Sunday, July 14, 2013

MBUNGE WA MUSOMA MJINI PAMOJA NA MEYA WASHIRIKI MAZISHI YA HUPHREY SIMON MKOANI MARA

Padre akiongoza ibada kumuombea marehemu Humphrey Simon iliyofanyika jana nyumbani kwao Makoko Musoma mjini. 

Mbunge wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere (katikati mwenye suti nyeusi) alihudhuria ibada hiyo sambamba na mazishi.

Waumini walishiriki meza ya bwana katika ibada hiyo ya kumuombea marehemu.

Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisusura akishiriki meza ya bwana.

Mmoja ya viongozi wa kampuni ya mawasiliano ya tigo akishiriki meza ya bwana.

Kusanyiko kwenye ibada nyumbani.

Mama Nyimbo akiongoza safu ya akinamama wenzake katika utoaji heshima za mwisho kwa mwili wamarehemu.

Sambamba wananchi wengine Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Mashangazi na ndugu wa karibu wa marehemu wakitoa heshima za mwisho 

Heshima za mwisho zilikoma kwa safu ya wanaume kufunga zoezi hilo.

Kisha safari ya kuelekea makaburini eneo la Makoko Musoma mkoani Mara ikafanyika.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo ambao wanafanya kazi na mke wa marehemu walitoa sapoti ya kutosha katika shughuli nzima za mazishi, hata wengine walidiriki kusafiri toka mikoa mbalimbali ili kuwakilisha.

Mwili wa marehemu Huphrey Simon ukiwa kwenye nyumba yake ya milele.

"Uliumbwa kwa udongo na mavumbini utarudi"

Mke wa marehemu Bi. Neema akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe.

Mke wamarehemu akiweka shada la maua.

Mjomba wa marehemu Mr. Tega akiwa na shangazi wakiweka shada la maua.

Shangazi wa marehemu.

Mbunge wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Humphrey.

Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisusura akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Humphrey.


Mtoto wa marehemu akiweka shada la maua. 
Picha ya pamoja ya wanandugu akiwepo mke wa marehemu (wa 3 kutoka kushoto) mbele ya kaburi .

Mtoto wa marehemu Huphrey Simon akiweka shada la maua juu ya kaburi la baba yake.

Marafiki wa marehemu.

Jina la bwana lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment