Sunday, December 16, 2012

TPBC YAWATAKIA WATANZANIA WOTE KHERI YA CHRITSMAS!


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
December 16, 2012

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) inapenda kuchukua fursa hii adimu kuwatakia Watanzania wote sikuu njema ya Kristmas pamoja mwaka mpya ujao wa 2013. Katika mwaka unaoishia tarehe 31 mwezi huu wa 12, TPBC inapenda kutoa shukrani zake za dhati kwa wadau wote wa ngumi waliosaidia kwa namna moja au nyingine katika maendeleo ya ngumi za kulipwa Tanzania.

TPBC inatambua wazi mchango wa wadau mbalimbali katika kukuza tasnia ya ngumi za kulipwa Tanzania.

1. MABONDIA

TPBC inapenda kuwashukuru mabondia wote waliojitokeza kugombea mataji yake mwaka 2012 katika uzito mbalimbali. Michango yao kwenye kukuza ngumi za kulipwa ni mkubwa sana hususan katika kukuza ajira na burudani. TPBC inachukua fursa hii kuwapongeza mabingwa wake wote katika mwaka 2012.

Aidha TPBC inependa kuchukua fursa hii kuwashukuru sana mabondia wote wa Kitanzania waliocheza nje ya nchi kwa kuitangaza vyema Tanzania. Mchango wao umeongeza na kukuza Utalii wa Michezo kwa Tanzania kwa kiwango kikubwa.

2. MAPROMOTA (WAKUZAJI), MAMENEJA NA MAKOCHA

TPBC inapenda kuwashukuru mapromota, mameneja na makocha wote waliojitokeza na kusaidia kupromoti mapambano mbalimbali mwaka 2013. Mchango wao ni mkubwa sana katika tasnia ya ngumi za kulipwa na tunazidi kuwaomba waendelee kukuza ngumi za kulipwa kwa manufaa ya taifa na wadau wenyewe.


3. VYOMBO VYA HABARI

Vyombo vya habari vikiwamo magazeti, radio, tv, blogs, tovuti, na vinginevyo vimetoa mchango mkubwa sana kwa TPBC katika kufikia malengo yake katika mwaka 2012. Wakati tukimaliza mwaka huu, tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa vyombo vyote vya habari na wanahabari wenyewe katika kukuza ngumi za kulipwa Tanzania.

4. WADHAMINI

TPBC inatambua kuwa mchango mkubwa wa wadhamini katika kukuza ngumi za kulipwa ni muhimu sana. Hivyo tunatoa shukrani kwa wadhamini mbalimbali ambao walitoa mchango wao katika kipindi kinachoishia mwaka 2012 katika kukuza ngumi za kulipwa Tanzania. Tunapenda kuwaomba wadhamini hao na wengine wengi ambao wanaipenda nchi yao kujitokeza kwa wingi katika kuchangia na kukuza tasnia ya ngumi katika mwaka ujao wa 2013 ili Tanzania iweze kwenda mbali zaidi.

5. VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA:

TPBC inapenda kuvishukuru sana vyombo vya ulinzi na usalama vikiongozwa na jeshi la Polisi katika kutoa ulinzi imara wakati wa mapambano mbalimbali katika mwaka huu unaoishia 2012. Mchango wao umesaidia sana katika kulinda usalama wa wadau wa ngumi pamoja na mabondia wenyewe mwaka huu, tunawaomba wazidi kuendelea kutoa ulinzi hususan wakitimiza malengo ya Polisi jamii.

6. MAMLAKA ZA MIJI:

Tunapenda pia kuwashukuru sana mamlaka za miji katika Halmashauri za Manispaa za miji yote ambayo yalisadia wakati wa mapambano mbalimbali yaliyofanyika mwaka 2012. Tunawaomba wazidi kutoa ushirikiano wao katika kipindi cha mwaka 2013.

7. MSAJILI WA VYAMA WIZARA YA MAMBO YA NDANI

TPBC inapenda kushukuru sana ofisi ya Msajili wa Vyana Wizara ya Mambo ya Ndani kwa msaada na ushirikiano wake katika kuendeleza ngumi za kulipwa Tanzania. Tunatambua mchango wake katika kuendeleza ngumi kupitia usimamizi wa ofisi yake kwa vyama vilivyoandikishwa katika ofisi yake kikiwamo TPBC.

8. KURUGENZI YA MAENDELEO YA MICHEZO

TPBC inapenda kutoa shukrani zake nyingi kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini kwa msaada, ushauri na ushirikiano wake katika kusaidia kufikia malengo yake mwaka huu 2012. Tunaomba ushirikiano huu uzidi kuendelea ili tasnia ya ngumi izidi kukua na kuifanya Tanzanai nchi yenye mabondia wazuri duniani.

9. BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA (BMT)

Tunapenda kuchukua fursa hii kuwashukuru viongozi na maofisa wa Baraza la Michezo la Taifa kwa mchango wao katika kukuza ngumi za kulipwa Tanzania. BMT walitoa misaada yote ambayo TPBC iliomba katika mwaka huu na tunaomba ushirikiano wetu uzidi kuendelea mwaka 2013.


10. WADAU WENGINE WOTE

TPBC inapenda kutoa shukrani zake kwa wadau wote ambao hawakutajwa hapo juu lakini walitoa michango wao katika kukuza ngumi za kulipwa nchini. Tunaenzi sana michengo yenu mungu awabariki.

11. MIPANGO YA MWAKA 2013

TPBC ina mipango kadhaa katika mwaka ujao wa 2013 ikiwamo pamoja na:

1. Kukuza ushirikiano wa karibu na mashirikisho mbalimbali ya michezo ndani na nje ya nchi ili kukuza tasnai ya nguni za kulipwa Tanzania na nje ya nchi kwa manufaa ya mabondia wa kitanzania.
2. Kufanya uchaguzi wake katika mikoa yote na baadaye taifa kuanzia March 2013
3. Kuidhinisha mapambamo mbalimbali ya ubingwa wa mikoa, kanda, taifa na kimataifa
4. Kufanya semina ya maofisa wa ulingo, mapromota, mameneja pamoja na makocha
5. Kuwatafutia mabondai wa kitanzanai ubingwa mbalimbali nje ikiwa ni pamoja na mataji mapya ya Jumuiya ya Madoka kwa bara la Afrika
6. Kuhamasisha watanzania wengi waweze kuwa mapromota (wakuzaji)
7. Kuwahamasisha wadhamini wengi ili kudhamini ngumi za kulipwa
8. Kushirikiana na mapromota na kuwaalika mabondia maarufu duniani kuzuru Tanzania ili kujenga heshima ya ngumi na kuitangaza nchi.
9. Kukuza na kuchangia sekta ya Utalii wa Michezo kwa kuwatumia mabondia wa Kitanzania watakaopigana nje ya nchi kuitangaza vyema Tanzania.

Tunapenda kusema tena:

Watanzania, Kheri ya Kristmas na mwaka mpya 2013.

Merry Xmas and Happy New Year 2013 Tanzanians,

Imetolewa na:


Onesmo A.M.Ngowi
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)
Registered as Societies (Application for Registration) Rules 5, 1954, by United Republic of TANZANIA
Technology House, 35-38 Ghalla Road,
P.O BOX 1106, Moshi - Tanzania
Cell: + 255-754-360828

No comments:

Post a Comment