Sunday, July 19, 2015

VIJANA CCM WAJITOKEZA KWA WINGI KUCHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA MOSHI MJINI

Mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini,Priscus Tarimo,akikabidhiwa fomu ya nafasi hiyo na katibu wa CCM manispaa ya Moshi,Loth Ole Nesele katika ofis za chama hicho za Wilaya ya Moshi mjini.
Mtia nia ya kugombea Ubunge jimbo la Moshi mjini,Priscus Tarimo,akitoa maelezo yake kwa Katibu Msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi mjini Donatha Mushi alipofika kwa ajili ya zoezi la uchukuaji wa fomu.
Priscus Tarimo akizungumza na na wanahabari( hawako pichani) muda mfupi baada ya kumaliza zoezi la uchukuaji wa fomu za kuwania kuteuliwa katika nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM jimbo la Moshi mjini.
Naibu kamanda wa Vijana wa CCM,manispaa ya Moshi ,Edmund Rutaraka akipokea fomu ya kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho kutoka kwa katibu msaidizi wa CCM wilaya ya Moshi mjini,Donatha Mushi.
Kada wa Chama cha Mapinduzi manispaa ya Moshi ,Daudi Mrindoko akiwa ameambatana na mkewemalipofika kucukua fomu katika ofisi za CCM wilaya ya Moshi mjin,Fomu hizo zilikabidhiwa kwake na katibu msaidizi wa chama hicho Donatha Mushi.
Mwakilishi wa jamii ya Bantu Union ,Omary Mwaliko akirejesha fomu za kuwania kuteuliwa nafasi ya Ubunge katika jimbo la Moshi mjini mara baada ya kuzijaza

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment