Saturday, May 12, 2012

HONDA YAJISIMIKA KIBIASHARA ROCK CITY

Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akizindua tawi jipya la Kampuni ya Quality Motors Limited mkoani Mwanza, kampuni inayo jihusisha na usambazaji na uuzaji wa pikipiki, majenereta, na vifaa mbalimbali vya kampuni ya Honda nchini Tanzania.

Mkuu wa wilaya Nyamagana Said Amanzi akijaribu ubora wa moja kati ya mali zilizopo kwenye tawi hilo jipya huku akishuhudiwa na wadau wa karibu wa kampuni hiyo.

Ufunguzi wa tawi hilo utakuwa na manufaa mengi kwa wakazi wa kanda ya ziwa kwani wataondokana na adha ya nishati ya umeme ambayo imekuwa kikwazo kikubwa katika utendaji kazi wao wa kila siku hali inayosababisha kuingia katika gharama za ziada zinazokwamisha maendeleo kutokana na kipato chao duni, ikumbukwe kuwa wakazi wengi hususani wa visiwani hutumia majenereta kama chanzo cha nishati ya umeme kwa viwanda vya usagaji na ukoboaji nafaka, umeme wa majumbani maduka ya kuchaji simu, karakana za uchoeleaji na kadhalika.
Uzinduzi wa tawi hilo umekuja wakati muafaka ambapo usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda ukiendelea kuwa tegemeo kwa wakazi wengi wa mikoa ya kanda ya ziwa kutokana na tozo nafuu la nauli, hali inayo wafanya wananchi wengi kuufanya usafiri huo kuwa kimbilio lao

Mteja wa kwanza katika duka la Honda Mwanza bw. Vicent Hariah kutoka kampuni ya African Wheels and Tyres LTD akikabidhiwa pikipiki yake mara baada ya kuinunua.

Wateja wakipata maelezo toka kwa wahudumu na wadau wa Tawi la Honda Mwanza lililopo katika barabara ya Kenyeta karibu na tawi la Benki ya Posta.
Honda 'Best quality at Chinese price'

Honda at Quality Motors, Nyerere road Mwanza.

Sudhir Bargaonkar ni meneja masoko wa Kampuni ya Quality Motors Limited akimtembeza mgeni rasmi kwenye karakana ya tawi hilo jipya lililozinduliwa.

Wakitoka kwenye karakana ambapo pia katika duka hili spea mbalimbali za Honda iwe ni jenereta au pikipiki zitauzwa.

Picha ya kumbukumku... Hadi kufikia mwezi march 2012 halmashauri ya jiji la Mwanza ilikuwa na madereva wa pikipiki za biashara zaidi ya 6,000 wanaotambulika nao wamekuwa wakiongezeka siku baada ya siku.

OBAMA ABARIKI NDOA ZA JINSIA MOJA

video platform video management video solutions video player Rais Barack Obama amesema kwamba watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana.
 
Bwana Obama amesema daima amekuwa mgumu kukubali kwamba wanaume na wanawake wenye uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja nchini Marekani watendewe haki na jamii kwa kutambua uhusiano huo, lakini amekuwa akipitia kile anachokiita mabadiliko ya kimtazamo kuhusu suala la ndoa za jinsia moja.

Kwa kauli hii Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kuunga mkono ndoa za jinsia moja, suala ambalo limeleta mgawanyiko miongoni mwa raia wa Marekani. Kumekuwa na maoni tofauti miongoni mwa Wamarekani kuhusu kuunga mkono ndoa za aina hii.

Rais Obama anasema amejadili suala hilo na familia, marafiki na majirani kwa muda mrefu na kutilia maanani wafanyakazi wenzake na askari ambao wamejikita katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.

Hatimaye amekuja na hitimisho kwamba ndoa zilizozoeleka hazikidhi matarajio ya wote.

Ni moja kati ya ndoa za mashoga iliyofungwa Jumamosi ya Oktoba 17, mwaka huu, kati ya Bw Daniel Chege Gichia (39) na Charles Ngengi (40), jijini London
Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.


Amesema wakati akiunga mkono ndoa ambazo hazijatambuliwa kisheria, kwa maoni yake, suala la ndoa za kawaida ni jambo lingine tofauti na hizo ndoa za jinsia moja.

Kauli ya Bwana Obama, imekuja siku moja baada ya jimbo la North Carolina kupitisha mabadiliko ya katiba ya jimbo hilo, yanayofafanua kuwa ndoa ni muungano tu kati ya mwanaume na mwanamke.

