Tuesday, June 28, 2011
VINJARI ZA MSIMU WA DHAHABU JIJI LA SANGARA
Wednesday, June 22, 2011
ZIMEBAKI SIKU TANO TU! HAINA MAJOTROOOOO!!!!

Wakazi wa Rock City wameonekana katika pilika za huku na huko madukani kujinunulia mavazi kuhakikisha kuwa wanashaini ile kisawasawa kuilaki burudani ya kweli ile hali upande wa watoa huduma mbalimbali iwe za mahoteli, malazi, chakula, wadau wa usafiri maduka ya mavazi na kadhalika wao wameahidi kutoa huduma safi katika kipindi hiki cha matayarisho hata kwa siku husika.
Tuesday, June 14, 2011
'SERENGETI FIESTA 2011 MWANZA NDIYO KWANZA'

MBONA tayari imekwisha tambulikaaaa kwambaaaa.... Serengeti Fiesta 2011 'Mwanza ndiyo kwanza'. Nina maaanisha kuwa wakazi wa Mwanza ndiyo wamekabidhiwa funguo za Show za 'kufufuka mtu' za msimu wa Dhahabu na Serengeti Fiesta.
Dhamana hii haijaja hivi hivi mwanawane' bali ni kutokana na utashi, mapenzi mema na makaribisho yenye thamani ya hali ya juu wayatoayo wakazi wa Rock City na Wilaya zake kwenye matukio ya Fiesta miaka yote....
Wakazi wa Mwanza husapoti muziki ladha zote, lakini jiulize ni muziki gani ulianza kushika kwa kasi na kukubalika hata leo na kuwarusha wengi!!!?
Wataalamu wa mambo watakwambia.. Ni Ragga, Dancehall na Reggae (ingawa reggae kilimanjaro grafu zinasoma juu kinoma) Tehe!! Lakini ukizungumzia Dancehall na Ragga->Mwanza ni Nowmaaaa!!!
SASA ANAKUJA MKALI WA RAGGA & DANCEHALL
Mr. Lover-lover/Mr. Romantic & Fantastic true jamacian rasta ilve ur music 'Shaggy' anatua Mwanza, siku ya Tukio ikiwa ni JUMAPILI ya tarehe 26juni2011 katika Uwanja wa CCM Kirumba uliopo wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
It's nice and cool man, Shaggy Welcome to Mwanza!!..........
Coz Mwanza Haina Majotrooo!!,
@ g.sengo
HATIMAYE MOYO WANGU YA PHILBERT KABAGO YATINGA SOKONI!!!
Mkali wa michano kutoka The Rock City Mwanza, ambaye vilevile ni prizenta wa Passion Fm, Philbert Kabago ameshusha rasmi mtaani kitu cha album. Blogu hii imefanikiwa kuchonga na mshtaa' na hiki ndicho alichosema- "Album imetoka rasmi, so na hii ni baada ya kuwa katika maandalizi makubwa, nimeamua kuiachia album hii yenye jina 'Moyo wangu' ikiwa na ngoma kibao za ukweli kama vile 'Dear', 'Moyo wangu' ambayo imebeba jina la album, 'mama' alioimba kumuenzi marehemu mama yake, wivu, 'Umeme wa mgao' ambayo ndio inayotamba kwa sasa kwenye baadhi ya vituo vya radio n.k"
Kuhusu wasanii aliowashirikisha katika album hiyo jamaa amefunguka kwa kusema kuwa ni pamoja na Farida, MB Dog, Mr hill, Hussein machozi, G.Sengo na wengine wengi. Album imefanyika katika studio mbalimbali zikiwemo Tetemesha Records, Mo Record za mwanza na Family studio Arusha! Wasambazaji ni GMC.
Thursday, June 9, 2011
Shhhhhhhhhhh, ITAFAHAMIKA TU MUDA SI MREFU!!!!

Imelipotiwa kuwa Arsenal imeshindwa kumshawishi nahodha Cesc Fabregas kubaki,na badala yake anaonekana siku zake zimewadia kurudi klabu yake ya zamani Fc Barcelona.
Meneja wa washika bunduki Arsene Wenger amemruhusu kuondoka lakini haruhusiwi kujiunga na vilabu vya England.
THUG LOVING!

WAPI KUFULI FAZA?
Subscribe to:
Posts (Atom)