Thursday, July 14, 2011

WAREMBO 15 WA MISS LAKE ZONE HAWAHAPA!!


Tracy Sospeter (20) Shinyanga

Lydia Mlimi (21) Mara

Glory Samwel (19) Shinyanga

Violeth Paschal (18) Mara

Sylvia Anatory (19) Kagera

Jaanath Abdul (21) Kagera

Irene Karugaba (21) Mwanza


Jackline Dismas (20) Shinyanga

Nani kati ya hawa kutawazwa Miss Lake Zone 2011? Shughuli kufanyika ndani ya meli ya Mv Umoja jumamosi ya tarehe 23 july 2011 jijini Mwanza.

Monday, July 11, 2011

LUDACRIS KUTUA BONGO SHOW YA FIESTA 2011

Mwaka huu ndani ya tamasha kubwa nchini Tanzania (Fiesta) linamdondosha mtu mzima kutoka marekani Ludacriss ambapo show itakua ndani ya viwanja vya leaders. Kauli mbiu ya 'Fiesta 2011 ni Habari zenyu bana! Haina majotro!!' stay tuned na your favourite station Clouds fm.

PICHA ZA UKUTANI CLUB MPYA ZOO



Ni Club mpya jijini Mwanza yaitwa Victoria, ikipatikana katika bar kubwa ya wastaarabu Victoria Prince pande za Kirumba, yaani ni full house, yenye full service. Karibia pale!!

Wednesday, July 6, 2011

THE BEAT FESTIVAL

FRI 8TH JULY - 20.00 - 00.00

Venue: Triniti - Msasani rd. 26, Oysterbay, Dar es Salaam, Tanzania.

TBL YAZINDUA KAMPENI YA JIVUNIE UTANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania,Robin Goetzche akizungumza leo katika uzinduzi wa Kampeni ya Jivunie Utanzania inayoendeshwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Lager ikiwa ni harakati ya kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania.Kampeni hii imezinduliwa leo hii katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa,katikati ya Jiji la Dar na kuhudhuriwa na wageni mbali mbali.

Suleiman Nyambui akiwaeleza jambo waandishi wa habari.

Wakongwe wa Muziki wa dansi nchini pia walikuwa ni sehemu ya wageni waalikwa katika hafla hiyo.

Wachezaji wa zamani wa timu za mpira wa miguu wa timu za Yanga na Simba pia walikuwepo.toka kushoto ni Salvatory Edward,Kenneth Mkapa,Mohamed Mwameja na Edbil Jonath Lunyamila.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe akiwa katika mazungumzo na Mkuregenzi wa Bodi ya TBL, Arnold Kileo pamoja na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Ali Mwaimu.

Monday, July 4, 2011

FIESTA SHY TOWN

Pamoja na kuwa imekuwa chance yake ya kwanza kanda ya ziwa mchizan amekubalika kwa kushuka kiudiferenti zaidi, densi kali, mashairi taiti...yani nowma!.

Huyu ndiye yule Mc ambaye pia ni Prizenta...Eyo Mchomvu! akitupia pale kati kitu cha baba Jonii

Vipaji toka Shy Town pia vilipata nafasi kulikwea jukwaa.

Zamu ya Sajna sasa kulibeng'isha.

Mwasiti...

Wadau wa Shy Town na raha zao.

Mh. Temba akiimbisha..

Hawa jamaa kila walichokuwa wakigusa kiligeuka dhahabu kwa kupata shangwe za kutosha..

Aisee fundi, niongezee tafadhali!

Ndani ya mmimino kitu cha Serengeti....

Mahudhurio.

Moja kati ya watangazaji wa Jahazi Wasiwasi Mwabulambo (wa3 kutoka shoto) akiwa na wadau wa JAHAZI Shy Town.

Engo

Mtangazaji wa Faraja Fm Shinyanga Emmanuel S. Msigwa (shoto) na mshkaji wake.

Peace!! Wasiwasi huyoooo akisepa!

Shughuli iliisha kwa mbinde.. Huku wakiimba 'NGOSHAaaaa!! NGOSHAaaa!!' wakazi wa Shinyanga walikataa kata kata kuondoka eneo la tukio mara baada ya muda kuisha wakilazimisha 'Ngosha The Don' aendelee kutema madini kwenye stage, ilibidi polisi waingilie kati kumwondosha eneo la tukio.

Tuesday, June 28, 2011

VINJARI ZA MSIMU WA DHAHABU JIJI LA SANGARA

"Kwa faida ya wale wasio na kawaida ya kumgeuza samaki kutokana na mila zao walizojiwekea agiza samaki mbili namna hii, kisha kula ile pande iliyo juu ya samaki w0te - Of coz utakuwa umekula samaki kamili,BASSSi!" Says Adam Mchomvu aka Baba Jonii

Nguli wa muziki wa Ragga na Dancehall Shaggy ameondoka leo jijini Mwanza majira ya saa 6 kuelekea Dar es salaam ambapo atapanda pipa jingine kurudi kwao.

Awali alitembelea vivutio vya utalii vilivyoko jijini Mwanza kama vile Bismark Rock, sehemu za biashara kuu ya zao la samaki, hifadhi ya makumbusho ya tamaduni za wasukuma iliyopo Bujora na halikadhalika sehemu zote za vivutio mwambao wa ziwa victoria.

Amesifia mazingira mazuri ya jiji la Mwanza, makaribisho aliyopata toka kwa waandaaji Prime Times Promotion na mashabiki wa Mwanza.

Mie na best female vocalist wa bendi ya Shaggy aitwaye Aisha

CEO wa blogu hii na Shaggy