Thursday, May 17, 2012

PATRICK MAFISANGO OF SIMBA SC IS DEAD

Marehemu Patrick Mafisango (kwenye kiduara) katika picha ya pamoja na kikosi cha Simba enzi za uhai wake.
Mchezaji wa Simba na timu ya Taifa ya Rwanda kiungo mkabaji Patrick Mafisango amefariki dunia kwa ajali ya gari leo alfajiri katika eneo la Tazara jijini Dar es salaam.
Hili ndilo Gari alilopatanalo ajali marehemu Patrick Mafisango maeneo ya TAZARA jijini Dar.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba bwana Aden Rage amesema kuwa taarifa za awali juu ya chanzo cha kifo cha mchezaji huyo zinasema kuwa mchezaji huyo amekutwa na mauti akiwa anaendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki.

Msiba huu unakuja wakati kocha wa timu ya Taifa ya Rwanda Milutin Sredovic 'Micho' akiwa amemteuwa kepteni wa zamani wa timu hiyo Hamada Ndikumana a.k.a 'Katauti' na Patrick Mafisango kujiunga na timu ya taifa hilo (AMAVUBI) kwaajili ya maandalizi ya nchi zitakazofuzu kwenda Brazil kwenye michuano ya Kombe la dunia 2014.

Kabla ya  kuichezea Simba mchezaji huyo alitokea Azam Fc ya jijini Dar es salaam.
Patrick Mafisango is dead.
Mwenyezi Mungu ilaze mahali pema peponi roho ya marehemu Patrick Mafisango.

No comments:

Post a Comment