Tuesday, July 7, 2015

ZOEZI LA UBORESHWAJI DAFTARI LA WAPIGAKURA LAENDELEA MKOANI PWANI, RAIS JAKAYA KIKWETE AJIANDIKISHA KUPITIA BVR KIJIJINI MSOGA

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo mpya wa kielektoniki(Biometric Voters Register( BVR) katika kijiji cha Msoga,kata ya Msoga wilayani Bagamoyo leo.Kulia akiangalia kwa makini ni mwandikishaji msaidizi Bi.Happyness Thomas Misana na katikati ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi Tume ya Taifa Uchaguzi Bi.Mariam Rajabu.Kushoto aliyesimama akishuhudia ni Mbunge wa Chalinze Ridhwani Kikwete.
 Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Uchaguzi Taifa ya Uchaguzi Bwana Sanif Khalfan akichukua lama za vidole vya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kijijini kwake Msoga wilaya ya Bagamoyo leo .
 Bwana SANIF Khalfan ambaye ni Afisa TEHAMA kutoka ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi akimpiga picha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipokwenda kujiandikisha kupiga kura kwa kutkumia teknolojia mpya ya BVR kijijini Kwake Msoga leo.
 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitambulisho chake wakati wa zoezi la kujiandikisha kijijni kwake Msoga leo.
 Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya Rais Kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
Rais Kikwete akimshukuru Mwenyekiti wa tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva baada ya kukabidhiwa kitambulisho chake cha kupiga kura baada ya kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo. Picha na Freddy Maro.
Rais akuonyesha kitambulisho chake alichopewa mara baada ya kujiandikisha katika daftari daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia teknolojia ya BVR huko kijijini Msoga wilayani Bagamoyo leo.
---
JUMLA ya watu milioni 11,248,194 wameandikishwa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura zoezi ambalo linaendelea kwa sasa hapa nchini likiwa limeingia mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa leo kwenye Kijiji cha Msoga kata ya Msoga wilayani Bagamoyo na mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Taifa Damian Lubuva alipokuwa anampa taarifa Rais Dk Jakaya Kikwete mara baada ya kujiandikisha.

Bw. Lubuva alisema kuwa malengo ni kuandikisha watu milioni 21 hadi 23 kote nchini mara zoezi hilo litakapokamilika kati ya Julai mwishoni au Agosti mwanzoni kama hakutatokea matatizo.

“Hadi sasa ni mikoa 11 inaendelea na zoezi ambayo ni Mwanza Shinyanga, Geita, Simiyu, Mara, Manyara, Arusha, Kilimanjaro Morogoro na jana ulianza mkoa wa Pwani,” alisema Lubuva.

Aidha alisema kuwa changamoto zilizojitokeza ni za kawaida hasa kutokana na mfumo huu kuwa ni mpya kwani kila jambo jipya lina changamoto zake.

“Mfumo huu ni mpya hivyo lazima kuwe na changamoto za hapa na pale lakini zoezi linakwenda vizuri na tunaamini kuwa tutafanikiwa kama tulivyopanga,” alisema Lubuva.

Mkoa wa Pwani una jumla ya vituo 1,752 na mashine za BVR 932 ambapo kata ya Msoga kuna jumla ya vituo 17 zoezi hilo kwa mkoa wa Pwani lilianza jana na litamalizika Julai 20.

TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR YATANGAZA MAJIMBO YA UCHAGUZI ZANZIBAR


Monday, July 6, 2015

CHANGAMOTO ZA WALEMAVU NDIYO SABABU KUBWA YA WASTARA KUINGIA KWENYE SIASA

Changamoto za Walemavu Ndiyo Sababu Kubwa ya Wastara Kuingia Kwenye Siasa Naitwa Wastara Juma kama watanzania wenzengu mnavyonifahamu mimi ni muigizaji wa filamu na kazi nyingine zinazohusiana na kiwanda cha filamu. 

Leo niongee kitu ili watanzania wenzangu muelewe kwanini nimeamua kujiingiza kwenye siasa, kikubwa kilichonisukuma kuingia kwenye siasa ni jambo moja kubwa sana kwangu ambalo ni (WALEMAVU) .

