Mgombea Ubunge Jimbo la Bagamoyo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Juma Salum Yungwe, akionesha fomu ya kugombea nafasi hiyo baada ya kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Kombo Kamote wilayani humo leo mchana.
Katibu Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Bagamoyo, Salum Mtelela (kulia), akimkabidhi stakabadhi ya malipo ya kuchukua fomu, Mgombea huyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Bagamoyo, Kombo Kamote (kushoto), akimkabidhi fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Bagamoyo, Mathew Juma Salum Yungwe wilayani humo leo mchana. Wa pili kulia ni Mama mzazi wa mgombea, Mary Yungwe na Meneja wa Kampeni wa mgombea huyo, James Mbuligwe.
Hapa mgombea huyo Mathew Yungwe, akionesha fomu hiyo baada ya kukabidhiwa.
Makada wa CCM wakimpongeza Mgombea huyo wakati wa kuchukua fomu hiyo.
Mgombea nafasi hiyo ya Ubungo Jimbo la Bagamoyo, Mathew Yungwe (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mama yake Mary Yungwe (kulia) na Meneja wa Kampeni wake, James Mbuligwe.
Hapa mgombea huyo na mama yake na meneja kampeni wake wakiondoka ofisi ya CCM Wilaya ya Bagamoyo baada ya kukabidhiwa fomu yake.
No comments:
Post a Comment