Mr Chabaka akitoa pete PETE ambayo ni Diamond ya Ukweli Wachumba wakiwa na baadhi ya marafiki zao na familia Wapenzi wakiwashukuru wageni waalikwa. Ni sherehe fupi ya kuvalishana pete ya Uchumba iliyofanyika Jumamosi Tarehe 22 Oktoba 2011 kati ya Naibu Balozi wetu Mh.Chabaka na Bi Irene. Sherehe hii ilihudhuriwa na baadhi ya ndugu pamoja na marafiki wa karibu waliojumuika kwa pamoja kushuhudia tukio hili muhimu katika safari yao ya kuelekea kwenye ndoa.
Vazi alilovaa Bi Irene limebuniwa na kutengenezwa ramsi na Anna Lukindo. Tarehe na pamoja taratibu zote za harusi zitatolewa rasmi muda muafaka utakapowadia.
Hivyo basi Blogu hii pamoja na Urban Pulse Creative na Miss Jestina George tunapenda kuwapa hongera na fanaka katika penzi lao na maisha yao ya baadae, Mungu Awabariki.
Leo ni siku ya kuadhimisha miaka kaadha ya kuzaliwa kwake Reuben Ndege wa Clouds Media Group, Wengi wakimtambua kama Nchakali aka Mzeeeyaa!! anayesomeka mwanzo mwisho ndani ya program lenye fuul ditelZ za Mastaa, Muziki na wanamuziki duniani Soso Fresh, at the same time ndiye anayeng'arisha kipindi cha kijanja ndani ya clouds radio XXL katika segment ya 255.
Blogu hii inaomba mkono wa baraka toka kwa Mwenyezi Mungu kwa kila kilicho chema ukigusacho.