Monday, July 16, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 YAMALIZIKA KWA WAWILI KUTWALIWA TOKA MWANZA


Mwanza itawakilishwa na washiriki wawili tu katika mchakato wa kitaifa kutafuta washiriki watakaoingia kwenye kambi ya EBSS jijini Dar es salaam pichani ni majaji wa EBSS mwaka 2012 Master J, na Salama Jabir wakimkumbatia Madam Ritha (katikati) mara baada ya shughuli nzito kumalizika jana katika ukumbi maalum uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Madam Ritha akishow Love na Jamaa aliyeweka rekodi.... Bubu aliyejitokeza kwenye shindano na kushindana kuimba (search BUBU AFANYA KWELI EBSS MWANZA)

Kijana mdogo kuliko wote ambaye kama vigezo vya kubanwa na shule visingekuwepo na kwasababu EBSS inathamini Elimu, basi alikuwa na ushawishi mkubwa kwa majaji. 

Akifanya mahojiano mara baada ya kutoka chumba cha usaili.

Mmechisho umo-mo.

Washiriki walipata vinywaji bure toka Coca cola.


Waliochemsha walipataje shida kuzing'oa namba zao...

Full kujiamini... mstarini kuelekea usailini..

Thats wozup...


Kutoka Mwanza hadi Dar es salaam ni umbali wa kilimeta 1200 na  ni washiriki 1200 waliojitokeza kwenye usaili wa EBSS Mwanza, kati ya hao ni 8 tu ndiyo walionekana kuwa na kipaji toka moyoni wastani wa  kilometa 150 ndipo umpate mshiriki mmoja, lakini hatimaye wawili tu kati ya hao nane wakapatikana kuwakilisha jiji la Mwanza kutokana na wengine kukosa sifa.  Jeh hii inamaanisha kuwa Mwanza haina vipaji?

Sunday, July 15, 2012

YUSUF MANJI MWENYEKITI YANGA, MAKAMU WAKE CLEMENT SANGA

Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manjikulia na Makamu mwenyekiti Clement Sanga wakiwa katika uchaguzi huo jana
Habari kwa hisani ya dinaismailblogspot.com
Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:


Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji  (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%


Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%,  Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%


Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068),  Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)


kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama

Wednesday, June 27, 2012

HAPPY BIRTHDAY CUTHBERT A. G. SENGO


Miaka minne iliyopita Siku kama ya leo my son Cuthbert anazaliwa akitofautiana wiki tu na tarehe ya kaka yake.
Happy Birthday to you my kid n' I wish all the best.
Papa & mama love's U'

WEMA SEPETU AZINDUA FILAMU YAKE 'SUPER STAR'



Wema Sepetu akipozi kwa picha mara baada ya kukaa kabla ya kuanza kuchezwa kwa Demo ya filamu hiyo usiku huu kwenye hoteli ya Hyyat Kilimanjaro.


Wageni waalikwa mbalimbali wakishuhudia uzinduzi wa filamu ya Super Star iliyochezwa na mwana dada Wema Sepetu kwenye hotli ya Hyyat Kilimanjaro


Hali ukumbini wakati wa uzinduzi wa filamu Super Star ya Wema Sepetu aliyoizindua kwenye hotel ya Hyyat Kilimanjaro jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo ikihudhuriwa na watu maarufu pamoja na wanamuziki na waigizaji.

Mtangazaji wa XXL B12 na friendz

Kutoka shoto ni Mange Kimambi, Wema Sepetu na Miriam Odemba

Omotola na makaribisho ya burudani.
Wanamzuiki, watangazaji pamoja na waigizaji mbalimbali wa filamu walihudhuria katika uzinduzi huo kutoka kulia ni Charles Baba wa Mashujaa Band, Hatman, Mtangazaji Benny Kinyaiya, Mchekeshaji Steve Nyerere, Muigizaj Ramond Kigosi, mwanamuziki Barnaba na Richie Mtambalike "Rich Rich" wakishoo Love.
Mwanamuziki Mwinyi ambaye ndiye aliyemvisha pete ya Uchumba Wema Sepetu katika filamu hiyo naye alikuwepo kwenye uzinduzi huo.

The area
Waigizaji mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo
Kundi la THT likifanya vitu vyake katika uzinduzi huo
Ankal Michuzi na maiwaifu wake kulia na rafiki yao wakipozi kwa picha

Kutoka kulia ni Asma Makau, Dina Marios, Moonshine na Janet wakiwa katika pozi kwenye uzinduzi huo.

Tuesday, June 12, 2012

MAKAMUZI YA MACHOZI BAND NA BARNABA YALIVYOFANA ROCK CITY

Video ya mduara wa Machozi Band.



Langoni ilikuwa unakutana na CD original za Lady jay Dee na Machozi Band
 

Ze dadaz wakipata flash juu ya red carpet kabla ya kuingia ukumbini, katikati ni Rhoda John, Asha Kissy na mashost zao...
 
  Kutana na Blogger Allan Kisoi pale kati akipata flash na Antonio Nuggas, Barnaba na Hellen.
  
Machozi Band katika Stage la Gold Crest Manza.

