Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Tuesday, October 22, 2013

REDD'S UNI-FASHION BASH JIJINI MWANZA ILIKUWA RAHA TUPU.

Full Ubunifu toka kwa wanavyuo washiriki.
Wowu...!!!
Kama mamtoni vile..!!
African thing...!! 
Kaba penati...!!
Wadau mbalimbali waliohudhuria Tamasha hilo wakifuatilia kwa umakini..
Burudani ilidondoshwa na Ngosha The Swagga Don Fid Q.
On the one and two alisimama DVJ Denis' wa Rock Bottom.
 Meneja wa Mauzo ya Rejareja wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda la Ziwa, Andrew Mbwambo (kulia) akikabidhi kitita cha Sh. Laki 5 kwa Mshindi wa Kwanza wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash,Fahad Rajab (kutoka Chuo cha Mt. Augustine ya jijini Mwanza) baada ya kuwagaragaza wenzake, katika Tamasha lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.
Washindi wa Mitindo kwenye Redd's Uni-Fashion Bash, na mikwanja yao katika Tamasha lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini, Mwanza.
Wadau mbalimbali waliohudhuria Tamasha hilo lililofanyika kwenye Bustani ya Charcoal Ribs Beach Resort jijini,Mwanza.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Thursday, January 3, 2013

BONDIA LULU KAYAGE AJIANDAA KUMKABILI SALMA KIHOBWA WA MOROGORO


Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro 



Bondia lulu Kayage 'kushoto' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake katika kambi ya Amana CCM Ilala ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro 

Bondia lulu Kayage 'kulia' akioneshana uwezo wa kutupiana makonde na Mohamedi Chipota wakati wa Mazoezi yake ya kujiandaa na mpambano wake na Salma Kihobwa utakaofanyika February 2 katika uwanja wa Jamuhuri Morogoro Picha nawww.superdboxingcoach.blogspot.com

Saturday, December 29, 2012

TASWA YAFANYA MKUTANO MKUU NA WANACHAMAWAKE BAGAMOYO MKOANI PWANI.


Baadhi ya wanachama wa TASWA wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete. 

Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akizungumza katika mkutano Mkuu leo 

Baadhi ya wanachama wa TASWA wakiburudika katika hotel kubwa mjini bagamoyo ya Kiromo view Hotel jana usiku kutoka kushoto ni Somoe Ng'itu, Hadija Khalili' Zena Chande na Angela Msangi

Shafii Dauda akiwa na dada Asha Muhaji. 

Mmiliki wa blog ya Bongo Staz Mahmud Zubeir kulia akizungumza na Wiliam Chiwango na Salim Said Salim

Mjumbe wa mkutano huo, Rajabu Mhamila 'Super D' akijitambulisha kwa mgeni rasmi

 
Ni wanachama wa TASWA wakisikiliza mada mbalimbali.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete walipokutana katika mkutano mkuu wa Taswa

 

Mmoja wa waandishi wa habari Egbert Mkoko akitoa salamu kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa TASWA. 


Katibu Mkuu wa TASWA Amir Muhando akitoa neno la shuklani kwa wajumbe waliohuzulia mkutano wakati wa kufunga mkutano huo.

Mwanachama wa Taswa Saleh Ally akichangia mada wakati wa mkutano huo.

 
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' kushoto  akiwa na Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys, Ridhiwan Kikwete pamoja na mweka hazini wa TASWA Sultani Sekilo walipokutana katika mkutano mkuu wa Taswa

 Picha na www.burudan.blogspot.com

Saturday, December 15, 2012

MAANDALIZI YA PAMBANO LA CHEKA NA MMLAWI CHIMWEMWE YAKAMILIKA



MAANDALIZI la pambano la Francis Cheka na bondia Chiotka Chimwemwe toka Malawi litakalochezwa Desemba 26 mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Abeid Amani Karume jijini Arusha yamekamilika.

Akizungumza  jijini Dar es Salaam promota wa pambano hilo Andrew George amesema taratibu za mchezo huo umekamilika.

"Taratibu zote za pambano zimekamilika kwa asilimia 90 ikiwa pamoja na kumtumia tiketi bondia Chiotka Chimwemwe", alisema George.

