Monday, December 17, 2012

EDGAR MAPANDE ALA NONDO

Edgar Mapande mara baada ya kutunukiwa pichani akiwa na Naibu Waziri wa Nishati na madini, mbunge wa Shinyanga mjini Mh. Steven Masele ambaye alikuwepo kuweka hamasa ya vijana kuthamini elimu, wengine kulia ni mwenyekiti wa serikali za mitaa eneo la Kunduchi Benedict Tibehenderwa, na kushoto ni bw. John Mbaga ambaye ni CEO wa Bayport Financial Service Ltd ambao nao walihudhulia maafali hayo.  



AEdgar Mapande mara baada ya kutunukiwa katika picha ya furaha mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Master Of Science in Marketing kwenye maafali ya 11 ya Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam yaliyofanyika ijumaa ya tarehe 14 Disemba 2012.






Edgar Mapande akiwa na dada yake Oliver J. Ryanna (Mrs Albert Sengo), katika picha ya furaha mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Master Of Science in Marketing kwenye maafali ya 11 ya Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam yaliyofanyika ijumaa ya tarehe 14 Disemba 2012.


Picha ya furaha na smile za wadau kwenye maafali ya 11 ya Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam yaliyofanyika ijumaa ya tarehe 14 Disemba 2012.


Picha part TWO ya furaha na smile za wadau kwenye maafali ya 11 ya Chuo Kikuu Cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam yaliyofanyika ijumaa ya tarehe 14 Disemba 2012.









Mtunukiwa Edgar Jonas Mapande akimlisha keki  Eva Mbaga huku mama wa mtoto huyo Gisele Mbaga akishuhudia tukio hilo muhimu la kumbukumbu.










Picha ya familia.


Mtunukiwa Edgar Jonas Mapande akipata picha ya pamoja na familia ya Bw. John Mbaga (R) ambaye ni CEO wa Bayport Financial Service Ltd, kulia ni mkewe  Gisele Mbaga na mtoto  Eva Mbaga.



Sunday, December 16, 2012

Mh. LOWASSA ASHIRIKI HARAMBEE YA KANISA AKYERI MERU

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokelewa na viongozi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha kwa ajili ya kuongoza harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya ukarabati wa kanisa hilo,iliyofanyika leo Mkoani humo.

===========     =========   =========
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa amesisitizia tena kuwa tatizo la ajira kwa vijana ni jambo la hatari kwa usalama wa nchi,wakati alipokuwa katika harambee ya kuchangia ukarabati wa kanisa la kilutheri usharika wa Akyeri Meru mkoani Arusha, Mh lowassa ameonya kuwa suala hilo lisiposhughulikiwa haraka litasababisha hali ya hatari.

''tunashuhudia maandamano katika mataifa ya ulaya vijana wakidai hali bora ya maisha pamoja na ajira.hali hiyo tusipoangalia inaweza kutokea hapa nchini kwetu.

huko nyuma niliwahi kusema kuwa makanisa, mashirika na watu binafsi wasaidie juhudi za serikali kutatua suala hilo''alisema Lowassa.

Lowassa ambaye katika harambee hiyo aliongozana na marafiki zake, ambapo yeye na familia yake pamoja na marafiki zake wamechangia kiasi cha shilingi millioni 33.2.

Zaidi ya shilingi millioni 160 zikiwa ni fedha tasilimu pamoja na ahadi zilipatikana katika harambee hiyo.

Kwa upande wake askofu Akyoo wa jimbo la Meru alimsifu Lowassa kwa uchapakazi wake popote alipokuwa.''Wakati ulipokuwa Waziri Mkuu ukimsaidia rais tulishuhudia uwezo wako mkubwa katika kufuatilia majukumu yako''alisema na kuongeza kuwa Lowassa ni mtu wa ibada

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa tatu kushoto) akiongozana na Askofu wa Kanisha hilo la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha,Askofu Akyoo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia muda mfupi kabla ya kuanza kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea ahadi ya mchango kutoka kwa mmoja wa wamini wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka kanisani hapo baada ya kumalizika kwa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Lutherani usharika wa Akyeri,Dayosisi ya Meru Mkoani Arusha.