 Mc wa shughuli usiku huo Albert G. Sengo toka Clouds Fm 88.1 Mwanza

 
Dance la Machozi Band likiendelea.
Mduara na mauno yamekolea anatunukishwa mtu kitu cha msimbazi.

Mikono kwenye pembejeo na zana maho kwenye kamera na Machozi Band.

Mwimbaji mwenye umri mdogo kuliko wote hatari kwenye stage Sam Machozi.

Sutumuka ya kwaitoZZZZzzz.com

Dance la kwaito.

Barnaba alichengua vilivyo.

Hadi ladiZ wanakiri kuwa Barnaba ni 'moTTo'

Nishakwambia kuwa Barnaba ni 'Motto' 

Mwanamuziki haitwi 'Mwanamuziki' bila kujua kutumia japo chombo kimoja wapo cha muziki.


Wageni toka mbali hawakukosa.

Kutoka kulia Anthonio Nuggaz wa Kambi popote, Captein Gadna G. Habbash, Ramma wa Villa Park na Albert G. Sengo

Zungusha zungusha....

PICHA LINAENDELEA...

Monday, June 11, 2012

MPAMBANO KATI YA MSONDO NA SIKINDE KUSINDIKIZA SHEREHE ZA VILLA PARK KUTIMIZA MIAKA MITANO

Villa Park Resort Mwanza inaadhimisha miaka mitani tangu kuanzishwa kwake, shamrashamra zitaanza wiki hii siku ya alhamisi katika usiku wa Mwambao ambapo mwanamama Jokha Kassimu atatoa burudani akichagizwa na Kanga Moko Ndembendembe kwa kiingilio cha sh 3000/=


Vilevile kwa mujibu wa mratibu mkuu wa soka Mzee Halphan Ngasa amesema kuwa kutakuwa na ligi ya mtoano (Villa Soccer Bonanza) ambapo timu za Mashabiki na wafanyakazi za Villa Sports Club, Lakairo Sports Club, Victoria Sports Club na Shooters Sports Club zitachuana.


Mshindi wa kwanza kwenye ligi hiyo ya mtoano kupata kombe kubwa, mbuzi na kreti ya kinywaji kutoka wadahamini TBL, mshindi wa pili kunyakuwa kombe na kreti mbili za kinywaji toka TBL, mshindi wa tatu ataondoka na kombe na kreti moja ya kinywa cha TBL


Lengo la mashindano hayo ni kuboresha afya na kusisitiza umuhimu wa mazoezi kwa jamii hususani watu wazima.

Burudani nyingine siku ya Ijumaa katika Compass Night na Miaka mitano ya Villa Park Dj PQ (Clouds fm) na Dj Mafuvu (East Africa Radio) na maDj wote wa Villa Park (Dj John Lyatow, Dj Samm, Dj Chriss) kumwaga burudani usiku huo kiushindani zaidi.

Katika usiku  wa Jumamosi Sambamba na disco kali ndani ya Villa Disco Teque vilevile uwanja wa nje kutakuwa na mpambano awamu ya kwanza wa Bendi za Msondo, Sikinde na bendi ya jijini Mwanza Super Kamanyola kiingilio usiku huo shilingi 5,000/= na shilingi 7,000/= kuzama hadi ndani.


Jumapili kuanzia saa 12 jioni ni Mpambano wa kukata na Shoka kati ya Bendi tatu kongwe hapa nchini zenye mashabiki wengi kama Simba na Yanga nazungumzia Msondo, Sikinde na Super Kamanyola nani zaidi?

Thursday, May 31, 2012

UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA

Kuanzia Alhamisi hii, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake. Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Masimba.

The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi, Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).

Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu; BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?

MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?

BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?

MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa

BC: Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka utotoni au la?

MM: Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk Show haikuwa ndoto yangu hapo awali. Lakini kama unavyojua,maisha huenda yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu. Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.

BC: Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania. Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini chanzo?

MM: Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha ha haaaa

BC: Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?

MM: Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio hapa tulipo hivi sasa.



BC: Katika pitapita yangu ya mitandaoni nimesoma mahali kwamba Oprah ni miongoni mwa wanawake wanaokuvutia sana na yeye ni sababu mojawapo ya w ewe kuanzisha The Mboni Show ikiwa kama hatua mojawapo ya kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya. Kuna ukweli wowote katika hilo?

MM: Ni ukweli kabisa kwamba Oprah Winfrey ananivutia kupita kiasi. Pamoja na hayo show yangu haitokuwa ki-Oprah moja kwa moja. Sitaki na wala siwezi kumuiga kwa kila kitu. Ntakachofanya mimi ni kuchukua yale ambayo naweza kuyachukua na hususani kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania zaidi. The Mboni Show ni show ya kitanzania kwa ajili ya watanzania.

BC: Katika maelezo ya awali ya The Mboni Show umeeleza kwamba malengo ya show yako ni kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya watanzania. Mmejipanga vipi kufikia malengo hayo?

