Wednesday, July 15, 2015

JUMAA MHINA 'PIJEI' ACHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KAWE, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE

Hapa ikionesha fomu baada ya kukabidhiwa.
 Kada wa CCM Jumaa Mhina 'Pijei' (katikati), akipokea fomu ya kuwania ubunge Jimbo la Kawe jijini Dar es Salaam, kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe leo mchana. Anaye shuhudia kulia ni Kada wa chama hicho anayewania ubunge jimbo la Iringa mjini kupitia CCM, Ramadhan Ndanga 'Potipoti'.
 Katibu wa CCM Wilaya ya Kinondoni, Athuman Sheshe (kushoto), akimpa maelezo ya kufuata baada ya kukabidhiwa fomu hizo.
Waandishi wa habari wakimuhoji nini atawafanyia wananchi wa Jimbo la Kawe iwapo atachaguliwa.

Na Mwandishi Wetu

MUWANIA nafasi ya Ubunge Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jumaa Mhina 'Pijei' amesema akipata nafasi hiyo atashirikiana na wananchi wa jimbo hilo katika kutatua changamoto zilizopo.


Hayo aliyasema wakati akichukua fomu ya kugombea nafasi hiyo Dar es Salaam leo mchana na utaja vipaumbele vyake vya maendeleo atakayofanya.

Alisema mwaka 2010 aligombea lakini katika kura za maoni ya ccm hazikutosha, mwaka huu anaamini zitatosha na kulikomboa jimbo lililo mikononi mwa wapinzani.

Alisema kipaumbele chake ni ajira kwa vijana, elimu, miundimbinu ya barabara na umeme na kuwa mafanikio hayo yatakuja iwapo atashirikiana kwa karibu na wananchi hivyo aliomba wananchi kuto muangusha wakati ukifika.

Alisema tayari ametoa ajira kwa vijana kwa kuwapa bodaboda ambazo zimepunguza tatizo la ajira na vitendo vya uhalifu katika jimbo hilo.

Mhina alisema kipaumbele kingine atakacho kitoa ni kuhakikisha anatumia uzoefu wake wa ujasiriamali kwa kuwajengea uwezo wanawake na vijana kwa kuwapa elimu na kuwawezesha kupata mikopo yenye riba nafuu ili kuinua mitaji yao.

No comments:

Post a Comment