George alisema ameamua kulipeka pambano hilo Arusha kwa kuwa anaamini watu wa Arusha wanapenda ngumi na siku hiyo ni siku ya sikukuu hivyo watakuja kwa wingi pamoja na familia zao kwani pambano litaanza saa nane mchana.

Pia alisema mabondia watapima uzito siku ya sikukuu ya krismasi jijini Arusha.

Pambano hili litakuwa ni la raundi 12 na Mmalawi huyu anajigamba atampiga Cheka ndani ya ardhi ya nchi yake hivyo kuwasihi watanzania kuja kwa wingi kwani hata ulinzi utakuwepo wa kutosha, alisema George 


MOJA YA MABANGO YALIYOTAPAKAA JIJINI ARUSHA KWA SASA KUHUSU MPAMBANO HUO

Sunday, July 15, 2012

YUSUF MANJI MWENYEKITI YANGA, MAKAMU WAKE CLEMENT SANGA

Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manjikulia na Makamu mwenyekiti Clement Sanga wakiwa katika uchaguzi huo jana
Habari kwa hisani ya dinaismailblogspot.com
Yusuf Manji amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa klabu ya Young Africans Sports Club, uchaguzi ulioitishwa kujaza nafasi zilizoachwa wazi, kufuatia kujiuzuru kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji, mwenyekiti na makamu wake.
Akitangaza matokeo hayo, majira ya saa 10:30 alfajiri katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi wa klabu ya Yanga Jaji John Mkwawa amemtangza Manji kama mishindi wa nafasi ya uenyekiti kufuatia kupata asilimia 97% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi hiyo.

Nafasi ya Makamu Mwenyekiti imekwenda kwa Clement Sanga aliyejipatia asilimia 62% ya kura zote zilizopigwa katika nafasi ya u makamu mwenyekiti.
Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaron Nyanda na George Manyama wamechaguliwa katika nafasi ya ujumbe wa kamati ya Utendaji.
Jaji Mkwawa amewashukuru wana Yanga kwa kuwa wastaarabu na watulivu, kitu kilicholekea kufanyika uchaguzi kwa amani na zoezi hilo kumalizika salama pasipo kuwa na rabsha yoyote.
Matokeo kamili ya wagombea ni:


Nafasi ya Mwenyekiti:
Yusuf Manji  (kura 1876) 97.0%, John Jembele (kura 40) 2.6%, Edgar Chibura (kura 4) 0.24%


Nafasi ya Makamu Mwenyekiti:
Clement Sanga (kura 1948) 62.6%, Yono S Kevela (kura 475) 23%,  Ayoub Nyenzi (kura 288) 14%


Nafasi ya Ujumbe:
Abdallah Bin Kleb (kura 1942), Moses Katabaro (kura 1068),  Aaron Nyanda (kura 922), Geroge Manyama (kura 682), Beda Tindwa (kura 391), Edgar Fongo (kura 295), Graticius Ishengoma (kura 247), Jumanne Mwamenywa (kura 251), Justine Baruti (610), Lameck Nyambaya (kura 425), Omary Ndula (kura 170), Peter Haule (441), Ramadhan Said (249), Yono Kivela (123)


kutokana na matokeo yalivyo hapo juu safu ya viongozi waliochaguliwa ni
Mwenyekiti: Yusuf Manji,
Makamu Mwenyekiti: Clement Sanga
Wajumbe: Abdallah Bin Kleb, Moses Katabaro, Aaaron Nyanda, Geroge Manyama

Thursday, May 31, 2012

UJIO WA THE MBONI SHOW: MAHOJIANO NA HOST WAKE,MBONI MASIMBA

Kuanzia Alhamisi hii, taswira za vipindi vya luninga nchini Tanzania haitokuwa kama ile ambayo wengi wetu tumeizoea. Kuna kitu kipya na cha aina yake. Ni Talk Show inayokwenda kwa jina The Mboni Show ambayo mwenyeji au host wake ni mwanadada Mboni Masimba.