MM: Yaani Jeff you will be Suprised .Wewe subiri tu utajionea.Lakini ki-ukweli The Mboni Show imejipanga vilivyo. Nawaambia The Mboni Show ndio kimbilio la Watanzania na mwokozi wao ha ha ha ha

BC: Mlolongo wa kuanzisha TV show ni mrefu na bila shaka umepambana na vikwazo kadhaa mpaka kufikia hatua hii. Unaweza kunieleza kidogo kuhusu vikwazo ulivyopitia na kitu gani kilikuwa kinakupa msukumo kwamba endelea tu usikate tamaa?

MM: Jeff sio kitu rahisi kama watu wanavyofikiria. Mimi na timu yangu tumeanza production since April last year na imagine ndio kwanza tumemaliza juzi juzi.Ni wazi kwamba katika kutimiza lengo au azma hii nimepitia vikwazo vingi ambavyo kwa kweli nisingesimama imara ningeweza kabisa kukata tamaa. Lakini mwisho ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia mpaka kufika hapa. Kwa upande wa kitu ambacho kilikuwa kinanipa msukumo naweza kusema ni asili yangu ya kuwa mvumilivu na mbishi sana ninapotaka la kwangu. Hizo ndizo silaha zangu; uvumilivu na ubishi wenye manufaa. Vikwazo vilikuwa vingi sana ingawa sitopenda kuvitaja.Kwa ufupi nawaambia sio kitu kirahisi hata kidogo, ni kukomaaa tu mpaka kieleweke.

BC: Tunaposikia mtu anaanzisha kipindi cha televisheni kuna maswali kadhaa yanakuja. Je kitakuwa ni kipindi cha kurekodiwa ndani ya studio maalumu au kitakuwa kipindi cha kurekodiwa nje ya studio kwa maana ya mtaani nk. Kwa upande wenu format ya production ya The Mboni Show imekaaje?

MM: Kwa upande wetu tuna sehemu maalum ya kurekodia kama hii session ya kwanza vipindi vyote tulirekodia pale Serena( zamani ilikuwa ikiitwa Movenpick). Nawashukuru sana Serena kwa mchango wao katika kufanikisha hili. Next session itakuwa the same japo huwa tunatoka kidogo na kurekodi nje. Kuna mtu ambaye tumerekodi naye nje na hivi karibuni tunapanga kuingia mtaani. The Mboni Show ni kwa ajili yenu watanzania. Popote tutawafuata.

BC: Upo ukweli kwamba Hosts wengi wa TV show huwa yawabidi wawe na tabia ya kujisomea sana ili kupata mawazo na mitazamo mipya kila mara na kwenda na wakati. Je, na wewe pia una hulka hiyo au umejipanga namna gani katika kuhakikisha kwamba sio tu unakwenda na wakati bali unapata ideas mpya mpya za show nk?

MM: Kama nilivyogusia hapo mwanzo, siri yangu kubwa ni kuangalia kwa makini show za wengine zinafanywaje. Namuangalia mtu kama Oprah,Tyra, Monique, Hellen etc ili kupata mtazamo tofauti na ili niweze kuboresha show yangu kila mara. Sidhani kama ni lazima sana kusoma sana vitabu kwa sababu inategemea na aina ya show uliyonayo au unayoifanya.

BC: Mbali na hii venture mpya ya kuwa Host wa TV show, wewe ni mjasiriamali. Siku hizi, kama tunavyoona, wanawake wengi zaidi nao wanaingia kwenye ujasiriamali. Una ushauri gani kwa wanawake wenzio kuhusiana na ujasiriamali?

MM: Kwanza lazima ujue hiki kitu ” Fanya kitu ambacho unakipenda na unakiweza. Wanawake wengi tunakurupuka kwenye ujasiriamali na wakati hatuuwezi. Watu wanafanya kama fashion. Let’s say mimi napenda kuwa na Boutique kwa sababu napenda fashion na ninaimudu.Haya sasa nina talk show kwa sababu naipenda na ninaimudu. Kwa hiyo wanawake wenzangu, tujaribu kufanya kitu ambacho tunakipenda na kukimudu. Ni rahisi zaidi kufanikiwa ukiwa na hayo mambo mawili. Mapenzi kwa kitu unachokifanya au kutaka kukifanya na uwezo wa kukifanya.

BC: Mwisho una ujumbe gani mahususi kwa watanzania? Na pia kwanini mtu achague kuangalia The Mboni Show badala ya show zingine lukuki kwenye luninga?

MM: Ujumbe kwa watanzania wenzangu “Tupende vya kwetu, tuthamini vya kwetu, Tupendane na tushirikane. Kama unaona una connection na wewe huna uwezo nao ila kuna mwingine anaweza basi msaidie na sio kubaniana na kuoneana vijiba vya roho bila sababu za msingi.. Na pia tupende kusifiana. Mwenzako kafanya kizuri basi mpe hongera zake na kama kakosea basi muelekeze( muongoze). Ha ha ha ha Trust me The Mboni show iko kitofaut kabisa na zile tulizozizoea.  Kwenye The Mboni show unapata kila kitu. Full package ha ha ha ha.

Kwa mengi zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya The Mboni Show katika www.thembonishow.com.