Friday, September 3, 2010

MAJIBU YA KIKAO CHA SIMBA KILICHOFANYIKA MWANZA JUMATANO WIKI HII

WANACHAMA WA SIMBA SPORT CLUB TAWI LA MWANZA WAMEJIPANGA KIKAMILIFU KATIKA KUIPOKEA TIMU YAO, KUIPA HIFADHI YENYE HADHI CLUB HIYO YA SOKA INAYOSHIRIKI LIGI KUU ILI IPATE USHINDI WA KISHINDO KWA MECHI ZAKE NNE ITAKAYOCHEZA WAKATI IKITUMIA UWANJA WA CCM KIRUMBA MWANZA KAMA UWANJA WA NYUMBANI.

AKIZUNGUMZA NA CLOUDS FM MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA TAWI LA MWANZA AMBAYE ANATOKA KATIKA KUNDI LA FRIENDS OF SIMBA AMESEMA KUWA UONGOZI WAKE PAMOJA NA WANACHAMA WA MWANZA NA UKEREWE WAMEJIPANGA KIKAMILIFU KUHAKIKISHA KUWA TIMU YAO INASHINDA NA KUCHUKUWA POINTI ZOTE PINDI ITAKAPO TIA TIMU JIJINI MWANZA.

ISHU ALIONGEZA KWA KUSEMA KUWA MWAKA JANA WANACHAMA WA SIMBA TAWI LA MWANZA WALIHAKIKISHA KUWA SIMBA INAENDELEZA WIMBI LAKE LA USHINDI NA KUTOFUNGWA MECHI HATA MOJA KWA KUHAKIKISHA WANAJIPANGA VYEMA NA KUKAMILIKA KILA IDARA, BASI VILE VILE MWAKA HUU NDIVYO ITAKAVYO KUWA.

KUHUSU USHINDANI WA JADI ULIOPO WA TIMU YAKE NA WANA KISHAMAPANDA (TOTO AFRIKA), ISHU ASHRAF AMEIPONDA TIMU YA TOTO KWA KUSEMA KUWA LICHA YA MABADILIKO YA USAJIRI KWA TIMU HIYO KUCHUKUWA WACHEZAJI WENYE VIPAJI, TIMU HIYO SI CHOCHOTE, SI LOLOTE KWA MNYAMA NAKUAHIDI KUWAFUNDISHA SOKA TOTO PINDI WATAKAPO KUTANA ANA KWA ANA DIMBANI.

TIMU YA SIMBA INAYOTEGEMEA KUWASILI MWANZA ASUBUHI YA TAREHE 12 SEPT 2010 KWA USAFIRI WA ANGA, IMEUTEUWA UWANJA WA CCM KIRUMBA WA JIJINI MWANZA KUWA UWANJA WAKE WA NYUMBANI KUPISHA UKARABATI KATIKA UWANJA WA BIBI DAR ES SALAAM.

No comments:

Post a Comment