The Mboni Show, kitakuwa kinarushwa kila siku ya Alhamisi, Saa 3 Kamili Usiku Mpaka Saa 4 na kisha marudio yake yatakuwa yanafanyika Saa 7 Mchana na Saa 10 jioni siku ya Jumamosi. Kwa maana hiyo ni kipindi ambacho,bila shaka, kitakufanya usibanduke hapo utakapokuwa ukikitazamia kwa muda wa takribani saa 1. Yote hayo ni kupitia kituo cha televisheni cha EATV(East Africa Television).

Lakini Mboni Masimba ni nani? Kipindi chake kitahusu nini na kitakuwa na tofauti gani kutoka katika vipindi vingine kadhaa vilivyoko katika stesheni mbalimbali za luninga? Ili kupata majibu kwa maswali hayo na mengine,nilimtafuta Mboni Mashimba. Haya hapa ni mazungumzo yetu; BC: Mboni, Karibu sana ndani ya BC. Mambo vipi?

MM: Mambo poa tu Jeff za kwako?

BC: Za kwangu nzuri Mboni. Asante kwa kukubali kufanya nami mazungumzo haya. Kwa kuanzia tu,Jina lako ni la kipekee kidogo…Mboni. Lina maana gani jina lako? Wazazi waliwahi kukwambia kwanini walikuita Mboni?

MM: Yeah ni kweli…jina langu ni la kipekee. Mimi ni Mboni…ile mboni ya Jicho. Kama unavyojua, mtu huwezi kuchezea Mboni ya jicho yako. Ukifanya hivyo utakuwa unajitafutia balaa. Mboni ni kitu cha kuangaliwa sana kwa sababu kipo very sensitive. Mama yangu aliniambia kwamba waliamua kuniita Mboni kwa sababu ni kitu cha thamani.Kwa maana hiyo nina thamani kubwa kwao na hususani ukizingatia kwamba mimi ni mtoto wa mwisho kwa mama yangu… Ha ha ha haaaaa

BC: Mara nyingi tunapokuwa watoto huwa tuna ndoto kibao za kuja kuwa watu fulani au kuwa kama fulani na fulani. Unakumbuka mambo gani muhimu wakati wa utoto wako. Na je unachokifanya hivi leo ni ndoto yako ya toka utotoni au la?

MM: Kwa kusema ukweli ndoto yangu toka nikiwa mdogo ilikuwa ni kupenda kuja kuwa mfanyabiashara mkubwa mwenye hela nyiiingi sana. Na pia nilikuwa natamani sana siku moja niwe Mbunge au Waziri. Kuwa na Talk Show haikuwa ndoto yangu hapo awali. Lakini kama unavyojua,maisha huenda yakibadilika na kadri mtu unavyokuwa na fikra tofauti nazo humjia mtu. Na lazima wakati fulani tukubaliane na ukweli kwamba sio kila ndoto inaweza kuja kweli. Hivyo basi, ni muhimu kwenda na wakati na jinsi dunia inavyokwenda na pia kutumia nafasi zinazojitokeza.

BC: Kwa kiasi kikubwa hivi leo wewe ni msichana maarufu nchini Tanzania. Lakini kuna watu ambao wanasema hawaelewi au hawajui chanzo hasa cha umaarufu wako. Wewe binafsi unadhani au unauelezeaje umaarufu wako.Nini chanzo?

MM: Binafsi naweza hisi labda umaarufu ulianzia niliposhiriki shindano la ulimwende la Miss Mbeya na Miss Southern Highland mwaka 2000 na hatimaye kushiriki Miss Tanzania mwaka huo huo.Lakini kama hiyo sio sababu basi naweza kusema labda ni kutokana na jinsi nilivyo mtu wa watu.Mara nyingi nimekuwa mstari wa mbele katika kujitolea kwa wenzangu,watanzania wenzangu kwa chochote kile ambacho ninakuwa na uwezo nacho. Isitoshe mimi ni mtu ambaye napenda sana kujichanganya na watu wa rika zote bila kubagua. Anyway, I was Born to Be a STAR ha ha ha haaaa

BC: Naam, sasa tuongelee kitu ambacho umekianzisha hivi karibuni. The Mboni Show. Hongera sana kwa hatua hiyo.Ilikuwaje wazo la kuanzisha The Mboni Show likakujia? Ni wazo binafsi au ushauri uliopewa na mtu?

