Tuesday, April 2, 2013

PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 ILIVYOFANA MWANZA




Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani akifungua utepe wa gitaa kuashiria uzinduzi wa Studio mpya za kurekodi muziki za COSU Studio zilizozinduliwa ndani ya tamasha la Muziki lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival ambalo nalo limeanzishwa rasmi mwaka huu jijini  Mwanza.


Nesta Sanga ni moja kati ya waimbaji waliosisimua ndani ya Gospel Festival tizama watu wa Mungu walivyomzunguka wakiimba naye. 




Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akifurahia yanayoendelea na Askofu Simeone Masunga wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Geita katika sherehe za Pasaka ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kwaya mbalimbali na waimbaji toka pande nyingi nchini walihusishwa.


Mwimbaji wa nyimbo za injili anayetamba Afrika Mashariki na Kati Neema Mwaipopo akiiimba wimbo wa 'Raha jipe mwenyewe' na wakazi wa Mwanza waliofurika uwanja wa CCM Kirumba kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013.


Waimbaji mbalimbali toka mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Arusha, wakimpa sapoti mwimbaji Neema Mwaipopo kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013 lililofanyika sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 


Hapa raha ya ufufuko ilimvuvia kila mmoja.


Mwimbaji nesta Sanga  akiimba wimbo ujulikanao kwa jina Twendeni huku akipewa sapoti ya kutosha.
Sura za watumishi wa muziki wa Injili zikiranda huku na huko kudadisi yanayoendelea.


Ni cheki ya 500,000/= toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mkolani Investiment (katikati) Suleiman Nguvu kuchangia uboreshaji wa vitendea kazi ndani ya studio za kisasa za COSU Studio ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa COSU Entertainment Fabian Fanuel (red tshirt) na Meneja wake Albert G. Sengo (kulia)


Wananchi hawakupitwa na shughuli za uwekaji kumbukumbu.

Jamani rahaaaaaaaa....Ndiyooooo....


Moja ya kwaya za jijini Mwanza zikihudumu.


Mwimbaji anayesisimua katika muziki wa injili akitamba na wimbo 'Zunguka' Enock Jonas akishusha upako...


Meza kuu ikijadili jambo.


Zunguka, zunguka, zunguka, zunguka eeeeeeeeeh!!!!!


Ilibidi muda usogee hata kiza kikaingia, tunamshukuru Mungu shughuli katika uwanja huu kwa kweli ilifana. Shukurani za dhati kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula, Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (twafahamu ni majukumu tu yamesababisha ukashindwa kuhudhuria), Mkurugenzi wa Sahara Media Group Dr. Anthony Diallo,  Michuzi Jr Blog na Kajunason Blog. 

Saturday, February 16, 2013

SHUHUDIA MING'ARO YA PICHA ZA VALLENTINE VILLA PARK

Mmoja kati ya waimbaji wa kundi la Jahazi Morden Taarab akiwa juu ya stage la Villa Park kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa Usiku wa Mwambao sambamba na kusherehekea sikukuu ya wapendanao duniani.


Mwanadada aliyependeza usiku huo alizawadiwa mizawadi toka kinywaji cha Reds.

Flowerz mwingine huyu alizawadiwa full seti ya Reds huku kushoto kabisa Mc Magoma akimeneji vinavyojiri.

Best couples  zilizo shine nazo zilitoka na mizawadi kibao toka Reds.

You cant c' Me

Hivi ndivy Papaa alitokelezea na mkewe katika usiku wa wapendanao Villa Park Mwanza.

Kwa kunyakuwa nafasi ya tatu Papaa alipata zawadi toka home Shoping Centre. 

Hawa ni washindi wa pili kwa Couples zilizopendeza nao walipata zawadi ya kulala Hotel JB Belamounte. 

Mc Magoma akitambulisha washindi nafasi ya kwanza kwa Couple zilizotokelezea usiku wa Vallentine Villa Park.

Washindi wa kwanza niiiiiiii........

Mwaaaaaa....!!!!! Hawa ndiyo washindi wa kwanza, nao walijipatia tiketi kwenda na kurudi dar kwa siku wanayotaka toka Precision Air.

Ni Mc Magoma (kushoto) na Dj John Lyatou (kulia) na nyuma yao Jahazi Morden Taarab. 

Hapa kila mmoja aliondoka na zawadi katika usiku wa wapendanao Villa Park  ukiambatana na uzinduzi wa Usiku wa Mwambao mara baada ya ukarabati mkubwa kufanyika

Hivi ndivyo rangi za hapa zilivyo someka toka dansing floo..

Guitalist.....

Ze eria...at Villa.

Live toka stejini.
We...

Mwanza nzima ilihamia hapa.

Thursday, January 3, 2013

BONDIA LULU KAYAGE AJIANDAA KUMKABILI SALMA KIHOBWA WA MOROGORO


Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro 



Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro 

Bondia lulu Kayage 'kulia' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, December 29, 2012

TASWA YAFANYA MKUTANO MKUU NA WANACHAMAWAKE BAGAMOYO MKOANI PWANI.


Baadhi ya wanachama wa TASWA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete. 

Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akizungumza katika mkutano Mkuu leo 

Baadhi ya wanachama wa TASWA wakiburudika katika hotel kubwa mjini bagamoyo ya Kiromo view Hotel jana usiku kutoka kushoto ni Somoe Ng'itu, Hadija Khalili' Zena Chande na Angela Msangi

Shafii Dauda akiwa na dada Asha Muhaji. 

Mmiliki wa blog ya Bongo Staz Mahmud Zubeir kulia akizungumza na Wiliam Chiwango na Salim Said Salim

Mjumbe wa mkutano huo, Rajabu Mhamila 'Super D' akijitambulisha kwa mgeni rasmi

 
Ni wanachama wa TASWA wakisikiliza mada mbalimbali.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete walipokutana katika mkutano mkuu wa Taswa

 

Mmoja wa waandishi wa habari Egbert Mkoko akitoa salamu kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TASWA. 


Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akitoa neno la shuklani kwa wajumbe waliohuzulia mkutano wakati wa kufunga mkutano huo.

Mwanachama wa Taswa Saleh Ally akichangia mada wakati wa mkutano huo.

 
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete pamoja na mweka hazini wa TASWA Sultani Sekilo walipokutana katika mkutano mkuu wa Taswa

 Picha na www.burudan.blogspot.com