 Huwezi kusimulia uchungu wa mwana wakati haujawahi kuzaa huwezi kumzunguzia au kumtetea mlemavu hali ya kuwa hujui uchungu, matatizo na maumivu yake,, Mpaka sasa nimeishi katika hali ya ulemavu kwa zaidi ya miaka 6 japo kuna wengine wamezaliwa wakiwa walemavu lakini kwa mda mchache tu miaka 6 nimepata mateso makubwa sana kuanzia kimaisha, kisaikolojia na hata kimiundombinu ya nchi yetu. 

Pamoja na umaarufu wangu wote lakini hakuna shirika wala taasisi yoyote iliyowahi kunishika mkono japo jambo hili halikuwa muhimu sana kwangu kwani naweza kujihudumia mimi na familia yangu. 

Jambo la muhimu kwa sasa na linaloniumiza sana ni kuona ndani ya nchi yetu walemavu hawana thamani wala haki yoyote si Mahosptalini, Maofisi ya Kiserikali, ndani ya vyombo vya Usafiri, makazini na hata majumbani. Labda moja tu ndio nimeona walemavu wamepewa nafasi angalau ya kupita kuelekea sehemu au kuingia na kukaa ni ndani ya jengo la Bunge tu hapo Dodoma. 

Ndani ya nchi yangu walemavu wote tunachukuliwa kama ombaomba na hali hii imewakatisha tamaa walio wengi mpaka kuamua kuingia mitaani na kuzunguka wakiomba shilingi mia mia za kujikimu kimaisha. Naumia sana napojitizama mimi na kufikiria je leo hii nisingekuwa maarufu ningeishi maisha gani? Napata jibu kuwa huenda na mimi ningetafuta kijana akanikokota na baiskeli na kuanza kuzunguka mitaani kuomba omba.

 Siamini kabisa kama kweli ukiwa mlemavu na akili yako pia inalemaa la hasha bali naamini kuwa serikali yetu haitutazami walemavu kama na sisi tuna haki sawa na wengine na tunastahili kujumulishwa na kila kitu wanachipata wasio na ulemavu. Kuanzia kielimu, kiafya, miundombinu na sehemu nyinginezo. 

Leo hii ni aibu kubwa kuwa hata television ya taifa inayotoa taarifa ya habari kwa nchi haina mtangazaji anae wahabarisha walemavu viziwi ambao nao wanahaki ya kujua nchi yetu na yaliyojiri.

 Leo hii ni aibu zinajengwa barabara lakini hazima sehemu ya kupita walemavu  Leo hii ni aibu kuona shule nyingi za ulemavu kwanza ni za zamani halafu hakuna hata vifaa vinavyoendana na dunia ya kisasa ya sayansi na teknolojia Ni aibu kuona hatuna viwanja vya michezo kwa walemavu wakati na sisi tunahaki ya kushiriki hata mashindano ya Paralimpic.

 Nimejaribu kuonyesha na kuwapigania walemavu wenzangu kupitia sanaa lakini nimeona sauti yangu ni ndogo na haisikiki kokote sasa nimeamua kuingia kwenye siasa ili nisamame na kuwapigania Walemavu wenzangu wasio na sauti nao sawa na kuona machozi, maumivu na mateso yao nayafuta vipi.

Pia ili niweze kufuta kiapo nilichoweka kwenye nafsi yangu baada ya kuona tunapokelewa vibaya ndani ya nchi yetu wenyewe kwamba lazima siku moja nitawapa furaha walemavu wenzangu kabla sijafa nitapigania haki zao za msingi ili nao au tujione tuna haki sawa na wengine nimekaa na dukuduku hili ndani ya miaka 5 sasa huu ni wakati wa kulitoa na kujitoa kwa nguvu zangu zote kuhakikisha walemavu wanawekwa katika mazingira mazuri kama nchi za wenzetu waishi vizuri na kufikia hata nusu yake tu basi nitakuwa nimefikia lengo la kutetea haki za msingi kwa walemavu wenzangu sababu hata mim ni muhanga nimetumia lugha nyepesi ili nieleweke sina tamaa ya chchote ila sitakuwa sawa kufa bila kuwaweka wenzangu kwenye maisha ya haki na sehemu sahihi kwa sasa kuonyesha nilichohahidi moyo wangu ni bungeni najua kma si wewe uliyelamaa basi ndugu rafiki jirani yako lazima atakuwa kwenye hali hii hivyo watanzania kutumia nguvu zetu kunisuport amtapoteza kitu bali mtaongeza msaada kwa wale wasijioweza asante kwa kusoma ujumbe huu Wastara Juma on Instagram 

MTIA NIA WA NAFASI YA UBUNGE MOSHI VIJIJINI ,EVARIST KIWIA AJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUPIGIA KURA.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi vijini Evarsit Kiwia akitoa maelezo binafsi mbele ya afisa wa tume alipofika kujiandikisha kupitia mfumo mpya wa BVR katika kata ya Old Moshi Magharibi.
Kiwia akijaza moja ya fomu zinazotakiwa kujazwa wakati wa zoezi a uandikishwaji.
Mtia nia wa nafasi ya Ubunge jimbo la Moshi Vijijini ,Evarist Kiwia akichukuliwa Taswira kwa ajili ya kupatiwa kitambulisho maalumu kwa ajili ya kupigia kura.
Kiwia akizungumza na wanahabari mara baada ya kumaliza zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kupitia mfumo mpya wa BVR.
Na Dixon Busagaga WA globu ya jamii Kanda ya Kaskazini,Moshi.

CHAMA cha Demkrasia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo la Moshi vijini kimeonesha kuwa na hofu kwa baadhi ya wananchi kushindwa kuandikishwa katika zoezi la uandikishaji kwa kutumia mfumo mpya wa BVR huku kikiiomba tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji kwa wakazi wa maeneo hayo.

Ombi hilo limekuja kutoka na kuwepo kwa madai ya kuwa baadhi yam ashine hazikuweza kufanya kazi vizuri hali iliyolazimu baadhi ya wananchi kushindwa kujiandikisha.

Sababu nyingine iliyopelekea ombi hilo ni kuhusu jiografia ya jimbo hilo pamoja na shughuli ambazo zimekuwa zikifanywa na wakazi wa maeno hayo ambao wengi wao wamekuwa wakitumia muda mwingi kufanya kazi ya kilimo na ufugaji hali inayochangia kukosa muda wa kutoka kwenda kupanga foleni kwa ajili ya uandikishwaji.

Akizungumza mara baada ya kujiandikisha Menyekiti wa Chadema jimbo la Moshi vijijini ,Ekarist Kiwia alisema kutokana na usumbufu unaotokana na mashine za BVR ni vyema tume ikatizama namna ya kuongeza muda wa zoezi la uandikishaji.

“Mimi mwenyewe nimeshindwa kujiandikisha  katika kituo cha Mande Kanisani ambapo ndiko eneo la langu ….nimeenda kitongoji kingine nikapewa ridhaa ya kujiandikisha lakini wako watu wanakosa fursa ya kujiandikisha kutokana na mashine kutofanya kazi vizuri”alisema Kiwia.

Kiwia ambaye pia ni miongoni mwa watia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo kupitia Chadema ,alisema licha ya uwepo wa changamoto hizo wananchi hawana budi kujitokeza kwa wingi ili kupata kitamburisho cha kupigia kura kitakachosaidia kumpata kiongozi bora wa jimbo hilo.


Kwa upande wao wananchi wa  kata ya old Moshi Magharibi walisema wamehamosika kujitokeza katika zoezi la uandikishaji,isipikuwa changamoto za mashine za BVR ndio zimekuwa zikiwakatisha tamaa kuendelea kungojea katika foleni.


Elizabeth  Massawe na Alex Kiwia walisema  kuwa walitakiwa kufanya kijiandikisha katika kituo cha Mande kanisani lakini  kwa siku tatu maofisa katika kituo hicho wanadaiwa kuwajibu wananchi kuwa  mashine ni chafu za kusafisha na kwamba hawana uhakika wa kujiandikisha.

“Mimi hata nikienda kituo cha jirani hawakubali   kuniandikisha  wanasema nijiandikishie sehmu ninayoishii sehemu ninayokaa ndio hizo mashine hazifanyi kazi mara utaambiwa ni zakusafisha huku muda wameweka kidogo ni wiki moja tuu”alisema Massawe.

