Monday, July 6, 2015

CHANGAMOTO ZA WALEMAVU NDIYO SABABU KUBWA YA WASTARA KUINGIA KWENYE SIASA

Changamoto za Walemavu Ndiyo Sababu Kubwa ya Wastara Kuingia Kwenye Siasa Naitwa Wastara Juma kama watanzania wenzengu mnavyonifahamu mimi ni muigizaji wa filamu na kazi nyingine zinazohusiana na kiwanda cha filamu. 

Leo niongee kitu ili watanzania wenzangu muelewe kwanini nimeamua kujiingiza kwenye siasa, kikubwa kilichonisukuma kuingia kwenye siasa ni jambo moja kubwa sana kwangu ambalo ni (WALEMAVU) .

 Huwezi kusimulia uchungu wa mwana wakati haujawahi kuzaa huwezi kumzunguzia au kumtetea mlemavu hali ya kuwa hujui uchungu, matatizo na maumivu yake,, Mpaka sasa nimeishi katika hali ya ulemavu kwa zaidi ya miaka 6 japo kuna wengine wamezaliwa wakiwa walemavu lakini kwa mda mchache tu miaka 6 nimepata mateso makubwa sana kuanzia kimaisha, kisaikolojia na hata kimiundombinu ya nchi yetu. 

Pamoja na umaarufu wangu wote lakini hakuna shirika wala taasisi yoyote iliyowahi kunishika mkono japo jambo hili halikuwa muhimu sana kwangu kwani naweza kujihudumia mimi na familia yangu. 

Jambo la muhimu kwa sasa na linaloniumiza sana ni kuona ndani ya nchi yetu walemavu hawana thamani wala haki yoyote si Mahosptalini, Maofisi ya Kiserikali, ndani ya vyombo vya Usafiri, makazini na hata majumbani. Labda moja tu ndio nimeona walemavu wamepewa nafasi angalau ya kupita kuelekea sehemu au kuingia na kukaa ni ndani ya jengo la Bunge tu hapo Dodoma. 

Ndani ya nchi yangu walemavu wote tunachukuliwa kama ombaomba na hali hii imewakatisha tamaa walio wengi mpaka kuamua kuingia mitaani na kuzunguka wakiomba shilingi mia mia za kujikimu kimaisha. Naumia sana napojitizama mimi na kufikiria je leo hii nisingekuwa maarufu ningeishi maisha gani? Napata jibu kuwa huenda na mimi ningetafuta kijana akanikokota na baiskeli na kuanza kuzunguka mitaani kuomba omba.

 Siamini kabisa kama kweli ukiwa mlemavu na akili yako pia inalemaa la hasha bali naamini kuwa serikali yetu haitutazami walemavu kama na sisi tuna haki sawa na wengine na tunastahili kujumulishwa na kila kitu wanachipata wasio na ulemavu. Kuanzia kielimu, kiafya, miundombinu na sehemu nyinginezo. 

Leo hii ni aibu kubwa kuwa hata television ya taifa inayotoa taarifa ya habari kwa nchi haina mtangazaji anae wahabarisha walemavu viziwi ambao nao wanahaki ya kujua nchi yetu na yaliyojiri.

 Leo hii ni aibu zinajengwa barabara lakini hazima sehemu ya kupita walemavu  Leo hii ni aibu kuona shule nyingi za ulemavu kwanza ni za zamani halafu hakuna hata vifaa vinavyoendana na dunia ya kisasa ya sayansi na teknolojia Ni aibu kuona hatuna viwanja vya michezo kwa walemavu wakati na sisi tunahaki ya kushiriki hata mashindano ya Paralimpic.

 Nimejaribu kuonyesha na kuwapigania walemavu wenzangu kupitia sanaa lakini nimeona sauti yangu ni ndogo na haisikiki kokote sasa nimeamua kuingia kwenye siasa ili nisamame na kuwapigania Walemavu wenzangu wasio na sauti nao sawa na kuona machozi, maumivu na mateso yao nayafuta vipi.

Pia ili niweze kufuta kiapo nilichoweka kwenye nafsi yangu baada ya kuona tunapokelewa vibaya ndani ya nchi yetu wenyewe kwamba lazima siku moja nitawapa furaha walemavu wenzangu kabla sijafa nitapigania haki zao za msingi ili nao au tujione tuna haki sawa na wengine nimekaa na dukuduku hili ndani ya miaka 5 sasa huu ni wakati wa kulitoa na kujitoa kwa nguvu zangu zote kuhakikisha walemavu wanawekwa katika mazingira mazuri kama nchi za wenzetu waishi vizuri na kufikia hata nusu yake tu basi nitakuwa nimefikia lengo la kutetea haki za msingi kwa walemavu wenzangu sababu hata mim ni muhanga nimetumia lugha nyepesi ili nieleweke sina tamaa ya chchote ila sitakuwa sawa kufa bila kuwaweka wenzangu kwenye maisha ya haki na sehemu sahihi kwa sasa kuonyesha nilichohahidi moyo wangu ni bungeni najua kma si wewe uliyelamaa basi ndugu rafiki jirani yako lazima atakuwa kwenye hali hii hivyo watanzania kutumia nguvu zetu kunisuport amtapoteza kitu bali mtaongeza msaada kwa wale wasijioweza asante kwa kusoma ujumbe huu Wastara Juma on Instagram 

No comments:

Post a Comment