Sunday, July 14, 2013

ANGALIA PICHA ZA BEHIND THE SCENE ZA VIDEO MAKING YA UDE UDE (Ngoma Inogile) NDANI YA BILICANAS ( MUCH MORE)

Bata huku video inaendelea


Director Pablo & Video queen


Pablo @ work


Pablo,Nancy & Equ junior


Pablo,queen dalin & Ude ude


Queen dalin akiinuka kwenda kutoa maelekezo kwa Ude ude


Ude ude & video queens on set


Ude ude @ work


Ude ude akiwa na mtoto mzuri


Videos queen


Videos queens on set
Msanii (Star) wa muziki wa kizazi kipya ambaye yupo chini ya BABUU KISAUJI (UDE UDE) Ambaye alikua kimya kidogo sasa kaamua kurudi na zote baada ya kuingia mkataba na BABUU KISAUJI ENTERTAINMENT kwa mujibu wa majibu yakebaada ya mahojiano nae. Hizi ndio picha za behind the scene ya video yake mpya iitwayo NGOMA INAGILE  ambayo Imefanywa na APEX ENTERTAINMENT PRODUCTION chini ya director PABLO ndani ya Bilicanas (Much More) Siku ya tarehe 08-07-2013.

MBUNGE WA MUSOMA MJINI PAMOJA NA MEYA WASHIRIKI MAZISHI YA HUPHREY SIMON MKOANI MARA

Padre akiongoza ibada kumuombea marehemu Humphrey Simon iliyofanyika jana nyumbani kwao Makoko Musoma mjini. 

Mbunge wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere (katikati mwenye suti nyeusi) alihudhuria ibada hiyo sambamba na mazishi.

Waumini walishiriki meza ya bwana katika ibada hiyo ya kumuombea marehemu.

Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisusura akishiriki meza ya bwana.

Mmoja ya viongozi wa kampuni ya mawasiliano ya tigo akishiriki meza ya bwana.

Kusanyiko kwenye ibada nyumbani.

Mama Nyimbo akiongoza safu ya akinamama wenzake katika utoaji heshima za mwisho kwa mwili wamarehemu.

Sambamba wananchi wengine Mbunge wa Musoma Mjini Vicent Nyerere akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Mashangazi na ndugu wa karibu wa marehemu wakitoa heshima za mwisho 

Heshima za mwisho zilikoma kwa safu ya wanaume kufunga zoezi hilo.

Kisha safari ya kuelekea makaburini eneo la Makoko Musoma mkoani Mara ikafanyika.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Tigo ambao wanafanya kazi na mke wa marehemu walitoa sapoti ya kutosha katika shughuli nzima za mazishi, hata wengine walidiriki kusafiri toka mikoa mbalimbali ili kuwakilisha.

Mwili wa marehemu Huphrey Simon ukiwa kwenye nyumba yake ya milele.

"Uliumbwa kwa udongo na mavumbini utarudi"

Mke wa marehemu Bi. Neema akiweka udongo kwenye kaburi la mumewe.

Mke wamarehemu akiweka shada la maua.

Mjomba wa marehemu Mr. Tega akiwa na shangazi wakiweka shada la maua.

Shangazi wa marehemu.

Mbunge wa Musoma mjini Mhe. Vicent Nyerere akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Humphrey.

Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisusura akiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Humphrey.


Mtoto wa marehemu akiweka shada la maua. 
Picha ya pamoja ya wanandugu akiwepo mke wa marehemu (wa 3 kutoka kushoto) mbele ya kaburi .

Mtoto wa marehemu Huphrey Simon akiweka shada la maua juu ya kaburi la baba yake.

Marafiki wa marehemu.

Jina la bwana lihimidiwe.

Tuesday, April 2, 2013

PASAKA GOSPEL FESTIVAL 2013 ILIVYOFANA MWANZA




Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani akifungua utepe wa gitaa kuashiria uzinduzi wa Studio mpya za kurekodi muziki za COSU Studio zilizozinduliwa ndani ya tamasha la Muziki lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival ambalo nalo limeanzishwa rasmi mwaka huu jijini  Mwanza.


Nesta Sanga ni moja kati ya waimbaji waliosisimua ndani ya Gospel Festival tizama watu wa Mungu walivyomzunguka wakiimba naye. 




Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula akifurahia yanayoendelea na Askofu Simeone Masunga wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God Geita katika sherehe za Pasaka ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival lililofanyika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kwaya mbalimbali na waimbaji toka pande nyingi nchini walihusishwa.


Mwimbaji wa nyimbo za injili anayetamba Afrika Mashariki na Kati Neema Mwaipopo akiiimba wimbo wa 'Raha jipe mwenyewe' na wakazi wa Mwanza waliofurika uwanja wa CCM Kirumba kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013.


Waimbaji mbalimbali toka mikoa ya Dar es salaam, Manyara, Arusha, wakimpa sapoti mwimbaji Neema Mwaipopo kwenye kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013 lililofanyika sikukuu ya Pasaka uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. 


Hapa raha ya ufufuko ilimvuvia kila mmoja.


Mwimbaji nesta Sanga  akiimba wimbo ujulikanao kwa jina Twendeni huku akipewa sapoti ya kutosha.
Sura za watumishi wa muziki wa Injili zikiranda huku na huko kudadisi yanayoendelea.


Ni cheki ya 500,000/= toka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Mkolani Investiment (katikati) Suleiman Nguvu kuchangia uboreshaji wa vitendea kazi ndani ya studio za kisasa za COSU Studio ndani ya Kusanyiko la Pasaka Gospel Festival 2013. Kushoto ni Mkurugenzi wa COSU Entertainment Fabian Fanuel (red tshirt) na Meneja wake Albert G. Sengo (kulia)


Wananchi hawakupitwa na shughuli za uwekaji kumbukumbu.

Jamani rahaaaaaaaa....Ndiyooooo....


Moja ya kwaya za jijini Mwanza zikihudumu.


Mwimbaji anayesisimua katika muziki wa injili akitamba na wimbo 'Zunguka' Enock Jonas akishusha upako...


Meza kuu ikijadili jambo.


Zunguka, zunguka, zunguka, zunguka eeeeeeeeeh!!!!!


Ilibidi muda usogee hata kiza kikaingia, tunamshukuru Mungu shughuli katika uwanja huu kwa kweli ilifana. Shukurani za dhati kwa Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula, Mbunge wa Monduli Edward Lowassa (twafahamu ni majukumu tu yamesababisha ukashindwa kuhudhuria), Mkurugenzi wa Sahara Media Group Dr. Anthony Diallo,  Michuzi Jr Blog na Kajunason Blog.