Kiwia alisema utaratibu uliowekwa na tume kuwa watu wajiandikishie shemu ambayo wanatoka  ni mbaya kutokanana kwamba mashine za BVR zinasumbua na hazitabiriki.

Alisema wananchi wengi watakosa haki yao ya msingi ya kupiga kura kutokana na kushindwa kujiandikisha na kwamba muda uliopangwa ukiisha wanondoka bila kuandikisha wananchi wote.



MBUNGE WA JIMBO LA TEMEKE ABBAS MTEMVU ATOWA MISAADA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM DAR ES SALAAM

Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu
 Baadhi ya misaada mbalimbali  iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu kwa watu wenye mahitaji maalum.


mwenyekiti wa Taasisi ya Sitti Tanzania Foundation , Sitti Mtemvu  akizungumza na walezi wa watu wenye mahitaji maalum, wakati Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  alipokabidhi misaada ya vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, mafuta ya kula, magodoro na kompyuta ambapo jumla ya vikundi kumi na vitatu vimepatiwa misaada mbalimbali na mbunge huyo.
 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu  akizungumza na walezi wa watu wenye mahitaji maalum, wakati alipokabidhi misaada ya vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, mafuta ya kula, magodoro na kompyuta ambapo jumla ya vikundi kumi na vitatu vimepatiwa misaada mbalimbali na mbunge huyo.
Baadhi ya vitu vilivyo tolewa na  Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu kwa watu wenye mahitaji maalum
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu akikabidhi misaada kwa Mlezi wa kituo cha Makao ya Taifa ya watoto wenye shida maalum cha kurasini  Beatrice Mgumilo



 Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (aliye vaa koti) akipiga makofi baada ya walezi wa vituo mbalimbali  kuomba Yamoto Band waimbe nyimbo moja
Mkurugenzi wa Mkubwa na Wanawe (Yamoto Band) akimshukuru Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu
Mbunge wa Jimbo la Temeke na Kamanda wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Mtemvu ametoa msaada wa vitu mbalimbali vya nafaka na magodoro pamoja na kompyuta kwa Yamoto Band ambapo jumla ya vikundi kumi na vitatu vimepatiwa misaada mbalimbali na mbunge huyo





Yamoto Band katika  Picha ya pamoja na baadhi ya Watoto wenye mahitaji maalum

Yamoto Band wakisalimia wazazi na watoto wenye mahitaji maalum
PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA

Sunday, July 5, 2015

KAMATI MAALUM YA CCM ZANZIBAR YAPITISHA JINA LA DKT. SHEIN KUGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, ambaye pia ni  Mjumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, akisalimiana na Rais wa Zanzibar, ambaye pia ni Makamu  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, wakati walipowasili kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria katika kikao cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar, ambacho leo kilipitisha jina la Dkt. Shein kuwania nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM. Picha na OMR
Makamu  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati Maalum ya CCM kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kupitisha jina la Mgombea Urais wa Zanziba kwa Tiketi ya CCM. (katikati) ni Mjumbe wa Kamati hiyo, ambaye aliongoza kikao baada ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti, Dkt.Mohammed Gharib Bilal na Mjumbe, Balozi Iddi. Picha na OMR
Kiti cha Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Shein, kikiwa wazi baada ya kukabidhi madaraka kwa wajumbe ili kujadili na kuteua jina la mgombea Urais wakati wa Kikao Maalum cha CCM, leo. Picha na OMR
Kaimu Mwenyekiti wa CCM, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao hicho maalum cha Kamati Maalum, baada ya kuteuliwa na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kushoto) ni Balozi Seif Iddi. Picha na OMR
 Dkt.Bilal na Balozi Iddi,wakifurahia baada ya Wajumbe kupitisha Jina la mgombea.

Mjumbe, Dkt.Bilal, akimpongeza Dkt. Shein baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe katika Kikao cha Kamati Maalum ili kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali. Picha na OMR
Mjumbe, Dkt.Bilal, akimpongeza Dkt. Shein baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe katika Kikao cha Kamati Maalum ili kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali. Picha na OMR
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.  Ali Mohammed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Malum, akiwashukuru baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar, katika Kikao kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Picha na OMR
Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.  Ali Mohammed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Malum, akiwashukuru baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar, katika Kikao kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. Picha na OMR
Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.
Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.
Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.