SHOW YA KOFFI JIJINI MWANZA


Koffi olomide akitambuklisha kwa mashabiki wake mmoja kati ya wasanii wa nyumbani aliyemvutia Mwanadada Recho toka THT.
Koffi Olomide akiliongoza skwadi lake la madensa jukwaani,full kujiachia.

Pichani shoto ni msanii kutoka THT,Rachel akionesha umahiri wake wa kucheza lingala huku Koffi Olomide akidekshia kwa mbaali hivi,palikuwa hapatoshi watu wangu.

Mwimbaji nyota wa Koffi Olomide,Cindy nae akionesha umahiri wake wa kujimwaya mwaya jukwaa,huku mashabiki (hawapo pichani) wakipiga miluzi na mayowe.

Wadau nao wakijichukulia taswira zao kwa ajili ya kumbukumbu.






Wakazi wa Mwanza walipfika kwenye uwanja wa ccm-kirumba walijionea vilivyo kwamba Koffi Olomide na kundi lake zima la Quartie Latin bado ni moto wa kuotea mbali.

Burudani ikiendelea jukwaani.

Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya SBL,Ephraim Mafuru, Anitha Msangi Maurice Njowoka na Patrick Kisaka kutoka kampuni ya bia ya Serengeti wakiwa katika picha ya pamoa usiku huu ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba.

Sehemu ya wakazi wa Mwanza wakifuatilia kwa makini burudani.

Lwaaaaa....!! 

Msanii mahiri kutoka THT,Rachael kama kawaida nyonga yake laiiini inayosisimua mashabiki wake kila awapo jukwaani,na ndivyo kwa wakazi wa Mwanza walivyobaki kupiga mayowe ya shangwe usiku huu ndani ya CCM-Kirumba.

Ilikuwa ni burudani mwanzo mwisho.

Madansa wa Koffi Olomide wakipanda jukwaani kwa staili ya kipekee kabisa tayari kuangusha bonge la burudani kwa washabiki na wapenzi wa kundi la Quartie Latin.

Cindu mwanamuziki mwenye sauti nyororo.laini na safi kabisa akiimba jukwaani kwa umahiri mkubwa huku akipambwa na madensa wa bendi hiyo ya Quartie Latin.

Cindy akiimba kwa hisia jukwaani.

Back up ya ukweli ya Koffi Olomide akiimba kwa pamoja jukwaani.

Mwanamuziki mahiri wa Koffi Olomide,Cindy akipewa maiki mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa CCM-Kirumba usiku huu tayari kwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wa kundi lao.Onesho la Tusker Carnival limeandaliwa na kampuni ya Prime Time Promotioni ikishirikiana kampuni dada ya Clouds Media Group,likidhamiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager "bia bora,marafiki wa kweli".


Mwanamuziki Koffi Olomide sambamba na mwimbaji wake nyota Cindy wakiwasili usiku huu kwenye uwanja wa CCM-Kirumba tayari kwa kuwatumbuiza wakazi wa jiji la Mwanza.

Cindy akiwaza jambo jukwaani kwa utulivu mkubwa.


H baba kama kawaida yake..







Ben, Mussa, Suzy na Crew.
Mwanamuziki Nyota wa kimataifa katika anga ya muziki wa dansi  kutoka  nchini DR-.Kongo Koffi Olomide akiwa ameambatana na mwanamuziki wake mahiri katika uimbaji aitwaye Cindy wakishukua jukwaani mara baada ya kumaliza kutumbuiza usiku huu ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza,Onesho liitwalo Tusker Carniva lilikuwa limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Tusker Lager


Koffi Olomide akiingia kwenye mchuma wake mara baada ya kumaliza onesho lake usiku huu na kufanikiwa kuzikonga nyoyo za mashabiki wake kwa kiasi kikubwa.