MM: Naweza kusema ni mchanganyiko wa ushauri wa watu na instincts zangu mwenyewe. Sema kuna rafiki zangu kadhaa walianza kuniambia kama miaka minne iliyopita. Sikuchukulia maanani sana.Then mwaka 2010 nikiwa na rafiki yangu mmoja tunakula zetu mihogo pale Coco Beach kwa jamaa mmoja muuza mihogo maarufu kwa jina la ITV, akanishawishi tena kuhusu suala hili. Then nkaanza kutake serious. Nakumbuka aliniambia hivi wewe hujiulizi kwanini mara kwa mara unaitwa kwenye tv interviews na katika most of then ukienda huwa baadae unapata reviews nzuri? Basi kuanzia hapo ndio nkaweka msisitizo zaidi katika Talk show.Matokeo yake ndio hapa tulipo hivi sasa.



BC: Katika pitapita yangu ya mitandaoni nimesoma mahali kwamba Oprah ni miongoni mwa wanawake wanaokuvutia sana na yeye ni sababu mojawapo ya w ewe kuanzisha The Mboni Show ikiwa kama hatua mojawapo ya kufanya kile ambacho amekuwa akikifanya. Kuna ukweli wowote katika hilo?

MM: Ni ukweli kabisa kwamba Oprah Winfrey ananivutia kupita kiasi. Pamoja na hayo show yangu haitokuwa ki-Oprah moja kwa moja. Sitaki na wala siwezi kumuiga kwa kila kitu. Ntakachofanya mimi ni kuchukua yale ambayo naweza kuyachukua na hususani kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania zaidi. The Mboni Show ni show ya kitanzania kwa ajili ya watanzania.

BC: Katika maelezo ya awali ya The Mboni Show umeeleza kwamba malengo ya show yako ni kuelimisha, kuhamasisha na kusaidia jamii ya watanzania. Mmejipanga vipi kufikia malengo hayo?

MM: Yaani Jeff you will be Suprised .Wewe subiri tu utajionea.Lakini ki-ukweli The Mboni Show imejipanga vilivyo. Nawaambia The Mboni Show ndio kimbilio la Watanzania na mwokozi wao ha ha ha ha

BC: Mlolongo wa kuanzisha TV show ni mrefu na bila shaka umepambana na vikwazo kadhaa mpaka kufikia hatua hii. Unaweza kunieleza kidogo kuhusu vikwazo ulivyopitia na kitu gani kilikuwa kinakupa msukumo kwamba endelea tu usikate tamaa?

MM: Jeff sio kitu rahisi kama watu wanavyofikiria. Mimi na timu yangu tumeanza production since April last year na imagine ndio kwanza tumemaliza juzi juzi.Ni wazi kwamba katika kutimiza lengo au azma hii nimepitia vikwazo vingi ambavyo kwa kweli nisingesimama imara ningeweza kabisa kukata tamaa. Lakini mwisho ya yote namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kunisaidia mpaka kufika hapa. Kwa upande wa kitu ambacho kilikuwa kinanipa msukumo naweza kusema ni asili yangu ya kuwa mvumilivu na mbishi sana ninapotaka la kwangu. Hizo ndizo silaha zangu; uvumilivu na ubishi wenye manufaa. Vikwazo vilikuwa vingi sana ingawa sitopenda kuvitaja.Kwa ufupi nawaambia sio kitu kirahisi hata kidogo, ni kukomaaa tu mpaka kieleweke.

BC: Tunaposikia mtu anaanzisha kipindi cha televisheni kuna maswali kadhaa yanakuja. Je kitakuwa ni kipindi cha kurekodiwa ndani ya studio maalumu au kitakuwa kipindi cha kurekodiwa nje ya studio kwa maana ya mtaani nk. Kwa upande wenu format ya production ya The Mboni Show imekaaje?

