kubaki, kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, laana inayowafuata wamarekani na jamaa zao, itawafuata ndani na nje ya nchi zao," imeonya taarifa hiyo.

"Furaha yao itakuwa masikitiko, na damu yao itachanganyika na machozi. Tunatoa wito kwa Waisilamu wenzetu nchini Pakistan, ambao katika ardhi yao Sheikh Osama aliuawa, wasimame na kupambana." Waandishi wa habari wanasema Wapakistani wengi wamekasirishwa na kile wanachoona kama Marekani kuingilia uhuru wa nchi yao.


Pia wanaishutumu serikali ya Pakistan kwa kuruhusu makomando wa Marekani kufanya shughuli zao, ingawa maafisa wanakanusha kuwa walifahamishwa.

Karibu watu 1,000 walikusanyika katikati ya mji wa Abbotabad baada ya sala ya Ijumaa, limeripoti shirika la habari la AFP.

Walichoma moto matairi ya magari, kuweka vikwazo katika barabara kuu na kupiga kelele wakisema "Hapana Marekani" na "magaisi, magaidi, Marekani ni magaidi".

Hata hivyo mwandishi wa BBC mjini Rawalpindi amesema maandamano ya kupinga Marekani yalikuwa madogo kuliko yalivyotarajiwa, huku watu 50 wakijitokeza.


hisani ya bbc swahili

MOURINHO APEWA ADHABU

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amepewa adhabu ya mechi tano kwa mechi za Ulaya, kutokana na matukio wakati wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya, dhidi ya Barcelona.Chama cha soka Ulaya, UEFA, kimesema Mourinho alitoa matamshi "yasiyofaa", baada ya Real Madrid kufungwa 2-0 na Barcelona, akiwatuhumu waamuzi kwa kujaribu kuisaidia Barcelona.

Mourinho tayari ametumikia adhabu ya mchezo mmoja kukaa jukwaani, katika mchezo wa pili, na michezo mingine mitano itatekelezwa iwapo atafanya makosa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

UEFA pia imemfungia kutocheza mchezo wa fainali kipa wa Barca wa akiba Jose Pinto.