Friday, July 17, 2015

AMINI SALIMINI AWANIA UBUNGEA JIMBO LA MKWAJUNI ZANZIBAR KUPITIA TIKETI YA CCM

Mtoto wa Komando Dk Salmin Amour Juma Amini Salimini achukua Fomu kogombea Jimbo la Mkwajuni Zanzibar akiwasili katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Gamba kwa ajili ya kuchukua Fomu kogombea Jimbo hilo, akisalimiana na Wananchi waliopo hapo. 
Mama wa Amini Salimi Bi Khadija Kasimi akisalimiana na Katibu Msaidi wa Ofisi ya CCM Wilaya Kaskazini A Unguja alipofika katika Ofisi hizo kumshindikiza Mtoto wake kuchukua Fomu ya Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar. 
Katibu Msaidizi wa Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Ndg Shafi Hamad akitowa maelezo kwa Mgombea kabla ya kumkabidhi fomu ya kuwania kuteuliwa kugombea Jimbo la Mkwajuni
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini akihesabu fedha kwa ajili ya kulipia Fomu ya kuomba kuteuliwa kugombea Ubunge kupitia CCM katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini Unguja Gamba.
Katibu Msaidi Ofisi ya CCM Wilaya ya Kaskazini a Unguja Ndg Shafi Hamad akimkabidhi Fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Amini Salimini, baada ya kukamilisha taratibu zote za malipo na kutimiza masharti ya Chama cha Mapinduzi.
Katibu Msaidi wa CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja akitowa maelezo kwa mgombea baada ya kumkabidhi fomu hiyo Ndg Amini Salimini.
Mgombea wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja  Amini Salimini akiwa katika picha ya kumbukumbu na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni kwa tiketi ya CCM, akiwa katika Ofisi za CCM Gamba.
Amini Salimini akiwa katika picha ya pamoja na familia yake baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge Jimbo la Mkwajuni Zanzibar.Akionesha fomu yake baada ya kukabidhiwa kwa hutua za ujazaji 
Amini Salimini akitoka katika Ofisi za CCM Wilaya ya Kaskazini A Unguja baada ya kuchukua fomu hiyo akionesha kwa wananchi walioko katika eneo hilo.
Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Wilaya ya Kaskazini A Unguja Amini Salimini akiwa na Mtoto wake wa Kwanza wakishikilia fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuiwakilisha CCM katika Jimbo la Mkwajuni Zanzibar. 
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Amani Salimini akiomba dua katika makaburi ya Wazee wake huko Kidombo baada ya kuchukua Fomu ya kuwania Ubunge wa Jimbo la Mkwajuni Zanzibar
Amini Salimini akipata dua kutoka kwa Wazee wa Kijiji cha Kidombo Mkwajuni baada ya kuchukua Fomu ya Kugombea Ubunge wa Jimbu la Mkwajuni Zanzibar kupitia CCM

No comments:

Post a Comment