Wednesday, December 19, 2012

Mh. Lowassa azindua josho la kisasa kwa mifugo kijiji cha Mfereji Monduli Juu

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo katika kijiji cha Mfereji Monduli juu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikaribishwa kwenye kijiji cha Mfereji Monduli juu,wakati alipokuwa akiwasili kijijini hapo kwa ajili ya shughuli ya uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akifunua kitambaa kwenye jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu,mara baada ya kuzindua josho la kisasa la Mifugo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa josho la kisasa la Mifugo,lililoko katika Kijiji cha Mfereji,Monduli Juu.
Mifugo ikiingizwa kwenye Josho hilo,mara baada ya kuzinduliwa.
Wakazi wa kijiji cha Mfereji,Monduli juu wakimsikiliza Mh. Lowassa (hayupo pichani).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Monduli juu,Mkoani Arusha wakati wa hafla ya uzinduzi wa josho la kisasa katika kijiji cha Mfereji Monduli juu. ambapo ametoa wito kwa wakulima na wafugaji nchini kuacha uhasama wa kugombea ardhi.

Amesema kuwa kila mtu ana haki yake hivyo ni muhimu kwa jamii hizo kuheshimiana na kukaa pamoja kutatua tatizo la ardhi kwa ajili ya malisho ya mifugo pamoja na kilimo.Kumekuwa na matokeo mengi sehemu mbalimbali ya kupigana kuwania ardhi kati ya wakulima na wafugaji, miongoni mwa maeneo hayo ikiwa ni mkoani arusha.

Amewaambia watu wa jamii ya kimasai ambao ni wafugaji kuingia katika ufugaji wa kisasa utakaowazuia kuhama hama kutafuta malisho ya mifugo yao.''Jamani watanzania wenzetu hawatakubali mtakapovamia maeneo yao bila ya ruhusa ni lazima tuondokane na tabia hii'' alisema.

No comments:

Post a Comment