Monday, June 11, 2012

MPAMBANO KATI YA MSONDO NA SIKINDE KUSINDIKIZA SHEREHE ZA VILLA PARK KUTIMIZA MIAKA MITANO

Villa Park Resort Mwanza inaadhimisha miaka mitani tangu kuanzishwa kwake, shamrashamra zitaanza wiki hii siku ya alhamisi katika usiku wa Mwambao ambapo mwanamama Jokha Kassimu atatoa burudani akichagizwa na Kanga Moko Ndembendembe kwa kiingilio cha sh 3000/=


Vilevile kwa mujibu wa mratibu mkuu wa soka Mzee Halphan Ngasa amesema kuwa kutakuwa na ligi ya mtoano (Villa Soccer Bonanza) ambapo timu za Mashabiki na wafanyakazi za Villa Sports Club, Lakairo Sports Club, Victoria Sports Club na Shooters Sports Club zitachuana.


Mshindi wa kwanza kwenye ligi hiyo ya mtoano kupata kombe kubwa, mbuzi na kreti ya kinywaji kutoka wadahamini TBL, mshindi wa pili kunyakuwa kombe na kreti mbili za kinywaji toka TBL, mshindi wa tatu ataondoka na kombe na kreti moja ya kinywa cha TBL


Lengo la mashindano hayo ni kuboresha afya na kusisitiza umuhimu wa mazoezi kwa jamii hususani watu wazima.

Burudani nyingine siku ya Ijumaa katika Compass Night na Miaka mitano ya Villa Park Dj PQ (Clouds fm) na Dj Mafuvu (East Africa Radio) na maDj wote wa Villa Park (Dj John Lyatow, Dj Samm, Dj Chriss) kumwaga burudani usiku huo kiushindani zaidi.

Katika usiku  wa Jumamosi Sambamba na disco kali ndani ya Villa Disco Teque vilevile uwanja wa nje kutakuwa na mpambano awamu ya kwanza wa Bendi za Msondo, Sikinde na bendi ya jijini Mwanza Super Kamanyola kiingilio usiku huo shilingi 5,000/= na shilingi 7,000/= kuzama hadi ndani.


Jumapili kuanzia saa 12 jioni ni Mpambano wa kukata na Shoka kati ya Bendi tatu kongwe hapa nchini zenye mashabiki wengi kama Simba na Yanga nazungumzia Msondo, Sikinde na Super Kamanyola nani zaidi?

No comments:

Post a Comment