Tuesday, April 2, 2013

PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 ILIVYOFANA MWANZA
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani akifungua utepe wa gitaa kuashiria uzinduzi wa Studio mpya za kurekodi muziki za COSU Studio zilizozinduliwa ndani ya tamasha la Muziki lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival ambalo nalo limeanzishwa rasmi mwaka huu jijini  Mwanza.


Nesta Sanga ni moja kati ya waimbaji waliosisimua ndani ya Gospel Festival tizama watu wa Mungu walivyomzunguka wakiimba naye. 
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akifurahia yanayoendelea na Askofu Simeone Masunga wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Geita katika sherehe za Pasaka ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kwaya mbalimbali na waimbaji toka pande nyingi nchini walihusishwa.


Mwimbaji wa nyimbo za injili anayetamba Afrika Mashariki na Kati Neema Mwaipopo akiiimba wimbo wa 'Raha jipe mwenyewe' na wakazi wa Mwanza waliofurika uwanja wa CCM Kirumba kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013.


Waimbaji mbalimbali toka mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Arusha, wakimpa sapoti mwimbaji Neema Mwaipopo kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013 lililofanyika sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 


Hapa raha ya ufufuko ilimvuvia kila mmoja.


Mwimbaji nesta Sanga  akiimba wimbo ujulikanao kwa jina Twendeni huku akipewa sapoti ya kutosha.
Sura za watumishi wa muziki wa Injili zikiranda huku na huko kudadisi yanayoendelea.


Ni cheki ya 500,000/= toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mkolani Investiment (katikati) Suleiman Nguvu kuchangia uboreshaji wa vitendea kazi ndani ya studio za kisasa za COSU Studio ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa COSU Entertainment Fabian Fanuel (red tshirt) na Meneja wake Albert G. Sengo (kulia)


Wananchi hawakupitwa na shughuli za uwekaji kumbukumbu.

Jamani rahaaaaaaaa....Ndiyooooo....


Moja ya kwaya za jijini Mwanza zikihudumu.


Mwimbaji anayesisimua katika muziki wa injili akitamba na wimbo 'Zunguka' Enock Jonas akishusha upako...


Meza kuu ikijadili jambo.


Zunguka, zunguka, zunguka, zunguka eeeeeeeeeh!!!!!


Ilibidi muda usogee hata kiza kikaingia, tunamshukuru Mungu shughuli katika uwanja huu kwa kweli ilifana. Shukurani za dhati kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula, Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (twafahamu ni majukumu tu yamesababisha ukashindwa kuhudhuria), Mkurugenzi wa Sahara Media Group Dr. Anthony Diallo,  Michuzi Jr Blog na Kajunason Blog. 

No comments:

Post a Comment