Asamoah Gyan alifuta furaha ya bao la Rafael van der Vaart wakati Sunderland ilipoinyima ushindi Tottenham katika uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Lane.
Spurs walikuwa wakijitahidi kuipenya ngiome imara ya Sunderland katika kipindi cha kwanza, huku Tom Huddlestone akiachia mkwaju uliopiga mwamba kutoka umbali wa yadi 25.
Walifanikiwa kupata bao la kuongoza wakati Gareth Bale alipomimina krosi kutoka upande wa kushoto na baada ya Peter Crouch kuurudisha kwa kichwa karibu na lango, Van der Vaart akautuliza na kuujaza kimiani.
Sunderland walisawazisha wakati Gyan alipotumia makosa ya walinzi wa Tottenham kupachika bao la kusawazisha na kujipatia pointi moja.
Kwa matokeo hayo Tottenham wameendelea kusalia nafasi ya sita wakiwa na pointi 16 na Sunderland wapo nyuma yao nafasi ya saba wakiwa na pointi sawa 16.
No comments:
Post a Comment