Monday, September 27, 2010

Frank Lampard kukosa mechi muhimu

Frank Lampard atakosa michezo muhimu kwa timu yake ya Chelsea na timu ya taifa ya England kutokana na kuendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji wa ngiri.

Lampard mwenye umri wa miaka 32 hajaichezea klabu yake kwa mwezi mmoja na meneja wake Carlo Ancelotti amethibitisha kiungo huyo hataweza kucheza kwa takriban wiki mbili zijazo.

Kipindi hicho atakosa mechi dhidi ya Marseille, Arsenal na mchezo wa kufuzu mashindano ya Euro 2012 wakati England itakapopambana na Montenegro.

Ancelotti ameendelea kusema, Lampard hawezi kucheza kwa sasa, wanahitaji muda zaidi tofauti na walivyotazamia.

Kwa vile hajaichezea Chelesea, Ancelotti amesema vile vile hatakuwa tayari kuichezea timu ya taifa.

Lampard alirejea mazoezini baada ya kufanyiwa upasuaji tarehe 31 mwezi wa Agosti, lakini amekuwa akisumbuliwa na maumivu kwenye kovu.

Tayari amekosa mechi za England walizoshinda za kufuzu michezo ya Euro 2012 dhidi ya Bulgaria na Switzerland mapema mwezi wa Septemba na pia atakosa mechi dhidi ya Montenegro katika uwanja wa Wembley tarehe 12 mwezi wa Oktoba.

Mara ya mwisho kuichezea Chelsea ilikuwa tarehe 28 mwezi wa Agosti timu hiyo ilipoifunga Stoke mabao 2-0.

No comments:

Post a Comment