Saturday, May 5, 2012

MEDIA NIGHT GALA AT MWANZA HOTEL

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya baraza la habari Tanzania (MCT)Jaji Robert Mihayo akionyesha kitabu kilichozinduliwa usiku wa jana, kiitwacho State of the media report 2011, mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani huku akishuhudiwa na mgeni rasmi mh.mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo (L) na Rais wa UTPC Abubakar Karsan (R) katika hafla hiyo iliyofanyika Mwanza hotel ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya maadili ya baraza la habari Tanzania (MCT)Jaji Robert Mihayo akimkabidhi nakala ya kwanza mgeni rasmi mh.mkuu wa mkoa wa Mwanza Eng. Evarist Ndikilo. 

Kisha neno la shukurani.. 

Ndipo Burudani ikafuata... 
Wanahabari wakipata flash kwenye mtoko huo.. 

Hapa ilikuwa mwanzo kabisa kabla hazija kolea mkichwa ili watu washushe matirio.. 

Blogger maarufu wa HOSANNAINC akigonga chiaz na mgeni rasmi. 

Yakafuata mambo yetu ya mboga saba kujisevia.. 

Drafti likiendelea kuchezeka kimya kimya...

Meza yetu na mapilipili mwaaaa... 

Meza zilichafuka balaaaaa... 

Meza iliyotishaaa "Muraaa...! Reta hapa.. bhana" 

Misosiso.. 

Wadau wakiendelea kujinafasi kwa nafasi bila tafash... 

Huyu hapa mshereheshaji wa sherehe hiyo iliyofana Mc Chonya. 

Ikafika zamu ya kuonyesha vipaji on the stage akapanda braza Alan Mlawa hakika aliutendea vyema wimbo wa Rangi ya chungwa akisaidiana na wanamuziki wa Jambo Stars band. 

Mpiga gitaa la bass akifanya mikuno. 

Dance lililofana usiku huo.. 

Ni maraha mwanzo mwisho.. 

Aaaah nami si nikageuka Samba Mapangala wafanya mchezo.. 'Dunia tunapita..eEEEee'

Wadau wa ukweli wakiongozwa na Alan Kisoi pale kati wakisutumukazzZZ.. 

Aaaaah Victaaaaaaa... 

Chungulia imo-MO. 

Kutoka kushoto ni Henry Mabumo, Albert G. Sengo na Jerome 'Kamanda' 

KonazzzZZZ.. 

Mwisho wa siku bendi nzima ikashikwa na waandishi wa habari... watu wewe.

Thursday, April 12, 2012

MWANZA YATOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MAREHEMU JENERALI MSTAAFU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Ernest Ndikilo leo ameongoza Umma aliojitokeza kutoa salamu za rambirambi kwa mwili wa aliyewahi kuwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aliyefariki dunia siku ya Jumanne wiki hii akiwa na umri wa miaka 87 ambaye ameagwa rasmi leo jijini Mwanza.
Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro alizaliwa mnamo tarehe 1/01/1923 nakufariki dunia 10/04/2012.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikiro akimfariji mke mdogo wa marehemu Zainab Kiaro.
Mmoja wa wanafamilia (Kushoto) akimfariji mke wa kwanza wa marehemu Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aitwaye Penina Kiaro (Kulia).
Makamanda wakijadiliana.
Makamanda wakizidi kufurika eneo la tukio kutoa salamu zao za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Makamanda wakiwa eneo la juu katika kilima kidogo cha mawe ili kushuhudia ibada ya salamu za mwisho jijini Mwanza.
Safu ya Makamanda wengine.
Mwili huo ulitoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mchana na hatimaye majira ya saa saba ukaagwa hapa katika nyumba yake ya kikazi maeneo ya Kapripoint kabla ya kusafirishwa kuelekea wilayani Tarime mkoani Mara kwaajili ya Mazishi.
Kwa mwendo wa pole mwili ulipelekwa eneo rasmi.
Moja kati ya wanajeshi akiongoza moja ya vifungu kwenye ibada hiyo.
Mapaparazi.
Wakati wa kutoa heshima za mwisho uliwadia.
Jeshi la polisi usalama barabarani nao walikuwepo kutoa heshima zao.
Heshima...
Heshima ziliendelea kutolewa.
Makamanda wakipanga mikakati.
Mzee Gachuma katikati akifanya majadiliano na baadhi ya maafisa wa Jeshi.
Msafara.
Mwili wa marehemu aliye kuwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro umesafirishwa leo kuelekea wilayani Tarime mkoani Mara kwaajili ya Mazishi ambayo yatafanyika kesho.