MM: Kwa upande wetu tuna sehemu maalum ya kurekodia kama hii session ya kwanza vipindi vyote tulirekodia pale Serena( zamani ilikuwa ikiitwa Movenpick). Nawashukuru sana Serena kwa mchango wao katika kufanikisha hili. Next session itakuwa the same japo huwa tunatoka kidogo na kurekodi nje. Kuna mtu ambaye tumerekodi naye nje na hivi karibuni tunapanga kuingia mtaani. The Mboni Show ni kwa ajili yenu watanzania. Popote tutawafuata.

BC: Upo ukweli kwamba Hosts wengi wa TV show huwa yawabidi wawe na tabia ya kujisomea sana ili kupata mawazo na mitazamo mipya kila mara na kwenda na wakati. Je, na wewe pia una hulka hiyo au umejipanga namna gani katika kuhakikisha kwamba sio tu unakwenda na wakati bali unapata ideas mpya mpya za show nk?

MM: Kama nilivyogusia hapo mwanzo, siri yangu kubwa ni kuangalia kwa makini show za wengine zinafanywaje. Namuangalia mtu kama Oprah,Tyra, Monique, Hellen etc ili kupata mtazamo tofauti na ili niweze kuboresha show yangu kila mara. Sidhani kama ni lazima sana kusoma sana vitabu kwa sababu inategemea na aina ya show uliyonayo au unayoifanya.

BC: Mbali na hii venture mpya ya kuwa Host wa TV show, wewe ni mjasiriamali. Siku hizi, kama tunavyoona, wanawake wengi zaidi nao wanaingia kwenye ujasiriamali. Una ushauri gani kwa wanawake wenzio kuhusiana na ujasiriamali?

MM: Kwanza lazima ujue hiki kitu ” Fanya kitu ambacho unakipenda na unakiweza. Wanawake wengi tunakurupuka kwenye ujasiriamali na wakati hatuuwezi. Watu wanafanya kama fashion. Let’s say mimi napenda kuwa na Boutique kwa sababu napenda fashion na ninaimudu.Haya sasa nina talk show kwa sababu naipenda na ninaimudu. Kwa hiyo wanawake wenzangu, tujaribu kufanya kitu ambacho tunakipenda na kukimudu. Ni rahisi zaidi kufanikiwa ukiwa na hayo mambo mawili. Mapenzi kwa kitu unachokifanya au kutaka kukifanya na uwezo wa kukifanya.

BC: Mwisho una ujumbe gani mahususi kwa watanzania? Na pia kwanini mtu achague kuangalia The Mboni Show badala ya show zingine lukuki kwenye luninga?

MM: Ujumbe kwa watanzania wenzangu “Tupende vya kwetu, tuthamini vya kwetu, Tupendane na tushirikane. Kama unaona una connection na wewe huna uwezo nao ila kuna mwingine anaweza basi msaidie na sio kubaniana na kuoneana vijiba vya roho bila sababu za msingi.. Na pia tupende kusifiana. Mwenzako kafanya kizuri basi mpe hongera zake na kama kakosea basi muelekeze( muongoze). Ha ha ha ha Trust me The Mboni show iko kitofaut kabisa na zile tulizozizoea.  Kwenye The Mboni show unapata kila kitu. Full package ha ha ha ha.

Kwa mengi zaidi unaweza kutembelea tovuti rasmi ya The Mboni Show katika www.thembonishow.com.

Monday, December 26, 2011

MANENO OSWARD VS RASHIDI MATUMLA AKUNA MBABE POINT 99 KWA 99 DROO

Bondia Rashidi Matumla (kushoto) akiwa chini baada ya kuteleza uku mpinzani wake Maneno Osward akimsubili kwa ajili ya kumpiga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.

Bondia Rashidi Matumla (kushoto) akiwa chini baada ya kuteleza uku mpinzani wake Maneno Osward akimsubili kwa ajili ya kumpiga wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.

Bondia Rashidi Matumla (kushoto) na Maneno Osward wakioneshana ufundi wa kutupa masumbwi wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.

Bondia Maneno Osward (kushoto) akimuacha Rashidi Matumla chini baada ya kuanguka kwa kuteleza wakati wa mpambano wao uliofanyika Dar es salaam jana wakati wa sikukuu ya Xmasi mpaka mwisho wa pambano point ni 99 kwa 99 hivyo kuwa droo.(Picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com)

Thursday, October 20, 2011

KAMBI YA MAFUNZO MPIRA WA KIKAPU KUMALIZIKA LEO JIJINI MWANZA

Kocha Twalib Puzo akitoa maelezo kwa washiriki (hawako pichani) kuanzia kushoto ni Iddy Zuberi, Sosho Kizito, Twalib Puzo, Vicent Shinde katika mafunzo ya mpira wa kikapu kwa vijana walio chini ya umri wa miaka 18 kutoka katika shule mbalimbali za sekondari jijini mwanza, yakiendelea kufanyika katika uwanja wa CCM Kirumba na yanatarajiwa kumalizika leo saa 10 jioni katika uwanja huu.

Mafunzo hayo yameandaliwa na kusimamiwa na Shirika la kijamii la Planet Social development (PSD) la jijini Mwanza pamoja na Mambo Basketball kutoka Dar es Salaam yamejumuisha jumla ya vijana 81 ikiwa wavulana ni 68 na wasichana ni 13.

Mafunzo hayo yalikuwa na malengo yafuatayo:
1.Kuangalia vipaji na jinsi ya kuviendeleza katika kusaidia maendeleo ya mchezo huu hapa Tanzania ambao ni wito wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania (TBF).
2.Kupata na kutoa picha halisi kwa wachezaji ikiwa ni sehemu ya mafunzo tutakayoyafanya mwakani kwa kushirikiana na kocha wa Basketball program ya Memorial Newfound University kutoka Canada. Hii ni baada ya mafunzo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam mwezi wa saba mwaka huu ambapo kijana wa ki Tanzania Alphaeus Kisusi alifanikiwa kupata “Partial Scholarship” kwenda kusoma katika chuo hicho.
3.Kubadilishana uzoefu na makocha wa mchezo huu hapa mwanza katika kuendesha mafunzo kama haya kwa siku zijazo.
4.Kuendeleza ushirikiano wa vikundi vyetu (Mambo Basketball na PSD) katika kutekeleza malengo tuliyojiwekea kama US Sports program Alumni baada ya safari yetu ya mafunzo nchini Marekani mwaka 2009 iliyogharamiwa na Ubalozi wa Marekani – Tanzania.

Washiriki kwenye training.

Mafunzo haya yanatarajiwa kufungwa na Rais wa shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania ndg. Mussa Mziya akiambatana na mlezi wa vijana katika chama cha mpira wa kikapu Mkoa wa Mwanza ndg Altaf H. Mansoor “Dogo”

Thursday, June 9, 2011

Shhhhhhhhhhh, ITAFAHAMIKA TU MUDA SI MREFU!!!!

Kuna tetesi kuwa huyu mjamaa kutoka the gunners Arsenal ya pale Emirates Uingereza huenda akatua Manchesta Yunaited, teh teh teh, kocha wake Arsene Wenger hataki kumuweka sokoni na hasa kwa mashetani hao wekundu, ila ye mwenyewe sasa msikie hapa akihojia na TF1 Telefoot huko kwao Ufaransani-"Do I want to go to Man United? Initially, we should see if it's real and if it is concrete." MMMMh!

Imelipotiwa kuwa Arsenal imeshindwa kumshawishi nahodha Cesc Fabregas kubaki,na badala yake anaonekana siku zake zimewadia kurudi klabu yake ya zamani Fc Barcelona.
Meneja wa washika bunduki Arsene Wenger amemruhusu kuondoka lakini haruhusiwi kujiunga na vilabu vya England.

Saturday, May 7, 2011

MOURINHO APEWA ADHABU

Kocha wa Real Madrid Jose Mourinho amepewa adhabu ya mechi tano kwa mechi za Ulaya, kutokana na matukio wakati wa nusu fainali ya kwanza ya ligi ya mabingwa Ulaya, dhidi ya Barcelona.Chama cha soka Ulaya, UEFA, kimesema Mourinho alitoa matamshi "yasiyofaa", baada ya Real Madrid kufungwa 2-0 na Barcelona, akiwatuhumu waamuzi kwa kujaribu kuisaidia Barcelona.

