Wednesday, July 15, 2015

RUGEMALILA RUTATINA ATANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJINI

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Rugemalila Rutatina akifafanua jambo wakati wa mkutano maalumu ulioandaliwa kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania kugombea nafasi ya ubunge kupitia tiketi ya CCM katika jimbo la Kibaha mjini   kwenye ukumbi wa  country side mjini Kibaha  kulia kwake ni mwenyekiti ccm tawi la sheli Yassin Mudhihili (Picha na Victor Masangu) BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

VICTOR MASANGU, KIBAHA PWANI

BAADA chama cha mapinduzi CCM kumaliza mchakakato mzima wa kumteuwa John Pombe Magufuli kupeperusha bendera ya CCM  kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Octoba 25 mwaka huu joto kwa sasa limeamia katika nafasi za wabunge pamoja na madiwani.
Katika kuelekea uchaguzi huo mkuu mumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Rugemalila Rutatina ameamua kujitokeza kutangaza nia yake ya kugombea ubunge kupitia tiketi ya CCM katika jimbo la Kibaha mjini.
Rutatina ambaye ametangaza nia yake rasmi hapo siku ya jana katika ukumbi ya Country side uliopo kibaha kwa lengo la kuweza kuleta ukombozi na mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wananchi wa jimbo la kibaha mjini.
Rutatina katika hotuba yake katika mkutano huo ambao ulihudhuriwa na umati wa wananchi kutoka maeneo mbali mbali ya Wilaya ya kibaha uliweza kuvuta hisia kubwa kutokana na hotuba yake ambayo iliweza kugonga na kugusa maslahi ya wananchi wenyewe na sio kwa manufaa na mtu mmoja.
Katika hotuba yake Rugemalila alisema kwamba amemua kujikita kutangaza nia ya kugombea jimbo la kibaha mjini kutokana na kuona hakuna msukomo wowote wa maendeleo kwa muda mrefu katika jimbo hilo hivyo akipata fursa yaa kuwa mbunge atashirikiana bega kwa bega ili kuweza kuleta maendeleo na sio vinginevyo.
Alisema kwamba katika jimbo la kibaha mjini kitu kingine kikubwa kilichoweza kumsukuma na kuona vijana wengi wanaoshi katika eneo hilo hawana ajira jivyo wamekuwa wakipata shida kubwa katika kupata fedha amabzo zitaweza kuwasaidia kujiendeleza katika shughuli zao mbali mbali za ujasilimali.
Pia aliongeza kuwa kitu kingine ni kwamba katika eneo la mjini wa kibaha kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakitata usumbufu mkubwa kutokana na miundombinu yake kuwa mibovu hivyo kujikuta wanashindwa kufanya shighuli zao za kimaendelea kwa muda wa muafaka.
Mjumbe huyo wa halmashauri kuu alifafafanua kuwa pia jimbo la kibaha mjini limekuwa katika wakati mgumu sana kwani wananchi wake wanapata shida ya kupata mahitaji yao muhimu kwani hakuna soka  la kisasa pamoja na stendi kitu amabcho amedai akiingia madarakani ataweza kuhakikisha analivalia njuga suala hilo ili kuweza kuwapa fursa wananchi wake kupata mahitaji yote muhimu kwa urahisi.
Aidha alisema kwamb avipaumbele vyake atakavyovifanya pindi atakapochaguliwa na wananchi katika jimbo hilo la kibaha mjini atahakikisha anawapa ajira vijana wa kibaha kupitia fursa mbali mbali zilizopo, pamoja na kuimarisha miundombinu ya baarabara pamoja na kujenga stendi ya kisasa pamoja na soko.

No comments:

Post a Comment