Showing posts with label UCHAGUZI. Show all posts
Showing posts with label UCHAGUZI. Show all posts

Thursday, July 9, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AZINDUA UKUMBI MPYA WAMIKUTANO WA CCM, MJINI DODOMA LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo mjini Dodoma, leo Julai 9, 2015. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, akibonyeza kitufye cha kengere kuashiria uzinduzi rasmi wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo maeneo ya ..... mjini Dodoma, leo Julai 9, 2015. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, na Balozi wa China nchini Tanzania, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, uliopo mjini Dodoma, wakati wa hafla ya uzinduzi iliyofanyika leo Julai 9, 2015. Picha na OMR
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.  Jakaya Kikwete, akimkabidhi mfano wa ufunguo wa Ukumbi mpya wa mikutano wa CCM wa Dodoma Convention Centre, Katibu Mkuu wa CCM Bara, Abrahman Kinana, baada ya kuzindua rasmi ukumbi huo leo, mjini Dodoma. Picha na OMR
Rais jakaya Kikwete, akionyesha mfano wa ufunguo wa Ukumbi huo baada ya kukabidhiwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa ukumbi huo leo, mjini Dodoma. Picha na OMR
Picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali baada ya uzinduzi huo. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwetena baadhi ya Viongozi, wakitembelea kukagua ukubi huo baada ya uzinduzi. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwetena baadhi ya Viongozi, wakitembelea kukagua ukubi huo baada ya uzinduzi. Picha na OMR
Rais Jakaya Kikwetena baadhi ya Viongozi, wakitembelea kukagua ukubi huo baada ya uzinduzi. Picha na OMR
Mwonekano wa meza kuu ya ukumbi huo. Picha na OMR
Picha ya pamoja baada ya kutembelea kukagua ukumbi huo. Picha na OMR 

Tuesday, July 7, 2015

ZOEZI LA UBORESHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA LAENDELEA MKOANI PWANI, RAIS JAKAYA KIKWETE AJIANDIKISHA KUPITIA BVR KIJIJINI MSOGA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
 Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
 Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.
Rais akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha katika daftari daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
---
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.

“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.

Sunday, July 5, 2015

KAMATI MAALUM YA CCM ZANZIBAR YAPITISHA JINA LA DKT. SHEIN KUGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye pia ni  Mjumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Makamu  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, wakati walipowasili kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria katika kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, ambacho leo kilipitisha jina la Dkt. Shein kuwania nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM. Picha na OMR
Makamu  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati Maalum ya CCM kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kupitisha jina la Mgombea Urais wa Zanziba kwa Tiketi ya CCM. (katikati) ni Mjumbe wa Kamati hiyo, ambaye aliongoza kikao baada ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti, Dkt.Mohammed Gharib Bilal na Mjumbe, Balozi Iddi. Picha na OMR
Kiti cha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Shein, kikiwa wazi baada ya kukabidhi madaraka kwa wajumbe ili kujadili na kuteua jina la mgombea Urais wakati wa Kikao Maalum cha CCM, leo. Picha na OMR
Kaimu Mwenyekiti wa CCM, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao hicho maalum cha Kamati Maalum, baada ya kuteuliwa na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kushoto) ni Balozi Seif Iddi. Picha na OMR
 Dkt.Bilal na Balozi Iddi,wakifurahia baada ya Wajumbe kupitisha Jina la mgombea.

Mjumbe, Dkt.Bilal, akimpongeza Dkt. Shein baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe katika Kikao cha Kamati Maalum ili kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali. Picha na OMR
Mjumbe, Dkt.Bilal, akimpongeza Dkt. Shein baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe katika Kikao cha Kamati Maalum ili kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali. Picha na OMR
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.  Ali Mohammed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Malum, akiwashukuru baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar, katika Kikao kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Picha na OMR
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.  Ali Mohammed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Malum, akiwashukuru baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar, katika Kikao kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Picha na OMR
Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.
Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.
Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.