Mourinho tayari ametumikia adhabu ya mchezo mmoja kukaa jukwaani, katika mchezo wa pili, na michezo mingine mitano itatekelezwa iwapo atafanya makosa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

UEFA pia imemfungia kutocheza mchezo wa fainali kipa wa Barca wa akiba Jose Pinto.

Thursday, November 11, 2010

FIFA YAMUONGEZEA PESA OBILALE WA TOGO.

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Togo Kodjovi Obilale atapatiwa dola100,000 kutoka Shirikisho la Soka Duniani- Fifa baada ya kujeruhiwa vibaya kwa risasi kabla ya kuanza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola mwezi wa Januari.
KODJOVI OBILALE.
Rais wa Fifa Sepp Blatter, alimwambia Obilale mwezi wa Septemba kwamba malipo ya dola 25,000 zitatolewa kutoka mfuko wa Fifa wa misaada ya kibinadamu.

Hata hivyo Shirikisho hilo la soka Duniani kwa sasa limeamua kuongeza kiwango hicho cha pesa.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 alifanyiwa upasuaji kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa mgongoni na tumboni kufuatia shambulio hilo.

Shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Cabinda nchini Angola, lilisababisha watu wawili waliokuwemo katika kikosi cha Togo kupoteza maisha pamoja na dereva wa basi lililokuwa limewachukua.

Obilale bado hawezi kutembea ikiwa ni miezi minane tangu lilipotokea shambulio la risasi lililofanywa na waasi wanaotaka kujitenga kwa jimbo la Cabinda na bado anaendelea kutibiwa nchini Ufaransa.

Togo ilijitoa katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola baada ya shambulio hilo na ilifungiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) kwa miaka minne kushiriki mashindano hayo.

Hata hivyo Fifa ilitengua adhabu hiyo.

Akiwa amekatishwa tamaa kwa kukosa msaada kutoka Caf na Angola ambao waliandaa mashindano hayo, Obilale alimwandikia barua Rais wa Fifa Blatter mwezi wa Agosti akimuomba msaada.

Blatter akamuahidi msaada kutoka mfuko huo wa Fifa wa misaada ya kijamii, pamoja na kumueleza Fifa haina dhamana na mashambulio ya Cabinda.

Obilale alieleza hadhari kukatishwa tamaa kwa kukosa msaada wa Caf na maafisa wa Angola baada ya shambulio hilo ambalo limekatisha matumaini yake ya kucheza soka.

Mlinda mlango huyo aliyekuwa akichezea klabu moja ya daraja la chini huko Ufaransa, hawezi kusogeza mguu wake wa kuume chini ya goti, pia mguu wake umekufa ganzi, lakini ana matumaini ataweza kutembea siku za baadae.

Kwa sasa anatumia kiti maalum cha kutembelea kuzunguka hapa na pale na amesema angekuwa na jina kubwa katika soka, basi matibabu yake yangekuwa tofauti na anayopatiwa sasa..

TOTTENHAM SARE YA 1-1 NA SUNDERLAND.

Asamoah Gyan alifuta furaha ya bao la Rafael van der Vaart wakati Sunderland ilipoinyima ushindi Tottenham katika uwanja wake wa nyumbani wa White Hart Lane.
Spurs walikuwa wakijitahidi kuipenya ngiome imara ya Sunderland katika kipindi cha kwanza, huku Tom Huddlestone akiachia mkwaju uliopiga mwamba kutoka umbali wa yadi 25.

Walifanikiwa kupata bao la kuongoza wakati Gareth Bale alipomimina krosi kutoka upande wa kushoto na baada ya Peter Crouch kuurudisha kwa kichwa karibu na lango, Van der Vaart akautuliza na kuujaza kimiani.

Sunderland walisawazisha wakati Gyan alipotumia makosa ya walinzi wa Tottenham kupachika bao la kusawazisha na kujipatia pointi moja.

Kwa matokeo hayo Tottenham wameendelea kusalia nafasi ya sita wakiwa na pointi 16 na Sunderland wapo nyuma yao nafasi ya saba wakiwa na pointi sawa 16.

Thursday, October 28, 2010

FIFA YATUMA RAMBI RAMBI KENYA.

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa amesikitishwa na yale yaliyofanyika siku ya Jumamosi usiku katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo mjini Nairobi,tukio lililosababisha vifo vya watu saba na wengine wengi kujeruhiwa.

"Napenda nieleze kusikitishwa kwangu na napenda nitangulize rambi rambi zangu kwa mashabiki wa soka nchini Kenya,na zaidi kwa jamii na marafiki kufwatia vifo hivi," alisema Rais wa FIFA.

"Nafahamu kwamba uchunguzi umeanzishwa. Lazima juhudi zifanywe ili chanzo cha tukio hili baya kijulikane kwa nia ya kuzuia hali hii kutokea kwenye uwanja wa Nyayo tena."

Ni hapo Jumatatu tu, ambapo FIFA ililitaka shirikisho la soka nchini Kenya FKL kuelezea mazingira, yaliyosababisha mkasa huo kutokea.

Shirikisho la FKL, limepiga marufuku mechi zozote kufanyika katika Uwanja wa Nyayo na ule wa City, hadi watimize masharti ya usalama kuambatana na kanuni za FIFA.

Mkasa huo wa Jumamosi ulitokea wakati mashabiki wa mahasimu wa jadi AFC Leopards na Gormahia waking'ang'ana kuingia uwanjani.

Ilikuwa ni katika pambano la ligi ya kitaifa.

Monday, September 27, 2010

Frank Lampard kukosa mechi muhimu

Frank Lampard atakosa michezo muhimu kwa timu yake ya Chelsea na timu ya taifa ya England kutokana na kuendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa ngiri.

Lampard mwenye umri wa miaka 32 hajaichezea klabu yake kwa mwezi mmoja na meneja wake Carlo Ancelotti amethibitisha kiungo huyo hataweza kucheza kwa takriban wiki mbili zijazo.

Kipindi hicho atakosa mechi dhidi ya Marseille, Arsenal na mchezo wa kufuzu mashindano ya Euro 2012 wakati England itakapopambana na Montenegro.

Ancelotti ameendelea kusema, Lampard hawezi kucheza kwa sasa, wanahitaji muda zaidi tofauti na walivyotazamia.

Kwa vile hajaichezea Chelesea, Ancelotti amesema vile vile hatakuwa tayari kuichezea timu ya taifa.

Lampard alirejea mazoezini baada ya kufanyiwa upasuaji tarehe 31 mwezi wa Agosti, lakini amekuwa akisumbuliwa na maumivu kwenye kovu.

Tayari amekosa mechi za England walizoshinda za kufuzu michezo ya Euro 2012 dhidi ya Bulgaria na Switzerland mapema mwezi wa Septemba na pia atakosa mechi dhidi ya Montenegro katika uwanja wa Wembley tarehe 12 mwezi wa Oktoba.

Mara ya mwisho kuichezea Chelsea ilikuwa tarehe 28 mwezi wa Agosti timu hiyo ilipoifunga Stoke mabao 2-0.

Monday, September 6, 2010

KASHFA YA KUPANGA MATOKEO YA KRIKETI UINGEREZA.

Gazeti moja la Uingereza limetoa madai mapya kuhusu kashfa ya kupanga matokeo ya mechi inayomhusisha mchezaji cricketi wa Pakistan.

Gazet hilo, The News of the World linadai Baraza la Kimataifa la Cricket -lCC-linamchunguza mchezaji huyo, ambaye jina lake halikutajwa kwa sababu za kisheria.
Baraza la ICC limesema haliwezi kutoa taarifa yoyote juu ya uchunguzi unaondelea.

Hatua ya kupanga matokeo ya mechi ni nzito kuliko madai yaliyotolewa na gazeti hilo wiki iliyopita.

Gazeti hilo lilifichua kashfa ya kamari ambayo ilisababisha wachezaji watatu wa timu ya Pakistan kusimamishwa na wanafanyiwa uchunguzi na Baraza la Kimataifa la Cricketi pamoja na polisi.